Prof. Anna Tibaijuka amkosoa Mh. David Kafulila

Prof. Anna Tibaijuka amkosoa Mh. David Kafulila

Hivi katiba tuliyonayo ambayo baadhi ya viongozi walidai inafaa haina haja ya kuandaa nyingine walitumia aina ipi ya sample kuiandaa na ni asilimia ngapi ya watanzania waliowakilisha? halafu rais aliandaa tume je aliiambia ni sample gani ikatumie kuuliza maswali? ACHENI LONGOLONGO ZENU CCM, TUNATAKA SERIKALI 3.
 
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario

Hivi kwani tume ilitakiwa ku-target watu wenye sifa fulani? Hivyo vikao vilivyokuwa vikifanyika vijijini vilikuwa vya nini basi?

Pia ikumbukwe kuwa tume ya jaji Warioba ilitumia pia mapendekezo kutoka tume zilizotangulia, ambazo zilifanya stratified sampling. Sasa sijui prof. alitaka hiyo sampling ifanyekaje zaidi?
 
Kikwete aliyesema 17,000 waliotoa maoni ni wachache alikuwa sahihi? Kafulila kahoji kama watu 17,000 ni wachache wao wabunge 600 wana uhalali gani? Ukiwa CCM hata uwe Profesa lazima ufikiri kwa kutumia Ma------ aise...of all people Anna Tibaijuka?

Sasa nawewe na kafulila ndio mnapotosha, wajumbe 600 ni wawakilishi wa watanzania wotevna mawazo yao ndio mawazo yetu, sasa iweje leo watu 17000 wanawakilisha mawazo ya nani? Jaribu kufikiri cyo lazima ufuate mawazo ya kafulila.
 
Last edited by a moderator:
Natamani mama(Prof) angekuja kulifafanua hili ili tumuelewe alichokuwa anakimaanisha hasa!
 
Tangu huyu mama kawa Waziri wa Ardhi migogoro ya ardhi imeongezeka na ameshindwa kazi kabisa.Viwanja vya wazi vilivyoporwa ameshindwa kurejesha kwa kwa wanainchi

Mkuu ukiwa na maccm yaani hata uwe prof akili inakuwa kama ya maiti. Anna tibaijuka! Of all the people!!!
 
Warioba, Nyalali, Kisanga,Amina, Ofisi ya makamu wa rais, Ofisi ya waziri mkuu, Bunge la JMT, Baraza la Wawakilishi, Abdul Jumbe Mwinyi....wote hawa walikosea?
 
Sasa nawewe na kafulila ndio mnapotosha, wajumbe 600 ni wawakilishi wa watanzania wotevna mawazo yao ndio mawazo yetu, sasa iweje leo watu 17000 wanawakilisha mawazo ya nani? Jaribu kufikiri cyo lazima ufuate mawazo ya kafulila.

wamwakilisha raised alaaaa
 
17,000 walikuwa ni watu wa kawaida huwezi kuwalinganisha kwa namna yoyote na wabunge 600 wawakilishi. Impact ya wabunge 600 ni kubwa kuliko watu laki 3 kwa pamoja waliotoa maoni. Watu waache kufikiri kinyumenyume.

Watu wa kawaida ni wepi na wasio wa kawaida ni wepi.?
Ofisi ya Raisi, Ofisi ya Waziri mkuu, Baraza la wawakilishi ni watu wa kawaida.?

CCM wakati mnapanga mikakati na kuhamasisha wananchi huko vijijini wakapendekeze maoni yenu hamkujua ni watu wa kawaida.?

