Prof. Anna Tibaijuka amkosoa Mh. David Kafulila

Prof. Anna Tibaijuka amkosoa Mh. David Kafulila

wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.

Haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?

Anna Tiba anamatatizo na ndio maana mwili wake hauna shukrani. Sijawahi kusikia akijenga hoja na kuisimamia. Ohh kweli Tiba kafilisika ki fikra.
 
Kuna quote moja toka hapo jirani (Malawi) Thandika Mkandawire “I have known politics turning intellectually respectable academics into political disasters and unfathomable idiots”
 
17,000 walikuwa ni watu wa kawaida huwezi kuwalinganisha kwa namna yoyote na wabunge 600 wawakilishi. Impact ya wabunge 600 ni kubwa kuliko watu laki 3 kwa pamoja waliotoa maoni. Watu waache kufikiri kinyumenyume.

Nadhani ni heri huyo mama akae kimya kuliko kuongea utumbo wa watu waliokimbia umande kama Sendeka. Aisubiri historia itakavyo mhukumu kwa haki yeye na wengi wenye weledi ambao wameamua kujidhalilisha kwa wanasiasa wa CCM na kuwasahau wananchi.
 
Prof yupo sahihi, ni vizuri watu warudi kujikumbusha statistics. Ile tume ilihoji watu takriban 350,000 kwa maana ndiyo sample inayowakilisha watanzania. Hivyo 17,000 walioongelea muungano ni asilimia 5 tu ya sample na ndiyo asilimia ya watanzania. Ukija kwa bunge la katiba wapo 600 ndiyo sample ya wawakilishi wa watanzania hivyo asilimia itatokea hapo (idadi ya wajumbe / jumla ya wajumbe)

Acha kupotosha; ile haikuwa electoral system ilikuwa ni maoni ; kwa hiyo yanakuwa treated CASE BY CASE!!!!
 
Kuna quote moja toka hapo jirani (Malawi) Thandika Mkandawire “I have known politics turning intellectually respectable academics into political disasters and unfathomable idiots”

Ni sahihi kabisa kwa kuwaangalia wasomi wetu wanavyo chemka wakiingia ktk siasa. Mwangalie huyu mama,ameishi na kufanya kazi ktk Taasisi zinazo heshimika, amerejea nyumbani hana mchango wa kusifia. Mfano mwingine ni Asha-Rose Migiro amefanya kazi ktk UN ktk nafasi kubwa, katembea duniani kutatua migogoro ambayo mingi inasababishwa na ukosefu wa haki. Karudi nyumbani hana tofauti na vijana toka vijijini kule Singida akina Mwigulu na Nnape!
 
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.

Haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?

Hapo naona Prof. Tibaijuka kateleza au hakuelewa alichokizungumza. Anaposema Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" kuwa alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling". Napata tabu kidogo juu ya alivyojichanganya Prof.

Msingi wa hoja yangu ni kama ifuatavyo;

Ikumbukwe kuwa Sampuli “Sample” inaweza kuwa wakilishi au isiwe wakilishi kutokana na “target area of interest”, say population ya watu, wadudu etc.

Sampuli isiyo wakilishi :

Mfano, Kipima joto (ITV), let say kuwa umewahoji watu 4, then kati ya hao wawili wakasema ndiyo na wawili wakasema hapana. Kwa aina hii ya sampuli huwezi sema(Ku-generalize) kuwa asilimia 50 ya watanzania/ wakazi wa Dar wamesema ndiyo. Bali utasema asilimia 50 ya watu WALIOHOJIWA wamesema ndiyo, na asilimia iliyobaki wamesema hapana.

Sampuli wakilishi:
Kimsingi, hii hufanyiwa mahesabu kutokana na ukubwa wa population yako, hapa namaanisha kwamba ni lazima kwanza ujue ukubwa (size) wa “population of interest” from which the sample is drawn, then yanafanyika mahesabu ambayo kwayo unapata namba ambayo ni ndogo kuliko ukubwa wa population yako LAKINI ni namba ambayo ni wakilishi na hapo ndipo unapoweza kufanya GENERALIZATION.

Sasa basi, ili kupata sampuli ambayo ni wakilishi au isiyo wakilishi kuna aina mbali mbali za sampling ambazo ni, Simple random sampling (SRS), Systematic sampling, Stratified sampling, Cluster sampling, Multi stage sampling (ambayo ni muunganiko wa kuanzia aina mbili za sampling).

