Fazili amjibu Mhaya na kuna makubwa ya kujifunza katika mahojiano haya; siri za utajiri wa kimungu

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,558
Hakuna kipindi katika maisha yangu nilichokuwa karibu na Mungu kama hiki. Sometimes mpaka najiona nimechelewa sana kuyafanya yale anayotaka kila siku niyafanye.
Wote wanaokuja kumjua Mungu wa Kweli hujilaumu kwanini wamechelewa kumjua Mungu na maisha yao hubadilika kabisa.
Mimi nilishakuwaga na mashaka sana na Mungu kwenye kujibu maombi, thats true bro lakini baadaye nikakaa na kujifikiria kwa nini? Watu wanasema Mungu anajibu, why kwangu hajibu? Sikutaka kuwasikiliza wachungaji wanasemaje, nikaingia chimbo.
Kwasababu hukumjua basi naye "hakukujua". Hii ni tabia ya ajabu sana ya Mungu.
Ndio! Nikaingia chimbo.

Nikapata elimu kuhusu Mungu. Huwa ninawaambieni humu kila siku. Kila ninachomuomba Mungu sasa hivi huwa anajibu kwa wakati ninaotaka anijibu.
Unajua kwanini? Ukimheshimu Mungu naye anakuheshimu! Na pia watu wengi hawapo kwa Mungu naye hayupo kwo!
Kitu cha kwanza lazima ukubaliane na dunia, hilo watu huwa wanalishindwa na lazima ujue kwamba shetani ana nguvu kuliko wewe, sio nguvu tu, bali anaweza hata kukuua.
Sio kweli shetani anaweza kukuua kila anapopenda, la sivyo angemaliza watu hasa walio wema ila hawezi kwa kuwa Mungu haruhusu afanye hivyo.
Mungu aliporuhusu shetani amjaribu Ayubu, miongoni mwa mambo aliyomwambia asimfanyie ni kumuua. Why? Hata Mungu anajua kwamba shetani kwa nguvu alizonazo, anaweza kukuua.
Kama akiruhusiwa na Mungu tu na sio vinginevyo. Hata wewe unaweza kuuwa mtu mwingine sivyo?
So cha kwanza kubaliana na dunia, usijifanye match know sana. Mtu anakwambia mambo makubwa duniani yanaongozwa na watu wa kishetani, anakuuliza nafasi ya Mungu ipo wapi? Bro! Kwanza kubaliana na hii dunia.
Ni kweli dunia hii watu wengi sana wamemezwa na maongozo ya kishetani hadi kufikia mahali watu wanafikiri Mungu hayupo na kwamba shetani ana nguvu kama Mungu au kumshinda, ni uongo mkubwa huu!
Tunaposema uwe humble, hata kukubaliana na hii dunia ni dalili ya kuwa humble, baada ya hapo sasa, saidia watu, ondoa chuki moyoni mwako halafu la zaidi kila siku utakapotaka kulala, chukua hata dakika 2 kumshukuru Mungu.
Sawa kabisa mshukuru Mungu kila siku. Hii ni siri kubwa ya kupata baraka zingine tena, mshukuru Mungu kila anapokubariki.
Usimshukuru kimoyomoyo, toa sauti yako mshukuru Mungu.
Kuna ukweli pia katika hili; kumsifu na kumshukuru Mungu hakuwezi kufanyika kimya kimya tu, ikifanyika kwa sauti huwa na nguvu ya ajabu.
Jumapili nilimwambia Mungu, mpaka inafika Ijumaa nataka hiki na kile, najua siwezi kuvipata na sijui nitavipata kwa staili gani. Ila wewe si ndiye Mungu ninayemshukuru kila siku? Wewe si ndiye Mungu ambaye namuabudu? Mungu basi kumbuka jinsi ninavyojitoa kwa watoto wa mitaani. Kama ninachokifanya ni sahihi, kwa nini usinipe sasa ninachokiomba?
Hii ni njia nzuri sana ya kum-provoke Mungu afanye jambo, kama umegundua hili basi ni chimbo kubwa!
Leo Jumanne... Mungu akanipa, hakutaka kusubiri mpaka Ijumaa.

Huyu Mungu muacheni tu.
Asifiwe!
Leo ukiniambia Mungu hakujibu maombi yako, maybe kuna sehemu unakosea, kuna codes bado hujazielewa.
Kweli.
Hebu wakati mwingine mjaribu Mungu. Si kwenye Biblia ameandika nijaribuni muone nitakavyowabariki? Sasa wewe mbona humjaribu? Unajitoa kwa watu, hebu mjaribu Mungu kwa kumwambia nataka hiki na kile, tena omba vile vilivyo nje ya uwezo wako.
Ni kweli kabisa, siri moja kubwa wasiojua watu ni kwamba; Mungu anafanya kazi na watu walio serious na yeye!
Mimi huwa nipo hivi....

