Povu la Emmanuel Mbasha baada ya madam Flora kuzindua kitabu chenye jina 'Siri za Flora Mbasha'

Sasa povu liko wapi? Niseme tu kwamba huyo mwanamume aliyemchukua Flora amekula hasara. Atakapoondoka kwake atakuwa anafanya hayo hayo. Huyu Florah ana roho ya uzinzi. Shetani hatamwacha salama. Atahangaika sana na dunia hii. Na kama hatatubu na kuomba msamaha ajue moto wa milele unamsubiri. Kwa sasa anaweza kuringia kiburi cha uzima. Lakini iko siku atajuta. Wala hiyo siku haiko mbali. Namshauri Emmanuel Mbasha aendelee kukaa kimya. Wala asimjibu. Ninajua inaudhi. Mwombe Mungu hekima na busara. Atakupa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uzinzi tu!! nyakati za mwisho. Huyo Flora sijui hata mzee wa NDIYOOOOOO angekuwepo akayaona haya na kuyasikia angejisikiaje!!! NDIYOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!
 
BAADA ya mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bongo, Flora Mbasha kusambaza kitabu alichokipa jina la Siri za Flora Mbasha kilichoanika ‘mabaya’ ya aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, mumewe huyo ameibuka na ‘kumchana’ vibaya mwimbaji huyo na kusema hafai kuwa mke.

Flora alikiachia kitabu hicho hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliyopitia kwenye maisha yake na Mbasha, alieleza namna ambavyo mumewe huyo wa zamani alivyokuwa akimtesa na hata kumuingilia kwa nguvu akiwa kwenye siku zake.

Akizungumza na mwanahabari wetu katika ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, Mbasha alianza kwa kueleza masikitiko yake juu ya kitabu hicho kwa kusema anashindwa kuelewa mume wa sasa wa Flora, Daud Kusekwa anajisikiaje pale Flora anapomzungumzia mara kwa mara.

“Yaani unajua watu wengine sijui wapoje bwana. Hivi kweli wewe hata huyo mwanaume wake anajisikiaje kuona mkewe ananiongelea kila wakati? Ni kukosa adabu, kwa nini wasifanye maisha yao? “Kweli mwanamke aliyefunzwa, akafunzika anaanzaje kumuongelea mwanaume wake wa zamani? Yaani kwangu mimi mwanamke wa aina hiyo anapoteza sifa ya kuwa mke,” alisema Mbasha.

Mbasha akizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Amani, alisema kuwa, aliamua kukaa kimya baada ya kupitia mambo mazito na mwanamuziki huyo ambayo kamwe hataki kuyasikia wala kurudi nyuma.

“Ametaka talaka mahakamani, tumeachana na mimi sikutaka tena hata kumzungumzia, lakini yeye kutwa amekuwa akinizungumzia. Halafu kwanza unamzungumziaje mtu ambaye mlishaachana? Mtu ambaye kwanza hana hata habari na wewe, anafanya maisha yake mengine, huu kama siyo ujinga ni nini?”

Alihoji Mbasha. Kama hiyo haitoshi, Mbasha alizidi kumwaga mboga kwa kusema kuwa, siku zote sikio la kufa huwa halisikii dawa kwani kitendo anachokifanya Flora cha kumzungumzia yeye kama zilipendwa wake, alishakifanya kwake kwa mwanaume mwingine.

“Kifupi ni kwamba tabia ni kama ngozi, huwezi kuibadili. Wewe unaona sasa hivi anavyoelezea mambo aliyokuwa akiyafanya na mimi na kuongeza uongo wake, alishanifanyia hata mimi wakati nimemuoa. “Yaani yule mwanamke sijui bana, Mungu amsaidie. Yaani kwanza wakati mimi naanza kumfuatilia, huwezi kuamini, alikuwa na mwanaume mwingine.
Hahaha watu kama hawa eti ni watumishi was mungu.
Mbele ya madhabahu ni haleluya kwa sana na kulia kwa sana duuh
Ee mungu tusaidie
 
Nani aliyekuwa analialia mitandaoni akitaka Flora wake? Ulishamsikia Flora akilia lia mitandaoni akitaka Mbasha wake?

Emman alisema mengi sana juu ya Flora lakini Flora alikuwa kimya.

Hafai kuw amke, kwa nini ulikuwa unamlilia kila wakti?

Ulimkuta na wanaume wengine, wewe ullipomuoa ulikuwa bikira?

Ulipomuoa Flora alikuwa mke wa nani vile? Sema kweli.

All in all, sipendi na sikubaliani na tangu mwanzo nilisema, mitandao ama jamii haijengi ndoa!. Niliwaonya sana Emma alipoanza kucheza taarabu mitandaoni nikamwambia hapa ndipo unabomoa ndoa yako mchana kutwa. Lakini hakunielewa.

Now it is over. Hakuna ufahaari wa kuanikana mitandaoni na kuanza kukandiana. Hawa watu wakumbuke wana mtoto wa kike ambaye kile wanakifanya kinamuumiza sana ylue binti na kumwathiri ki saikiolojia.

Amri: Komeni kualika watu kwenye unyumba wenu. Mapenzi hayana nguvo zaidi ya watu wawili. Now, kila matu amove kivyake. Flora na Emma acheni upumbavu!.
 
Inaonesha huyo flora bado hajapata uhondo aliokuwa anapewa na Emma.
 
Sasa povu liko wapi? Niseme tu kwamba huyo mwanamume aliyemchukua Flora amekula hasara. Atakapoondoka kwake atakuwa anafanya hayo hayo. Huyu Florah ana roho ya uzinzi. Shetani hatamwacha salama. Atahangaika sana na dunia hii. Na kama hatatubu na kuomba msamaha ajue moto wa milele unamsubiri. Kwa sasa anaweza kuringia kiburi cha uzima. Lakini iko siku atajuta. Wala hiyo siku haiko mbali. Namshauri Emmanuel Mbasha aendelee kukaa kimya. Wala asimjibu. Ninajua inaudhi. Mwombe Mungu hekima na busara. Atakupa.

Sent using Jamii Forums mobile app
roho ya uzinzi unayo wewe.usatembea na watu wangapi wewe kwenda huko
 
Wanandoa wa siku hizi mmh hawana siri kabisa
Huyo Emanuel Mbasha ni mwanamume kweli???? Kwa nini anajishushia hadhi zaidi kwa kutaka kuongelea mambo ya ndoa[hasa mabaya] hadharani? Hivi hajafundwa huyo, Anachotakiwa ni kunyamaza kimya kwani 'time always tell'
G Habasha aliwahi kukosea kidogo kuhusu mtalaka wake lakini alipopewa ushauri wa kunyamaza kimya alifanya hivyo na mwisho wa siku mambo yamekwenda shwari. Kuzungumzia mambo ya ndoa[mabaya] hadharani kwa mwanamume haifai kabisa. Kwa akina mama wao kwa hulka ya walivyoumbwa ni sensitivi sana na mbadala wa musuli kwao ni maneno hivyo anaweza sema mengi mabaya lakini mwisho wa siku ukweli unajidhihiri.
 
Back
Top Bottom