Kwa maana ya aina za sampuli nilizozielezea hapo juu na kwa maana ya alichokisema Prof. Tibaijuka, ni kuwa "non-stratified sampling" ni aina nyingine za sampling kwa maana ya SRS, Systematic sampling, Cluster sampling na Multi stage sampling na siyo “stratified sampling”
Kwa kifupi unapozungumzia "stratified sampling" ni aina ya sampuli ambayo unaifanya kiasi kwamba elements zake zinakuwa zimegawanywa kimakundi ambapo element katika ndani ya kundi moja zinakuwa hazifanani/tofauti na elements ndani ya kundi jingine. Mfano: kundi la wavulana pekee yao, na kundi jingine la wasichana peke yao, au watu wa vijijini kundi moja na watu wa mijini kundi lao/jingine.
Itakumbukwa kuwa Tume ya Warioba walizunguka nchi nzima, ambapo watu wa mkoa mmoja unaweza sema ni kundi moja, na watu wa mkoa mwingine ni kundi jingine na kadhalika. So kwa maana hiyo hiyo watu waliotoa maoni wanaweza wakawa stratified KI-MIKOA.

Ukija kwenye muundo wa wajumbe 201 wa Bunge la Katiba waliochaguliwa, wajumbe hawa wanaweza wakawa stratified kwa makundi wanayowawakilisha. Mfano kundi la wafugaji, kundi la walemavu, kundi la waganga wa jadi, kundi la vyama vya siasa, wawakilishi wa madhehebu etc. Hawa wote ni Stratified sampling.

Ukija kwa wajumbe waliosalia ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kimsingi hawa walichaguliwa na wananchi lakini hawa nao pia unaweza kuwa Statify kimikoa wanayotoka, mfano wabunge wote wa kutokea mkoa wa Iringa watakuwa kundi moja, wa mkoa wa Mara watakuwa kundi jningine etc, hivyo hawa wote nao ni Stratified.

Kwa ujumla alichoongea Kafulila ni aina Stratified Sampling.

Hoja aliyoisema Prof. Tibaijuka kuwa Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani haina mashiko, kwa sababu hao wote waliojitokeza mbele ya tume ni watanzania haijalishi wapo vipi. Hii ni sawa na jinsi wajumbe 201 walivyochaguliwa, haijalishi ni wa umri upi, au wawe wamesomea kutunga katiba, au wawe na kimo cha futi fulani etc, cha msingi ni watanzania.

Swali ambalo Prof angohoji ni kama idadi ya watu (sampuli) waliohojiwa na Tume ya Warioba ni wakilishi kwa watanzania wote? Na je sampuli ya wajumbe 601 ni wakilishi kwa watanzania wote? Na sio kusema ni Stratified au Non stratified!

Karibuni kwa mjadala.

Prof yupo sahihi, ni vizuri watu warudi kujikumbusha statistics. Ile tume ilihoji watu takriban 350,000 kwa maana ndiyo sample inayowakilisha watanzania. Hivyo 17,000 walioongelea muungano ni asilimia 5 tu ya sample na ndiyo asilimia ya watanzania. Ukija kwa bunge la katiba wapo 600 ndiyo sample ya wawakilishi wa watanzania hivyo asilimia itatokea hapo (idadi ya wajumbe / jumla ya wajumbe)

hao 350000 walihojiwa kuhusu muungano?
 
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.

Haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?

Kuna kitu kinaitwa "Common Sense" Ukiwa na hii kitu hata uprofessor sio dili.Kwani mie naona maprofessor wetu wanafundishwa kusoma mawazo ya wengine, hivyo kufanya dhana nzima ya elimu nchini ionekane haina maana.

suala la muungano linahitaji common sense tu!kwamba mfumo uliopo umeshindwa kufanya kazi.Haya mambo ya kuanza sijui samping ni kulifanya liwe gumu na watu kutafuta hoja ya kupinga serikali tatu.Kama vile tunavyoambiwa sijui,muungano utavunjika,mara vita ,mara nini sijui.

Mie napata hasira tu mshahara wangu unakatwa tu,halafu jambo rahisi la kuamua ama serikali tatu au moja ,watu wanabishana miezi.
 
Mkuu kusema tume haikufanya stratification kwa maana nyingine unasema maoni yalikusanywa arbitrarily ambayo sio sahihi. Uamuzi wa kusema utakusanya maoni kila mkoa tayari hapo mikoa ni STRATA. Then kwenye kila mkoa ukichagua watu randomly hiyo ndo inatengeneza STRATIFIED RANDOM SAMPLING. Lakini pia kulikuwa na Mabaraza ya Wilaya ya Katiba, haya yalipatikana kwa division ya kiwilaya. Hapo wilaya zilikuwa Strata. Kwa hiyo kama hoja ni stratification hiyo ilifanyika sema tu haikusemwa.
Usilazimishe mambo mkuu, ilibidi waende kila mkoa.
Kuhusu mabaraza wote tunajua ni chama kimoja tu.
 
