POSHO: Kuanzia Bungeni Hadi Kwenye Maandamano.. Watanzania na ulaji..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,534
40,160
Leo ni Mei Dei... baadhi ya mashirika na idara za serikali ambazo zinashiriki maandamano zinalipa wafanyakazi wake posho ya kuja kuandamana na mabango. Mojawapo ya mashirika yanayofanya hivyo ni la ATC ambapo leo wale wote walioshiriki maandamano walikusanyika Mnazi mmoja na kujiandikisha (kwa ajili ya posh) na kuelekea uwanja wa Taifa.

Hivi, kweli kuna ulazima wa kulipa watu kuandamana au ndiyo namna nyingine kumegeana kula. Wenyewe wakitoka uwanja wa Taifa basi wanarudi Terminal One kulipokea dege lao kubwa linalokuja na nusu ya viti vichakavu...

kazi ipo...
 
Mi naona wakazichukue tu...si wanajua wanachochukua mabosi wao..na zaidi wanajua aliyekuwa bosi wao mkubwa Chenge alikuwa na vijisenti vyake nje ya nchi..they have got nothing to loose..wamekata tamaa!
 
kwani maandamano maana yake nini?? je ni sehemu ya kazi?? ni kutaka kufahamu tu sio pingamizi wakulu
 
Mimi nilidhani watu wanaandamana kuunga mkono kitu fulani si kwa sababu wanalipwa. Je zikiondolewa posho za maandamano watu wataendelea kuandamana au idadi itapungua?

Yawezekana wakati mwingine tunaona watu wa kampuni fulani wanapita mbele ya mgeni wa heshima kwa furaha si kwa sababu wanafurahia kilichowaleta hapo bali wanapigia mahesabu 'posho ya bajeti'?

Hivi si watu wanalipwa kwa mwezi, sasa na hiyo siku ya maandamano si imo ndani ya mwezi huo? Ni sawa na posho ya kikao, ambapo kikao cha ndani ya kujadili mikakati mipya watu wanalipwa posho...
 
Mwanakijiji,

Nafikiri kwa kuwa mizizi yote ya RUSHWA na UFISADI imetanda hadi katika maofisi yote, basi watu hawaoni hata haya kudai hio fwedha ya bure ambayo huwa ni kama kipooza jasho wakidhania hio ni sifa.

Lakini sisi huku ughaibuni tunachapa kazi na tutapumzika kuanzia Ijumaa hadi Jumatatuu.... Si unaona logic hapo? Maana yake kazi zote zimalizwe Ijumaa na Tukirudi Jumanne ni mambo mengine kabisaa (lakini samahani wale wafanzao weekend)

Hapo uzalishaji na tija vinaongezeka bila kuathirika na maandamano yasiyo kichwa wala miguu hayana nafasi kabisaaa...
 
Mimi nilidhani watu wanaandamana kuunga mkono kitu fulani si kwa sababu wanalipwa. Je zikiondolewa posho za maandamano watu wataendelea kuandamana au idadi itapungua?

Yawezekana wakati mwingine tunaona watu wa kampuni fulani wanapita mbele ya mgeni wa heshima kwa furaha si kwa sababu wanafurahia kilichowaleta hapo bali wanapigia mahesabu 'posho ya bajeti'?

Hivi si watu wanalipwa kwa mwezi, sasa na hiyo siku ya maandamano si imo ndani ya mwezi huo? Ni sawa na posho ya kikao, ambapo kikao cha ndani ya kujadili mikakati mipya watu wanalipwa posho...

Mkuu Mwanakijiji, unamkumbuka waziri wa fedha alisema tunahitaji miaka 40 kufika huko? Ukipiga kima cha chini kuwa ni shilingi 80,000, ni wazi kuwa kwa kuendelewa kuishi kwa kima hicho naweza kusema kuwa bila hizi 'posho' ambazo unaweza kuziona kuwa zinatokana na ufisadi au zenye harufu ya ufisadi, watu wote wangeshaacha kazi...in fact haiwezekani kwa jinsi maisha yalivo juu sasa hivi

Ndio maana inabidi wabuni 'vimiradi' kama hivi vya maandamano walau anaweza kupata apo ada ya shule, sare na kodi ya nyumba....its so hard!
 
