Povu la Emmanuel Mbasha baada ya madam Flora kuzindua kitabu chenye jina 'Siri za Flora Mbasha'

Ni hatari sana kuoa mwanamke mjinga.

Ni hatari zaidi mkiachana na huyo mwanamke

mjinga maana atakugeuza mbao ya matangazo
 
Huyo mwanamke ni kilaza, tena yule dogo aliyemuoa kapata double loss kwa kua kaoa bibi bomba lakini pia hana akili anasema sema hovyo.

Sasa kama aliingiliwa akiwa P hilo ni jambo la kusema hadharani?
Kashaolewa yanini kuhangaika na mambo ya mtu aliyeachana nae?

sent from Sokoro nkorambokande
 
Kumchana ex wako inaonyesha jinsi gani amekushinda/amekuachia doa.Kama wewe ndo ulimuacha huwezi kumzungumzia maana hana maana wala thamani kwenye maisha yako.Ukiendelea kumzungunmzia ex wako ina maana kwamba bado yumo moyoni mwako,kama siyo unampenda basi itakuwa kuna mahali alikukomesha.
kweli afu mbasha kanaonesha ukidume hana habari na huyo flora ndiyo kwanza yupo bize na mambo yake na hata alivyo jibu amejibu kwa busara sana.
 
BAADA ya mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bongo, Flora Mbasha kusambaza kitabu alichokipa jina la Siri za Flora Mbasha kilichoanika ‘mabaya’ ya aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, mumewe huyo ameibuka na ‘kumchana’ vibaya mwimbaji huyo na kusema hafai kuwa mke.

Flora alikiachia kitabu hicho hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliyopitia kwenye maisha yake na Mbasha, alieleza namna ambavyo mumewe huyo wa zamani alivyokuwa akimtesa na hata kumuingilia kwa nguvu akiwa kwenye siku zake.

Akizungumza na mwanahabari wetu katika ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, Mbasha alianza kwa kueleza masikitiko yake juu ya kitabu hicho kwa kusema anashindwa kuelewa mume wa sasa wa Flora, Daud Kusekwa anajisikiaje pale Flora anapomzungumzia mara kwa mara.

“Yaani unajua watu wengine sijui wapoje bwana. Hivi kweli wewe hata huyo mwanaume wake anajisikiaje kuona mkewe ananiongelea kila wakati? Ni kukosa adabu, kwa nini wasifanye maisha yao? “Kweli mwanamke aliyefunzwa, akafunzika anaanzaje kumuongelea mwanaume wake wa zamani? Yaani kwangu mimi mwanamke wa aina hiyo anapoteza sifa ya kuwa mke,” alisema Mbasha.

Mbasha akizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Amani, alisema kuwa, aliamua kukaa kimya baada ya kupitia mambo mazito na mwanamuziki huyo ambayo kamwe hataki kuyasikia wala kurudi nyuma.

“Ametaka talaka mahakamani, tumeachana na mimi sikutaka tena hata kumzungumzia, lakini yeye kutwa amekuwa akinizungumzia. Halafu kwanza unamzungumziaje mtu ambaye mlishaachana? Mtu ambaye kwanza hana hata habari na wewe, anafanya maisha yake mengine, huu kama siyo ujinga ni nini?”

Alihoji Mbasha. Kama hiyo haitoshi, Mbasha alizidi kumwaga mboga kwa kusema kuwa, siku zote sikio la kufa huwa halisikii dawa kwani kitendo anachokifanya Flora cha kumzungumzia yeye kama zilipendwa wake, alishakifanya kwake kwa mwanaume mwingine.

“Kifupi ni kwamba tabia ni kama ngozi, huwezi kuibadili. Wewe unaona sasa hivi anavyoelezea mambo aliyokuwa akiyafanya na mimi na kuongeza uongo wake, alishanifanyia hata mimi wakati nimemuoa. “Yaani yule mwanamke sijui bana, Mungu amsaidie. Yaani kwanza wakati mimi naanza kumfuatilia, huwezi kuamini, alikuwa na mwanaume mwingine.
Shetani atawaaibisha sana kwa kuamua kuvunja kiapo cha kutokuachana milele.
 
Mwanawake akiona x amzungumzi ata kama yeye ndo alimtenda anakuaga kama anawashwa,... Na nyenyere, tuliza kiseb icho we Flora,
 
Back
Top Bottom