Usilazimishe mambo mkuu, ilibidi waende kila mkoa.
Kuhusu mabaraza wote tunajua ni chama kimoja tu.

Unauliza kama walienda kila Mkoa, au unasema walitakiwa waende kila Mkoa?

NB: Tume ilipita kila mkoa. Lakini kitu ambacho sijasikia wakina Anna Tibaijuka wakitolea ufafanuzi ni je, ni wapi Tume ilikwenda kinyume na HADIDU REJEA (ToRs) katika ukusanyaji maoni? Na Anna Tibaijuka na genge lake walikuwa wapi muda wote ? Kwanini hawakuongea kuwa ukusanyaji wa maoni hauzingatii "stratified sampling? " mpaka kazi inamalizika ndio wanaanza kupiga kelele? Kumbuka rasimu iliyoko bungeni ni "edition" ya pili.
 
Last edited by a moderator:
Usilazimishe mambo mkuu, ilibidi waende kila mkoa.
Kuhusu mabaraza wote tunajua ni chama kimoja tu.

Ishu sio kwenda kila mkoa wala kila sehemu ya nchi, ishu ni kuigawa kazi yao kimikoa sio stratification? Strata sio lazima iwe mkoa, inaweza kuwa hata zone! Swali la msingi kwako ni strata zilikuwepo au hazikuwepo?
 
Ndugu wanajamvi, nani ambaye amewahi kuona panya mwenye akili kuliko wenzake? Panya hata awe mkubwa ni panya tu na mawazo yake ni ya kipanyapanya tu. Akili za mapanya zinafanana. Usimshangae kusema hivo kwa sababu yeye ni ukoo ule ule wa mapanya. Tunaoamini ukweli tunaendelea kuamini ukweli.
 
Wananchi tuamke hawa mbuzi wa ccm miaka yao imeisha ni w kuchinja tena pasaka hii wawe kitoweo....
 
Kikwete aliyesema 17,000 waliotoa maoni ni wachache alikuwa sahihi? Kafulila kahoji kama watu 17,000 ni wachache wao wabunge 600 wana uhalali gani? Ukiwa CCM hata uwe Profesa lazima ufikiri kwa kutumia Ma------ aise...of all people Anna Tibaijuka?

Alichosema JK ambacho ndio ukweli ni kwamba, katika watu laki 7 waliofikiwa na tume.. 0nly elf 47 ndio waliozungumzia juu ya muundo wa muungano... wengine wote hawakuona tatizo juu ya suala la muundo wa muungano.. kati ya hao elf 47.. watu elf 17 ndio waluotaka serikali 3..
 
Last edited by a moderator:
Hapo naona Prof. Tibaijuka kateleza au hakuelewa alichokizungumza. Anaposema Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" kuwa alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling". Napata tabu kidogo juu ya alivyojichanganya Prof.

Msingi wa hoja yangu ni kama ifuatavyo;

Ikumbukwe kuwa Sampuli “Sample” inaweza kuwa wakilishi au isiwe wakilishi kutokana na “target area of interest”, say population ya watu, wadudu etc.

Sampuli isiyo wakilishi :

Mfano, Kipima joto (ITV), let say kuwa umewahoji watu 4, then kati ya hao wawili wakasema ndiyo na wawili wakasema hapana. Kwa aina hii ya sampuli huwezi sema(Ku-generalize) kuwa asilimia 50 ya watanzania/ wakazi wa Dar wamesema ndiyo. Bali utasema asilimia 50 ya watu WALIOHOJIWA wamesema ndiyo, na asilimia iliyobaki wamesema hapana.

Sampuli wakilishi:
Kimsingi, hii hufanyiwa mahesabu kutokana na ukubwa wa population yako, hapa namaanisha kwamba ni lazima kwanza ujue ukubwa (size) wa “population of interest” from which the sample is drawn, then yanafanyika mahesabu ambayo kwayo unapata namba ambayo ni ndogo kuliko ukubwa wa population yako LAKINI ni namba ambayo ni wakilishi na hapo ndipo unapoweza kufanya GENERALIZATION.

Sasa basi, ili kupata sampuli ambayo ni wakilishi au isiyo wakilishi kuna aina mbali mbali za sampling ambazo ni, Simple random sampling (SRS), Systematic sampling, Stratified sampling, Cluster sampling, Multi stage sampling (ambayo ni muunganiko wa kuanzia aina mbili za sampling).

