Prof. Anna Tibaijuka amkosoa Mh. David Kafulila

Malingumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
616
Reaction score
433
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.

Haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?
 
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.
(haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?)
Kikwete aliyesema 17,000 waliotoa maoni ni wachache alikuwa sahihi? Kafulila kahoji kama watu 17,000 ni wachache wao wabunge 600 wana uhalali gani? Ukiwa CCM hata uwe Profesa lazima ufikiri kwa kutumia Ma------ aise...of all people Anna Tibaijuka?
 
Last edited by a moderator:
Kama anaona kauli za Kafulila zina kasoro basi huyu mama atakuwa hajamwelewa Kafulila
 
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.
(haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?)
Tangu huyu mama kawa Waziri wa Ardhi migogoro ya ardhi imeongezeka na ameshindwa kazi kabisa.Viwanja vya wazi vilivyoporwa ameshindwa kurejesha kwa kwa wanainchi
 
Kikwete aliyesema 17,000 waliotoa maoni ni wachache alikuwa sahihi? Kafulila kahoji kama watu 17,000 ni wachache wao wabunge 600 wana uhalali gani? Ukiwa CCM hata uwe Profesa lazima ufikiri kwa kutumia Ma------ aise...of all people Anna Tibaijuka?[/QUOa TE]

huyu mama yetu ni member humu ajjitokeze tumshushie nondo za kitafiti, ndo atajua kuwa prof. ni sehemu ndogo sana ya taaluma , kuna mambo mengi yeye ni lay....
 
Lets say anayosema ni ya kweli ? Na kama walijua hayo kwamba mawazo ya watu watakaotoa yatakuwa ni ya wachache kwanini waliunda Tume ? Si wangejichagua tu hao 600 (ambao wanajiona ndio wengi) alafu watunge Katiba
 
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario
 
Watanzania wengi wanataka serikali tatu, kupinga uhalali wa hii hoja ni ku-force mambo na kuonyesha jinsi usivyokuwa attached to regular wanananchi mitaani.
However, kufananisha wabunge walivychaguliwa na maoni yalivyosikilizwa ni sampling methods mbili tofauti. Wabunge walikuwa stratified based on groups wanazowakilisha while rasimu haiku-stratify watoaji wa mapendekezo (kama stratification ilifanyika ni znz vs bara tu).

Kwa hiyo ni kweli kaflila alikosea kutoa mfano huo.
 
A.Tibaijuka ana kosoa kauli ya wao 600 kulinganisha na tume ilivyofanya. wao wameteuliwa kwa maana imetumika stratified sampling( kwa maana uteuzi wao ulicheck sifa fulani). lakini tume haikufanya stratified sampling.hivyo hoja ya A.tibaijuka iko sahihi kwenye ukosoaji wa hiyo scenario
Ndio tatizo la jirani zake Kagame hujiona wanajua kila kitu, hivi Tibaijuka kuna cha maana gani amefanya wizara ya ardhi? huyu mama hafai kabisa angejua watu tunafuatilia hati za viwanja kwa miaka zaidi ya mitano na bado hatupati angetulia. Mwenzake Magufuli alionesha nia na alikuwa anchapa kazi.
 
Tuelimisheni wakuu mambo ya stratified sampling ili Kafulila naye akiingia humu apate shule!
 
Huyu mama kwa kifupi yeye ni profesa asiye na akili.. Amejawa na ushabiki usiokuwa na maana. Kweli maprofesa wa kiafrika ni wajinga sana. Mama kama upo umu na una hoja em njoo tupambane hapa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
huyu mama bora angetulia na heshima yake ya UN, kuliko kuchanganya elimu yake na rangi za kijani na njano zinazoharibu akili hata uwe prof, pole tibaijuka. ila kumbuka unaharibu heshima yako zaidi.
 
Huyo Prof Tibaijuka anaweza kuwaambia Watanzania ni kifungu gani kwenye hadidu rejea kinachoongelea 'stratified sampling?

Sijui kwa nini wabunge wa CCM wameamua kujitenga na wananchi? Wako sooo out of touch!

Nani alitegemea Prof Tibaijuka angekuwa kinara wa udikteta kama anavyofanya huko Dodoma?
 
Shule ya Kafulila inamatatizo. Sampling nzuri ni idadi ya waliosema 'A' dhidi ya waliosema 'B' kati ya 'C' walioulizwa/waliochangia swali!!! ktk hoja ya muungano 17,000 ni kati ya idadi 'X' waliochangia hoja. Na ktk Bunge Maalum la Katiba tunataraji idadi 'y' kati ya 621 waseme kitu juu ya muungano
 
Ndio tatizo la jirani zake Kagame hujiona wanajua kila kitu, hivi Tibaijuka kuna cha maana gani amefanya wizara ya ardhi? huyu mama hafai kabisa angejua watu tunafuatilia hati za viwanja kwa miaka zaidi ya mitano na bado hatupati angetulia. Mwenzake Magufuli alionesha nia na alikuwa anchapa kazi.
Mkuu acha diversion. mimi sijqzungumzia utendaji kazi wake kwenye wizara. mimi ni check hiyo scenario namii nikato maoni yangu kulingana na logic ya scenario. punguza jazba mkuu
 
wadau nilikuwa naangalia habari,Prof. A Tibaijuka amesema Mh. Kafulila hakuwa sahihi alipokuwa anazungumzia kuhusu "samples" alisema,alichokisema kafulila siyo "stratified sampling" wala "non-stratified sampling" maana Tume ilikuwa inawahoji watu wa aina yoyote waliojitokeza mbele yao hivyo haikuwa inapanga iwafikie watu wa aina gani.
(haya mambo ya sampuli hayo,wataalamu mnasemaje?)

Prof yupo sahihi, ni vizuri watu warudi kujikumbusha statistics. Ile tume ilihoji watu takriban 350,000 kwa maana ndiyo sample inayowakilisha watanzania. Hivyo 17,000 walioongelea muungano ni asilimia 5 tu ya sample na ndiyo asilimia ya watanzania. Ukija kwa bunge la katiba wapo 600 ndiyo sample ya wawakilishi wa watanzania hivyo asilimia itatokea hapo (idadi ya wajumbe / jumla ya wajumbe)
 
Hiyo inaitwa simple random sampling yaani unapick sample randomly na inakubalika pia katika tafiti, kwa mfano tume ilitembea nchi nzima na walipokea maoni ya yoyote yule aliyejitokeza so hawakuwa bias
 
Mkuu acha diversion. mimi sijqzungumzia utendaji kazi wake kwenye wizara. mimi ni check hiyo scenario namii nikato maoni yangu kulingana na logic ya scenario. punguza jazba mkuu

Professor aliyeshindwa kutoa suluhisho la matatizo ya jamii yake na kukimbilia pesa /uongozi ni sawa na jitu lenye nguvu lililopewa chakula kilicho baki ili akalete chakula kwenye kijiji cha mbali na yeye akahamua kutokomea huko.
Tatueni matatizo ya nchi sio kutuletea vingereza vingi tu hapa.
 
Back
Top Bottom