Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha

Acha chuki... zitakuua kabla ya siku zako!

Na huu upumbavu ndio unagawa watu kwenye kutetea maslahi ya taifa!!..
Punguza munkari kiongozi. JF hawa watu wapo tu. Wakati wa Magu kuna ID zilikuwa critical wakati zilikuwa supportive kwa Jakaya. Na kuna ID zilikuwa critical kwa Jakaya lakini kipindi cha Pombe zikawa supportive. Hata sasa kuna ID tulizisahau zinaibuka na kumpa support mama na wengine wamemgeuka Makamu wao wa few months ago.

Hawa watu wapo! So save your energy for better.

Wasichojua ni kuwa mwanasiasa ni mwanasiasa tu. Ata support chochote kitakachompa impetus ya kutimiza malengo yake. Lakini pia kuna wanaotumia kigezo cha "mwenzetu" ili tumbo lipate chochote kitu.

Hii nchi ina shida sana. Anyway tutafika tu mwisho wa safari...!
 
"Nilihudhuria 70th (1992) birthday ya Mwalimu. Sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha. Alipokuwa anaondoka, mama mmoja kampa portrait yake aliyechora mama huyo mwenyewe. Akamambia msaidizi wake apokee. Zawadi ya Benz kwa Mzee wetu ikanishtua kidogo." ...
Alikuwa ni mkali, hayumbishwi na hababaishwi na lolote na yuko tayari kufa kwa faida ya kila mtu, lakini wachache wenye chuki binafsi, walitamani afe pindi aonekanapo hadharani au ndani ya nyumba. Aliyazuia yasiyo na tija na kuhifadhai kwa faida ya wananchi, lakini wenye maslahi binafsi na mlengo hasi walimchukia.

Siku chache kabla ya mauti, ni kama nguvu za asili zilikuwa zinamwelekeza kilele chake alitamka mahala akiwa njiani kwenda jijini Dar "...Mtanikumbuka kwa mema sio mabaya....."
Haya yote ni sharti yatokee ili kuumba ujumbe katika utimilifu wake.

Mtu ana 'promote' barakoa iliyotengezwa nchi za nje tena N95 kwenye hadhira ambayo inatumika na daktari au nesi maalum kwenye chumba cha upasuaji 'surgery' badala ya kuhamasisha utenenezaji barakoa hapa nchi ni dharau za kutupwa.

Mtajenga majumba ya kifahari na kuhifadhi mali kuneemesha ukwasi lakini hatazikalia wala mali kuzifaidi kamwe.

Wazee ni muhimu zaidi kushughulikiwa kero zao kwa kuwa manufaa kwao ni salama kwa jamii na taifa kwa kuwa kunufaika kwao ni muda mchache tu wa kukaa hapa duniani.

Hakuna muda ambao bajeti itakuja kutosha kuhudumia mahitaji ya kila kada ya jamii ila kinachotakiwa ni kupima umuhimu wa kila jambo na manufaa yake yaliyoendelevu
 
Je, uliwahi kemea ile siku mwendazake alipoenda kuwaonesha hawa hastaafu mijengo yao? Au mwendazake alipokuwa anagawa maburungutu ya minoti barabarani? If not huna uhalali wa kusema si sawa la sivyo itakuwa ni wivu tu
Ndiyo, niliandika haya tarehe 18 Oktoba mwaka jana.
Huu ni uporaji. Wawe na hakika watatakiwa kujibu haya siku wakifa.
 
SIDHANI MAANA NI VIKAO VYA WAFANYAKAZI WA UMMA,MASHIRIKA NA VYAMA HUWA NA POSHO HIZO, PIA TUKI RECALL PALE ALIPOBABAIKA KUHUSU KUKOSA PENSION JAPO ELFU 30 WE UNAFIKIRIAJE HYO PESA INGEWEZA KU COVER MANGAPI VIJANA WANGAP LEO, MAKUNDI MAALUM MANGAP LEO YANAPAMBANA NA UCHUMI HALI MBAYA UKATUMIA NUSU BILION KWAAJILI YA GARI TU LA MSTAAFU
Ikiwa tu waandika habari hupewa "bahasha" na madc seuze wazee waalikwa kwa Mkuu wa nchi.
Acheni utani basi...
 