Kwa maana ya aina za sampuli nilizozielezea hapo juu na kwa maana ya alichokisema Prof. Tibaijuka, ni kuwa "non-stratified sampling" ni aina nyingine za sampling kwa maana ya SRS, Systematic sampling, Cluster sampling na Multi stage sampling na siyo “stratified sampling”
Kwa kifupi unapozungumzia "stratified sampling" ni aina ya sampuli ambayo unaifanya kiasi kwamba elements zake zinakuwa zimegawanywa kimakundi ambapo element katika ndani ya kundi moja zinakuwa hazifanani/tofauti na elements ndani ya kundi jingine. Mfano: kundi la wavulana pekee yao, na kundi jingine la wasichana peke yao, au watu wa vijijini kundi moja na watu wa mijini kundi lao/jingine.
Itakumbukwa kuwa Tume ya Warioba walizunguka nchi nzima, ambapo watu wa mkoa mmoja unaweza sema ni kundi moja, na watu wa mkoa mwingine ni kundi jingine na kadhalika. So kwa maana hiyo hiyo watu waliotoa maoni wanaweza wakawa stratified KI-MIKOA.

Ukija kwenye muundo wa wajumbe 201 wa Bunge la Katiba waliochaguliwa, wajumbe hawa wanaweza wakawa stratified kwa makundi wanayowawakilisha. Mfano kundi la wafugaji, kundi la walemavu, kundi la waganga wa jadi, kundi la vyama vya siasa, wawakilishi wa madhehebu etc. Hawa wote ni Stratified sampling.

Ukija kwa wajumbe waliosalia ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kimsingi hawa walichaguliwa na wananchi lakini hawa nao pia unaweza kuwa Statify kimikoa wanayotoka, mfano wabunge wote wa kutokea mkoa wa Iringa watakuwa kundi moja, wa mkoa wa Mara watakuwa kundi jningine etc, hivyo hawa wote nao ni Stratified.

Kwa ujumla alichoongea Kafulila ni aina Stratified Sampling.

Hoja aliyoisema Prof. Tibaijuka kuwa Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani haina mashiko, kwa sababu hao wote waliojitokeza mbele ya tume ni watanzania haijalishi wapo vipi. Hii ni sawa na jinsi wajumbe 201 walivyochaguliwa, haijalishi ni wa umri upi, au wawe wamesomea kutunga katiba, au wawe na kimo cha futi fulani etc, cha msingi ni watanzania.

Swali ambalo Prof angohoji ni kama idadi ya watu (sampuli) waliohojiwa na Tume ya Warioba ni wakilishi kwa watanzania wote? Na je sampuli ya wajumbe 601 ni wakilishi kwa watanzania wote? Na sio kusema ni Stratified au Non stratified!

Karibuni kwa mjadala.

Uko sahihi kuhusu aina za sampling. Uko sahihi pia kuwa takwimu za Tume zaweza kusemwa zimezingatia stratification, ila umekosea kufikiri stratified sampling huchukuliwa baadaye (after the fact). Ni lazima ifanywe kabla, na ili iwe na maana ni lazima iwe ama systematic sampling au random systematic au simple random KWA KILA STRATA! Tume haikufanya hilo. Hata sampling ya kawaida ambayo ingeweza kutumia administrative multistage sampling badala ya demographic sampling units za National Statistical Bureau, ambayo ingetumia simple random kwa mikoa, kisha wilaya, tarafa, kata, vijiji, vitongoji, kata, kaya, wakazi hadi wanaume au wanawake ndani ya kaya haikufanyika. Ndiyo tatizo kubwa la takwimu za Tume - kukosa uwakilishi. Tatizo kubwa si wingi wa waliohojiwa, ni jinsi walivyopatikana. Hata wewe utajua kutokana na uelewa wako kuwa Tume haikufanya sampling kabisa. Walihoji yeyote anayejitokeza. Hili la watu 17,000 ni kosa jingine, lakini ni jepesi zaidi, ila nalo linashangaza kuwa watu hawa walio asilimia ndogo ya wahojiwa zaidi ya 300,000 wanaelezwa kuwa ndiyo maoni ya wengi. Serikali 3 zitetewe kwa hoja zingine nzuri, siyo hii ya takwimu mbaya.
 
Mkuu siyo tu Tume ilikutana na wananchi wakatoa maoni bali hata yule ambaye alishindwa aliweza kuwasilisha maoni yake kwa maandishi kupitia barua na mitandao. Kama huyu mama angekua na hoja kwamba kuna wapiga kura wake walishindwa kuwasilisha maoni yao kwa njia zote zilizo tumiwa na Tume ningemwelewa.