Jana kuna mahali(mada ya Mwanahaki kuhusu kero ya usafiri Dar) niliandika kwamba mifumo ya uendeshaji hapa Tz ni mibovu; na inaachwa katika hali hiyo kwa sababu inakuwa ni mifereji ya kutiririsha kipato haramu cha lazima kuongezea kwenye kipato halali kidogo ikilinganishwa na gharama za kuishi.

Hili la kuwalipa watu ili waende kwenye maandamano ni mfano halisi. Kwa habari nilizonazo wengine hulipwa elfu 20+ kwa tukio kama hili. Zinasaidia kusukuma siku. Mabosi wanaiba. Wafanyakazi wa chini hugawiwa kidogo, au kuachiwa mianya ya kujitengenezea chochote.

Katika hili: Serikali ya CCM inajijengea mazingira ya "kupendwa" miongoni mwa watumishi wa serikali na umma.
 
Ndio maana mojawapo ya majaribu yanayozunguka kichwani mwangu ni lile la kukubali yaishe. Hii vita ni kubwa mno kiasi kwamba ushindi tunaweza tusiuone katika maisha yetu..
 
Leo ni Mei Dei... baadhi ya mashirika na idara za serikali ambazo zinashiriki maandamano zinalipa wafanyakazi wake posho ya kuja kuandamana na mabango. Mojawapo ya mashirika yanayofanya hivyo ni la ATC ambapo leo wale wote walioshiriki maandamano walikusanyika Mnazi mmoja na kujiandikisha (kwa ajili ya posh) na kuelekea uwanja wa Taifa.

Hivi, kweli kuna ulazima wa kulipa watu kuandamana au ndiyo namna nyingine kumegeana kula. Wenyewe wakitoka uwanja wa Taifa basi wanarudi Terminal One kulipokea dege lao kubwa linalokuja na nusu ya viti vichakavu...

kazi ipo...

MwKjj,

Hiyo ndiyo Bongo, usidhani imebadilika. Tena ukombozi unaoimbwa hapa juu ya ufisadi na madhila mengine; labda kizazi kijacho ndio watakaokamilisha hii kazi.

Watanzania wamezoea hata mikutano ya kampeni wengi hupewa posho kabla ya kuhudhuria na kushangilia kwa nguvu; hapa ni kwa vyama vyote na ukubwa wa mkutano hutegemea uwezo wa kifedha wa chama husika.

Kuna posho za vikao! Mtu anatoka nyumbani kwenda kazini, wanaitisha mkutano unaohusu kazi hiyo hiyo, kisha wanalipwa posho kwa kikao ambacho hakizidi muda wa masaa 3, tena pesa nyingi tu!

Aliyekuwa M/kiti wa bodi ya ATCL, aliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya NBC wakati wa utawala wa 'Mr. Clean' na akahoji uhalali wa posho za aina hii; matokeo yake akalazimishwa kujiuzulu ujumbe wa bodi!

Posho hizi nilikuwa naziona Chuo kikuu Mlimani enzi hizo wakati wa vikao vya Faculty board na Senate; wanafunzi wengi walikuwa wanagombea uwakilishi huo kutokana na hiyo incentive kisha wanasaidia ku-rubberstamp maamuzi ya vikao.
 
Jana kuna mahali(mada ya Mwanahaki kuhusu kero ya usafiri Dar) niliandika kwamba mifumo ya uendeshaji hapa Tz ni mibovu; na inaachwa katika hali hiyo kwa sababu inakuwa ni mifereji ya kutiririsha kipato haramu cha lazima kufidia kipato halali kidogo ikilinganishwa na gharama za kuishi.

Hili la kuwalipa watu ili waende kwenye maandamano ni mfano halisi. Kwa habari nilizonazo wengine hulipwa elfu 20+ kwa tukio kama hili. Zinasaidia kusukuma siku. Mabosi wanaiba. Wafanyakazi wa chini hugawiwa kidogo, au kuachiwa mianya ya kujitengenezea chochote.

Katika hili: Serikali ya CCM inajijengea mazingira ya "kupendwa" miongoni mwa watumishi wa serikali na umma.
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni; wenzetu Bongo wanatoa posho ili watu waandamane; lakini katika baadhi ya mataifa ya Africa mf. Ethiopia, askari hupita nyumba hadi nyumba siku hiyo na wanahakikisha watu wote wanashikriki.
 