"Nilihudhuria 70th (1992) birthday ya Mwalimu. Sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha. Alipokuwa anaondoka, mama mmoja kampa portrait yake aliyechora mama huyo mwenyewe. Akamambia msaidizi wake apokee. Zawadi ya Benz kwa Mzee wetu ikanishtua kidogo."

-- Issa Shivji kupitia Twitter


Sijui kwa nini wazo la Vijana kuwa na Baraza/Jumuia yao rasmi nje ya vyama vya siasa linapuuzwa hasa na serikali.

Vijana hawawezi kuwa wamoja kupitia Jumuia za vyama kwa kuwa Jumuia hizi zinawagawa kuliko kuwaunganisha!

Magufuli alimjengea KIKWETE nyumba.

Magufuli alimjengea MWINYI nyumba.

Rais Suluhu amemnunulia MWINYI Gari la Anasa, aina ya Benz.

Hivi Marais hao wastaafu wenye kulipwa nusu ya Mishahara ya Rais aliyeko madarakani Wanashida hizo?

Hawamudu gharama?

Mr mkiki
80%
 
Yani wale wazee wa dar juzi walipewa hata nauli kweli?? Huyu mzee serikali bado inamuhudumia mwanzo mwish alafu leo kodi zetu wanatumia kumnunulia gari... Mara magu nae aliwajengea nyumba kwamba wakiwa madarakani huwa hawajipangi kuwa ipo siku watatoka. Mama anaanza kukwama sana
Hawa wanachezea mali za umma balaa
 
Alijenga nyumba za wastaafu wote

80% ya mshahara wa aliyepo madarakani. Magu alishusha mshahara wake ili kukabiliana na huo mzigo mzito, wanahudumiwa kwa kila kitu.
Kisha akagawa mapesa ya ofisi mitaani kama njugu...
 
Mbona wakati the late pres anagawa hela
Barabarani hakusema lolote!
Wakati mwingine bora ufunge mdomo wako

Ova
 
"Nilihudhuria 70th (1992) birthday ya Mwalimu. Sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha. Alipokuwa anaondoka, mama mmoja kampa portrait yake aliyechora mama huyo mwenyewe. Akamambia msaidizi wake apokee. Zawadi ya Benz kwa Mzee wetu ikanishtua kidogo."

-- Issa Shivji kupitia Twitter


Sijui kwa nini wazo la Vijana kuwa na Baraza/Jumuia yao rasmi nje ya vyama vya siasa linapuuzwa hasa na serikali.

Vijana hawawezi kuwa wamoja kupitia Jumuia za vyama kwa kuwa Jumuia hizi zinawagawa kuliko kuwaunganisha!

Magufuli alimjengea KIKWETE nyumba.

Magufuli alimjengea MWINYI nyumba.

Rais Suluhu amemnunulia MWINYI Gari la Anasa, aina ya Benz.

Hivi Marais hao wastaafu wenye kulipwa nusu ya Mishahara ya Rais aliyeko madarakani Wanashida hizo?

Hawamudu gharama?

Mr mkiki
Siyo nusu ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani mkuu, ni 80% ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani. Naomba isomeke hivyo tafadhali!
 
Huyu Mzee Shivji hovyo Sana. Yaani ana ishu ndogondogoo kama sio Prof. Anazidiwa mbali na Mabala
Wa hovyo ni kama nyinyi msiomuelewa. Kwani kuwa profesa ni kukubali ufisadi ambapo matajiri wanapeana zawadi kwa mgongo wa maskini. Hapa Shivji ameeleza ukweli na hisia zake kuwa marais hawapaswi kuzawadiwa zawadi wakati wananchi wa kawaida wanaolipa kodi wanaumia. Huu ni ufisadi wa kimfumo.
 
Back
Top Bottom