Anayedaiwa kumwingizia Panga mkewe sehemu za siri akamatwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Makong’onda, wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara, akituhumiwa kumpiga mkewe kisha kumuingizia panga sehemu za siri (njia ya haja kubwa) na kumsababishia majeraha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 14, 2023; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 8 saaa moja jioni katika Kijiji cha Makong’onda.

Kabla ya tukio hilo, Kamanda huyo ameeleza kuwa mtuhumiwa pamoja na mkewe, walikuwa katika shughuli zao za kuokota korosho, kaada ya hapo, mwanamke huyo alikwenda kwa binamu yake kutwanga kisamvu ambapo ni eneo la jirani na wanapoishi.

“Baada ya kukaa huko kwa muda akitwanga kisamvu hicho mumewe alihisi kuwa mkewe ameenda kwa mwanaume mwingine, baada ya kurejea alianza kumshambulia hadi mwanamke huyo kupoteza fahamu,” amesema Kamnda Katembo na kuongeza;

“Baada ya kipigo hicho, inadaiwa mtuhumiwa alichukua panga na kumuingizia sehemu ya haja kubwa na hivyo kusababisha majeraha. Hata hivyo muhanga huyo sasa anandelea vizuri baada ya kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Newala.”

Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi akiwataka kushiriki katika kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kuhu akisema: “Tutaendelea kuwachulia hatua kali za kisheria wote watakabainika kuhusika katika vitendo hivi vya kikatili kwa jamii zetu kwa kisingizio cha wivu wa mapenzi na mengineyo.”

Kwa upande wa Hamis Millanzi ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, amesema: “Nilipewa taarifa na mgambo wa kijiji, nilipofika nilikuta mhanga akiwa anavuja damu miguuni hivyo nilazimika kumuwahisha zahanati ya kijiji ambapo alipewa huduma ya kwanza.”

Mwenyekiti huyo aliendelea kueleza: “Hawa wanandoa wamekuwa wakipigana mpaka wanaumizana kuna wakati huyu mwanaume alichoma moto nyumba wanayoishi, sasa amemjeruhi mkewe, nilishatoa taarifa kwa Mtendaji wa Kata ili tutoe taarifa kwa Jeshi la Polisi.”

Mwanamke aliyejeruhiwa (jina linahifadhiwa) amesema kuwa wivu wa mapenzi umekuwa sababu kubwa ya mumemwe kumfanyia matukio mabaya ikiwemo kuchomwa sehemu za siri.

“...nilipoingia ndani nikamkuta amesimama akanishika shingoni na kuanza kunipiga mpaka nikazimia ambapo kelele za watoto ndio zilileta watu nyumbani na kunisaidia, hataki niende hata chooni ana wivu yaani hata hapa kaniacha peke yangu kwa kuwa yuko Polisi,” amesema mwanamke huyo na kuongeza;

“Kuna wakati ananipiga hadi ananichoma sehemu ya siri, sio mara moja nimekuwa nikimshitaki kwa mwenyekiti, tunasuruhiswa na kusameheana, hii ni ndoa yangu ya tatu, sikutaka kuhangaika ndio maana nilikuwa namsamehe mume wangu, sema ana wivu sana hata shambani nasindikizwa, chooni nasindikizwa.”

Kwa upande wake Sadam Madai Daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Newala amesema kuwa walimpokea mgojwa huyo akitokea Zahanati ya Makong’onda ambapo walimpatia matibabu ya awali na kwamba anaendelea vizuri na matibabu.

MWANANCHI
 
Kama alikua na uhakika kwamba anachofanya ni haki kwanini anakimbia?

Human's anatomy ikoje? Panga limekua na angle gani?
 
Back
Top Bottom