Mbona mambo mengeni kwenye Rasimu mnakubali bila kuhoji ni watu gani wametoa hayo maoni.?
 
ndo maana KINGUNGE NGOMARE MWIRU.AKACHAGULIWA KUWAKILISHA WAGAGANGA WA KIENYEJI.WAPI NA WAPI AU NA YEYE NI MGANGA WA CCM.MBONA HUJIELEWI WW AU UMEROGWA?.
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario
 
Watanzania wengi wanataka serikali tatu, kupinga uhalali wa hii hoja ni ku-force mambo na kuonyesha jinsi usivyokuwa attached to regular wanananchi mitaani.
However, kufananisha wabunge walivychaguliwa na maoni yalivyosikilizwa ni sampling methods mbili tofauti. Wabunge walikuwa stratified based on groups wanazowakilisha while rasimu haiku-stratify watoaji wa mapendekezo (kama stratification ilifanyika ni znz vs bara tu).

Kwa hiyo ni kweli kaflila alikosea kutoa mfano huo.
Mimi nina mtizamo tofauti na wako, Wabunge 201+399 wametoka kwenye sample ya watu milion 40, Na 201 wakiwa stratified, wakati 399 wakiwa wametokana na watu million 40 unstratified (201 wakiwemo), Lakini watu 17000 wametokana na population watu Million 40 ambapo hii representation ni kubwa sana na hasa ukizingatia kuwa hawa Watu 40m sio wote wanaweza kufikiwa , kusema na kusikika hata kama ukifanya simple sampling.
 
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario

Prof. A.Tibaijuka yupo sahihi lkn kaingiza facts zake hizo mahali pasipo. Anaingiza methodology badala ya ku-analyse hoja ya Kafulila iliyojikita ktk implications za mbinu iliyotumiwa na TUME YA KATIBA MPYA kufikia ,simamo wa muundo wa S3 badala ya S2.
Prof ameingia ktk mkumbo wa kina Mwigulu,Sendeka na Serukamba ya kutoa hoja utumbo ili kuvuruga hoja.Basis ya yote hayo si utashi wa Mama wa BAWATA,la hasha, ni kufanikiwa kwa mbinu mbovu za ccm kutibua hoja za weledi kwa mtindo huo wakijua wazi wana genge kubwa la maamuma wao watakaowaunga mkono.
My take, WELEDI WOTE TUUNGANE NA KUSIMAMA KIDETE NYUMA YA VINATA WETU KINA JUSSA LIPUMBA LISSU MBOWE na Maalim Seif, kuhakikisha S3 unakuwa ndio muundo wa utawala wa JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA.
 
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.
(haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?)

Nasikitika sana. Pamoja n.a. Kwamba tume haikutumia stratified or non stratified sampling bado Mfumo ?walioutumia wa kila mmoja kupewa nafasi una tafsiri nzuri ambayo inaonesha 17000 ndio wenye uelewa Wa Muungano. Wale ambao hawakuzungumzia kabisa muungano inawezekana hawaufahamu, Hawana hoja au hawakujianda kuzungumzia hilo ila wakipewa fursa tena watatoa maoniyao
 
Tume ingefanya stratification no dhahiri stratum ya wasomi wasio wanasiasa wangezungumzia kero za muungano na wangetoa suluhu nzuri
 
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario

Kama unajua research, which is the best most reliable sampling technique? Anayoisema Tibaijuka au aliyotumia Warioba na km ilivyofafanuliwa na Kafulila?
 
Uh hivi katika masuala ya katiba ya muungano, unataka stratified samples za namna gani? Tunazo mbili tu nazo ni Wazanzibar na Watanganyika...sasa hawa hawakuhojiwa? Haya mambo ya kudhani ku-stratify ni kutafuta makundi ya waliosoma sijui na wakulima au wafugaji...katiba hii ni ya wananchi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa hiyo samples ni mbili tu...Zanzibar na Tanganyika, kama hao upande mmoja haukuhojiwa then siyo stratified samples.
[h=2]Definition of 'Stratified Random Sampling'[/h]
A method of sampling that involves the division of a population into smaller groups known as strata. In stratified random sampling, the strata are formed based on members' shared attributes or characteristics. A random sample from each stratum is taken in a number proportional to the stratum's size when compared to the population. These subsets of the strata are then pooled to form a random sample.

