Ni ktk bajeti hii wabunge wa chadema wakiongozwa na waziri kivuli wa wizara ya fedha, ZITTO ZUBER KABWE(ZZK), kwa mara nyingine wanajaribu kuwashawishi wabunge wa ccm na vyama vingine, wajiondolee posho za vikao mbalimbali, na badala yake fedha hizo zikatumike kwa manufaa ya umma. Ni jambo la kupongeza na zuri, na mimi natamani lingetendeka jana badala ya leo. ZZK amekwenda mbali kidogo hadi kufikia hatua ya kumwandikia barua katibu wa bunge akimtaka asimamishe malipo ya posho kwake na badala yake fedha hiyo iende kwenye akaunti ya ngo ya KDI. Safi sana.
Kwa muelekeo, hadi hivi sasa hoja hii nzuri inaelekea kushindwa kwani inapambana na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa ccm. Nina uhakika mwisho wa siku hoja hiyo iliyo kwa ajili ya manufaa ya umma na taifa itashindwa na haitatekelezwa.
Baada ya kushindwa hoja hiyo, nini kifanyike?
(i)Wabunge wa chadema waendelee na msimamo huo. Na kwa pamoja wahakikishe wanakubaliana kwa dhati.
(ii) Wafungue akaunti benki, ambayo itazikusanya fedha zao zote wanazolipwa kama posho.
Baada ya kukusanywa fedha hizo zifanye kazi gani?
(i) Zitumike ktk kuimarisha miundo mbinu ya chama, hii ni pamoja kujenga au kununua majengo ya ofisi za mikoa yote ya tz.
(ii)kununua vifaa vya uenezi kama maspika na amplifier ktk kila wilaya.
(iii)kugharamia shughuli zote zinazohusiana na chama chetu chadema.
Ndugu wana chadema wenzangu, kama tupo sirias, na hoja yetu ikakataliwa bungeni. Basi tuzigeuze pesa hizo kuwa mwiba kwa ccm kwa kuimarisha chama chetu. Endapo tutaweka mikakati mizuri na tangible juu ya pesa hizo, wao wenyewe ccm watapeleka hoja kuziondosha posho hizo kwani tumezigeuza kuwa miiba ktk miili yao. Wakikataa kuziondosha, tusizikatae, tuzichukue tuimarishe chama chetu kama nilivyoshauri.
Naomba kuwasilisha.