Hali ya uchumi ni mbaya na watu wetu wanalipwa mishahara ya masikhara isiyoweza kukidhi mahitaji hata ya mtu mmoja pekee. Hii hali inasababisha wafanyakazi wabuni mbinu nyingi sana (halali na ziso halali) za kujiongezea kipato, na sasa imefikia hatua kuwa umaskini wa wafanyakazi unatumika kama chombo cha kuwanyanyasa na kuwalaghai kuingia hata katika mambo wasiyoyataka au kuyaunga mkono kwa dhati. Mugabe ametumia mbinu hii huko Zimbabwe kudororesha harakati za mageuzi, mfano majuzi chama cha upinzani cha MDC kiliitisha mgomo nchi nzima kupinga kuzuiliwa kwa matokeo ya uchaguzi, lakini wafanyakazi waliogopa kushiriki wakihofia "tutakula nini?" Na hata hapo Bongo kama wewe ni kiongozi eneo la kazi mwenye bajeti unayosimamia, ukitaka wafanyakazi wakupende, kila siku wakuombee dua njema na wakupiganie hadi mwisho dhidi ya yeyote anayenyemelea "mkate" wako, basi uwe mbunifu wa warsha, semina, makongamano nk ambayo utawashirikisha wafanyakazi wakapatieko "vijisenti", utapendwa mno! Nadhani hayo maandamano inaweza kuwa ni mradi wa baadhi ya vigogo huko ATC ya ku-consolidate nafasi zao, kwa hiyo wanawamotisha washiriki kwa huto tujisenti.
 
Mwanakijiji! Nakubaliana na hoja yako na Kakalende! Hii kusema eti mshahara mdogo , wacha wachukue maana mabosi wanachukua is WRONG! And our mind has been corrupted just as our souls! It is ridiculous! Kama overtime ieleweke, lakini MayDay maandamano si suala la posho, ni suala la activism and we lack that BIG time!
Alafu mnashangaa CCM bado wanashika hatamu, tunabaki kupigia kelele ufisadi. Tusimlaumu Chenge au fisadi yeyote yule, wao walikuwa wajanja zaidi yetu, walikuwa wamepewa nafasi nzuri zaidi lakini ole wenu wale wa chini wakipata nafasi hizi nao wataendelea "kuchuma"!
Sasa fikra kama hizi ndizo ninazopiga vita na ninasema the time has come to change our mind set.
Kama mshahara hautoshi fanyeni MAANDAMANO kama wenzenu huko Turkey, Ufaransa na Latin America walivyofanya on MayDay na si kukubali kupoozwa na posho!
 
Mkuu acha tu wakatafune hako kakeki kadogo...maana wakubwa zao wameshafanya kufuru what do you expect??? Let them eat!!! Mbuzi hula mwisho wa kamba yake bwana
 
Ndio maana mojawapo ya majaribu yanayozunguka kichwani mwangu ni lile la kukubali yaishe. Hii vita ni kubwa mno kiasi kwamba ushindi tunaweza tusiuone katika maisha yetu..

Ushindi gani unaotegemea kuuona ktk maisha yako?

Ni vigumu sana kwa mtu kubadilika jinsi alivyo....(...had to rub that in...)
 
At least hatuko kwenye denial...
Mlioko kwenye denial hali halisi inawasuta...Lol
Nyani, kutokuwa katika denial siyo justification ya hii malady... tunaweza kuwa tunasutwa na hali hii kwa sababu ya inevitability ya kuwa tunaishi pamoja na ma-propagator katika jamii, lakini si kwa makusudio wala matendo yetu. Inseparability ya belonging na acceptance yake ndicho chaonekana chanzo cha kujisuta hapa.

SteveD.
 
Tatizo la Tanzania siyo fedha au mishahara. Tatizo ni kuwa mishahara inavyolipwa ndiyo kiini cha ufisadi. Hata hapa US wangeanza kulipa mishahara kama nyumbani kungekuwa na rushwa kila mahali. Wenzetu ndivyo walivyo, na sisi ndivyo tulivyo kwani hata tunapojua njia ya kupunguza rushwa hatutaki kufuatilia kwa sababu we can't imagine living without it, but we can't stand it either... its like that proverbial cake.. you can't have it and eat it too..
 
Back
Top Bottom