ngungwangungwa
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 642
- 554
Umofia kwenu
Wanajamvi.
Naomba Kwa mjadala huu tujikite kwenye Hoja bila mihemko, kila mtu anafahamu jamii forum Ndiyo jukwaa pekee huru linaloibua mijadala mikubwa na kutoa suluhisho.
Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani papa Francis Hivi karibuni alitoa waraka unaodaiwa kuwa wa mashaka. Kauli iliyoleta mkanganyiko zaidi hapa nchini kwetu ni kauli yake ya kutaka makasisi wa Kanisa katoliki kote Duniani KUWABARIKI WAPENZI WA JINSIA MOJA.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkali zaidi hasa kwenye mitandao ya kijamii. Na makasisi wa Kanisa katoliki baadhi yao kutumia mahubiri ya Noel kukataa agizo hilo.
Lakini Hebu tuangalie Kwa makini liko wapi kosa la Kiongozi huyo wa kidini anayeheshimika zaidi Duniani!? Kimsingi papa kwenye kauli yake bado alisimamia msimamo wa Kanisa kwamba "Ndoa ni kati ya mume na mke" na ndoa za jinsia moja ni DHAMBI. Kuhusu baraka papa alisema Kanisa linaweza KUMBARIKI MTU na si kubariki Ndoa ya jinsia moja.
Maana yake ni kwamba mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja Anaweza kuombewa yeye Kama yeye akihitaji Msaada wa Kanisa Lkn Kanisa halitabariki uhusiano wake Yaani ndoa yake ya jinsia moja.
Hebu Wanajamvi mnisaidie, kosa hapo la papa liko wapi!? Kwa sababu Kanisa halifanyi Kazi ya kubagua watu.. Kanisa Kazi yake ni kuwahubiri watu juu ya ufalme wa mbingu. Kama watu wanalalamika kuwabariki mashoga wakija kanisani, vipi kuhusu wanaotenda dhambi zingine km mauaji, uchawi, wizi, uzinzi nk nao Kanisa litawatenga!? Au shoga anatenda dhambi kubwa zaidi kuliko mauaji, wizi nk!??
Mbona hata Yesu alisema Sikuja kuwaita watu wema wapate kutubu bali wenye dhambi!? Kwa nini leo tunataka kuwatenga na kuwabagua wapenzi wa jinsia moja!? Hivi Kanisa lisipowaombea na kuwabariki wataacha vp kufanya huo uchafu!?
Kanisa likikaa kimyaa na kuwabagua mashoga, ina Maana ushoga Ndiyo hautakuwepo!? Kwa nini watu wanataka Kanisa lisichukue hatua madhubuti za kukabiliana nalo Kwa sababu ni tatizo lililopo katika jamii!?
Tujadili..