Mtu akiniomba 500, nikampa, halafu akasema nashukuru sana, huwa naweza kumuongezea hata 2000, nipo hivyo. Huwa nasikia raha sana mtu akinishukuru. Sasa najiulizaga, kama mimi nasikia raha hivi, vipi kuhusu Mungu? Akinipa hiki, nikamshukuru sana, kesho nikimuomba kingine hawezi kunipa? Lazima atakupa kwa kuwa una moyo wa shukrani.
Dah! upo sahihi sana, Mungu anataka kujenga mahusiano na wanadamu, hivyo kumshukuru Mungu na sawa tu na kumwomba, tena ni kwa hali ya juu zaidi.
Braza! Mimi ni kasela flani hivi ila nipo humble sana kwa Mungu. Mimi mjanja mno ila ujanja nauwekeaga mfukoni nikiingiaga kwenye mambo kuhusu Mungu.
Mungu naye atakuheshimu hivyo hivyo, umejulia wapi hilo?!
Namwambiaga jamaa anayenitengenezea App... Bro usiwe na presha, yaani hata kama ipo tayari, just relax, muda wa Mungu ukifika, wewe mwenyewe utanikabidhi, lakini pia nikitaka unikabidhi wiki ijayo, nikamwambia Mungu wangu, wiki ijayo utakuwa umeimaliza na kunipa.

Nikijaga humu nakuwa kama fala, nakwambia ndugu yangu tujichange tukawasaidie watoto wa mitaani hata kwa chakula. Unaniona fala fulani.
Hakika kama umejua hilo wewe hutapungukiwa na kitu, unajua wanadamu ni mradi wa Mungu na yeyote anayewategemeza binadamu humgusa Mungu moja kwa moja na yeye kubarikiwa ni lazima, matajiri wa kweli wanajua siri hii na hawasemi kwa mtu, hii ndio dhambi yao kubwa1
Bro! Nikifikaga kule ndio najua kwa staili hii Mungu hawezi kukuacha hata iweje. Fikiria unawapa chakula watoto, wanachukua na kimoja kinabaki, kila ukitafuta mtoto, humuoni, unaamua kuondoka nacho. Tena unajikuta ukipita katika njia ambayo huwa hupitagi hata siku moja.
Kweli tupu.
Njiani unakutana na jamaa tu wa mtaani ambaye kwa kumwangalia unaona hajala, unataka kumpa, unahisi kabisa uzito moyoni, unaondoka. Njiani unakutana na muokota makopo, unamsogelea na kumpa ile plate, anaipokea, anakushukuru mno na anakwambia ni kwa namna ameteswa na njaa siku hiyo, daktari alimwambia kwa jinsi anavyoumwa, ale ashibe, atakula wapi? Anaamua kuokota makopo akauze apate pesa ya chakula tu ili ale ashibe kama daktari alivyotaka.
Mhuuu! Ukiwalisha watu hao unamsaidia Mungu mambo yake na umeweka deni kwake na yeye ni mwaminifu lazima atakulipa tu!
Ghafla njiani anakutana na wewe, unampa chakula. Bro! Mtu huyo anavyokushukuru, mwanaume mtu mzima mpaka anataka kulia, hebu jifikirie Mungu atamfanyia nini huyu Nyemo na watu waliojichanga kwa ajili ya hao watu? Unadhani wakimwambia Mungu tunataka hiki na kile atashindwa kuwapa? Thubutu.
Watu wengi hawajui siri hii!!!
Nilimwambia mama nitakuwa bilionea wa kwanza kwenye familia yetu, nilipokuwa chumbani nikamwambia Mungu nataka nipige hatua moja hadi nyingine mpaka niwe bilionea, yaani nizione hizo njia.
Wewe unapata wapi maarifa haya makubwa hivi?!
Naongea hivyo na Mungu wangu, simu inaita, napokea na sauti ya dada mmoja inaniita, Mambo vipi bilionea! Of course ananiitaga hivyo lakini why ananipigia simu na kuniita hivyo muda niliotoka kumuomba Mungu? Ni miezi mingi hatujawasiliana.
Unaonekana upo serious na Mungu na Mungu pia yupo serious na wewe, ni kama marafiki wa kweli.
Guys! Hizi ni code.

Unashangaa watu wanakuwa na pesa nyingi na wanaongoza kutoa. Wewe hauna pesa nyingi unakuwa mchoyo.
Laiti watu wajue siri hii, asante kwa kutokuwa mchoyo!
Majuzi nilitaka kupata ajali pale Ubungo, yaani kwa namna ilivyokuwa, nikajisemea aliyeniokoa hapa ni Mungu wala si ujanja wangu. Huyu ni Mungu dhahiri.
Ni yeye kweli kwa kuwa anakusudi bado na wewe hapa duniani.
Codes ni hizi.

1. Saidia wasiojiweza.
2. Mshukuru Mungu kwa sauti kila unapotaka kulala.
3. Ondoa chuki moyoni mwako na ujaze upendo.
Hayo ndio mambo aliyojibu Yesu Kristo alipoulizwa: Dini ya kweli ni ipi? Akajibu;
1. kusaidia yatima na wajane na kujilinda na dunia usitende dhambi.
2. Mshukuru Mungu wa miungu kwa maana fadhili zake zadumu milele.
Yesu alipoulizwa amri kubwa zaidi ni ipi? Alijibu:
3. Mpende Bwana Mungu wako wa moyo wako wote, na mpende na jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
Hizo ndio code zenyewe za Ufalme wa Mungu.
Fanya hivyo, mwezi ujao utaniletea majibu.
Ninaishi hivyo siku zote na sijapungukiwa na kitu kwani Mungu ni mwaminifu kwa rafiki zake, wale waijuao sheria yake na kuifuata!
By the way... Pasaka hii tunakwenda kulisha wale watoto kama kawaida yetu.
Na Mungu atatubariki kama kawaida yake kwani tumefanya kuwasaidia watu wake kuwa kawaida yetu!
 
Back
Top Bottom