Maoni yake ambayo bila shaka hayatoki rohoni bali yakiangalia maslahi finyu sana ya leo na kesho kisiasa ni kielelezo na mfano wa wasomi wachumia tumbo waliojazana ktk Siasa za Kibongo. Huwezi tofautisha Anna Tibaijuka na John Komba ama Ole Sendeka wakiwa jukwaani. Ni aibu. Na hatuwezi andika Katiba ya maana kwa wajumbe wengi wenye akili hizi za kuchumia tumbo.

Hapana, ndugu. Chukua muda kuelewa kuwa takwimu za Tume si sahihi kwa sababu mbili. Muhimu ni kuwa walikusanya maoni kiholela kwa kumsikiliza kila anayejitokeza. Hilo ni sawa kama unataka kupata fununu ya kwanza ya jumla. Ukitaka maoni wakilishi ni lazima utumie simple random sample inayowakilisha nchi nzima, hata kama sample hiyo ni ya watu 3,000 tu - hiyo itakuwa wakilishi kuliko a haphazard sample of 300,000. Hili jambo si la kubuni au la ushabiki. Ni la kitaalamu. Kazi hiyo hufanywa hivyo. Wasomi wamelihangaikia hili kisayansi hadi wakajua kuwa representative opinions zinapatikana kwa njia hiyo tu. La pili ni dogo na rahisi. Takwimu za Tume yenyewe, pamoja na makosa ya ukusanyaji, zinaonyesha kuwa watu17,000 kati ya 300,000 waliohojiwa ni asilimia ndogo, kwa hiyo hawawezi kuwa ndiyo mawazo ya wengi. Tetea serikali 3 kwa hoja zingine nzuri, siyo hii ya takwimu za Tume.
 
Watanzania wengi wanataka serikali tatu, kupinga uhalali wa hii hoja ni ku-force mambo na kuonyesha jinsi usivyokuwa attached to regular wanananchi mitaani.
However, kufananisha wabunge walivychaguliwa na maoni yalivyosikilizwa ni sampling methods mbili tofauti. Wabunge walikuwa stratified based on groups wanazowakilisha while rasimu haiku-stratify watoaji wa mapendekezo (kama stratification ilifanyika ni znz vs bara tu).

Kwa hiyo ni kweli kaflila alikosea kutoa mfano huo.

Wakati wa kukusanya maoni kulikuwa na wananchi wa kawaida kuzunguka nchi nzima of course wards, districts, baadaye kukawa na maoni ya NGOs, viongozi wastaafu, mashirika ya dini, vyama vya siasa, etc. Je, hiyo ina tofauti gani na wajumbe wa bunge la katiba walivyopatikana au maoni wanayowakilisha yanatoafauti gani na yale yaliyotolewa wakati wa rasimu 1 na 2?
 
Maswala ya sample na takwimu ni mawili tu. La kwanza, wahojiwa walijichagua, walikuja wenyewe. Maana yake wanaweza kujihamasisha kuwa na msimamo mmoja. Hiyo haikubaliki katika utafiti wa maoni. La pili, swala si watu 17000 kuwa wengi au wachache, ila hao ni asilimia ngapi ya waliotoa maoni. Ndiyo maana wanaoyajua haya wamekuwa wanasema kuwa wazo la serikali tatu lijikite kwenye utetezi mwingine tu, siyo wa takwimu kwa sababu hazitoshi kuwa authoritative kwa wazo la serikali tatu. Mwenyekiti Warioba alilikataa hili mwanzo kabla hajaelewa. Sasa ameelewa na kukiri hivyo katika interview gazeti la wiki hii la Raia Mema.

Hao watu 17,000 ya waliopendekeza mfumo wa serikali 3 ni asilimia 5 ya watu wote 300,000+ waliotoa maoni kwenye tume. Naomba nisaidiwe, je hii asilimia tano, ni ya ngapi katika list ya mambo yaliyo changiwa kwa asilimia kubwa (Je, kuna jambo au mawili yaliongelewa kwa percentage kubwa zaidi ya hilo?)
achilia mbali ile namba nyingine ambayo maoni yao haya kuchukuliwa kwa sababu ya utaratibu uliowekwa kuwa mmoja akushaongelea jambo, mwingine hatatakiwa kuliongelea jambo hilo hilo, kitu kinachoashiria kuwa kama si restriction iliyowekwa basi huenda namba ingekuwa 17,000 x 10.
Naomba kufahamu kuhusu rank ya hiyo 5% in the list sababu kwa utaratibu uluowekwa na tume kwa namna ya watu kutoa maoni yao, basi hiyo 5% kitakwimu inaweza kuwa authorative.
 
Back
Top Bottom