Kwani shared attributes zetu kama wananchi ni nini si uTanzania? Haya Prof. twakushukuru lakini bado inafaa kueleza zaidi kama kweli tume ya Jaji Warioba haikufanya kile ilichotumwa na serikali.
 
Huyu mama sijui na yeye amekua CCM masalia ametoka CCM asili (CCM ya Nyerere). wakati wa CCm ya Nyerere lazima uwe kichwa na sio ya sasa unatakiwa uwe na kichwa cha Nazi. Kinachonishangaza kwa huyu mama anasema sample ya Warioba Haikuwa stratified sio kweli. Kwanza Tume ilipokea maoni kutoka kwenye general public (huku kada zote walikuwepo) pili tume ilipokea maoni kutoka kwa makundi maalumu (wanasheria, wanataaluma, wanasiasa, viongozi wastaafu, viongozi wa dini, makundi ya walemavu vijana, mawaziri, n.k). Pia ieleweke wasomi wengi hawakupata nafasi ya kutoa maoni yao kwa kusema bali wengi waliandika email na machapisho mbali mbali na kuwakilisha tume. Tukisema kati ya 722,000 waliotoa maoni 10% (70,000) yao ni makundi maalum na kati yao waliozungumzia katiba ni 10% (7,000) na kati yao waliotaka muundo waserikali tatu ni 25% (1,750) je hawa si wengi kuliko bunge la katiba. Note nimetumia (10%) ambayo ni ndogo kuliko ilivyo kwenye vielelezo vya katiba kuhusu suala la Muungano na muundo wa serikali. Mama Tibaijuka sio kweli stratified sampling method haikutumika nilivyoonesha hapo juu hivyo hoja yako haina mashiko watu mia nne kasoro (maana ni 600 - wapinzani + baadhi ya 201) muone hoja za watu 17,000 hazifai
 
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario
MHS David Kafulira kauliza kama ni halali Raisi kuchaguliwa na wananchi 5,000,000/ million out of 45,000,000! na isiwe halali kwa tume ya Mhs Jdg Warioba kutoa hizo takwimu zake?? Hao wanajaribu kuzima ukweli, Watanganyika tunataka nchi yetu, Wazenji wanataka uhuru wao!! Hapo sijui wanatumia nini kuzima huo moto???

Watanzania wengi wanataka serikali tatu, kupinga uhalali wa hii hoja ni ku-force mambo na kuonyesha jinsi usivyokuwa attached to regular wanananchi mitaani.
However, kufananisha wabunge walivychaguliwa na maoni yalivyosikilizwa ni sampling methods mbili tofauti. Wabunge walikuwa stratified based on groups wanazowakilisha while rasimu haiku-stratify watoaji wa mapendekezo (kama stratification ilifanyika ni znz vs bara tu).

Kwa hiyo ni kweli kaflila alikosea kutoa mfano huo.

Mkuu kusema tume haikufanya stratification kwa maana nyingine unasema maoni yalikusanywa arbitrarily ambayo sio sahihi. Uamuzi wa kusema utakusanya maoni kila mkoa tayari hapo mikoa ni STRATA. Then kwenye kila mkoa ukichagua watu randomly hiyo ndo inatengeneza STRATIFIED RANDOM SAMPLING. Lakini pia kulikuwa na Mabaraza ya Wilaya ya Katiba, haya yalipatikana kwa division ya kiwilaya. Hapo wilaya zilikuwa Strata. Kwa hiyo kama hoja ni stratification hiyo ilifanyika sema tu haikusemwa.
 
Kikwete aliyesema 17,000 waliotoa maoni ni wachache alikuwa sahihi? Kafulila kahoji kama watu 17,000 ni wachache wao wabunge 600 wana uhalali gani? Ukiwa CCM hata uwe Profesa lazima ufikiri kwa kutumia Ma------ aise...of all people Anna Tibaijuka?

Kweli kabisa wao 600 wana uhalali gani katika hili....au JK ana uhalali wa kua Rais wa nchi kwa kura zisio zidi milion 6,kati ya watu milion 45
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom