Pope Francis: Ndoa za jinsia moja ni dhambi lakini wahusika wakaribishwe kanisani wasitengwe na ikibidi kupewa baraka

John Gregory

JF-Expert Member
Jul 14, 2019
1,060
1,957
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani ametoa waraka unaoelezea kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la mahusiano baina ya waumini. Katika waraka huo Kiongozi huyo ameruhusu makasisi wa kanisa hilo kuwapokea na ikibidi kuwabariki wale wanaojihusisha na mahusiano ya jinsia moja.

Akisisitiza kwamba daima kanisa halipaswi kuwasukuma waumini mbali na kanisa bali linapaswa kuwaleta karibu bila kujali hali zao za kiroho na kusema kama jinsi mvua iwanyesheavyo wema na waovu ndivyo kanisa linapaswa kuwapokea na kuwapa mafundisho wale wote wanaoenda kinyume na miongozo ya kanisa.

Pia kiongozi huyo amesisitiza kwamba kamwe hii haihalalishi mahusiano hayo na daima haiwezi kuwa mbadala wa Sakramenti ya Ndoa Takatifu.

GBspNAjXoAAtOQH.jpeg
GBspNAlW0AABqWi.jpeg
 
Hali si Hali huko Vatican na Kanisa Katoliki Duniani Kwa Papa Francis kubadili GIA Angani akidai watu wanapotosha taarifa ya mafundisho yake.

Adai kinachotakiwa Kubarikiwa ni vitu vyao ila sio Ndoa zao 🤣🤣🤣

My Take
Acheni kutapatapa,Kwa asili yake RC linakubaliana na Ushoga ndio maana Kwa miaka Mingi Makasisi wake Wana kashfa za ulawiti na Kanisa Huwa linaficha.
 
Kwamba papa anabariki kazi na vitu vya mashoga ila sio mashoga wenyewe, hizo akili ama bangi?

Kwamba kitimoto huli ila mchuzi wake unakunywa.

Watu wakiambiwa hizi dini ni taasisi za kitapeli Mungu hayupo watu hawataki kuelewa.

Sasa huyo ni Mungu gani asie na akili ambae yeye mwenyewe hataki ushoga ila ameruhusu watu wake kama Papa wabariki kazi za mashoga,.
 
K
Hali si Hali huko Vatican na Kanisa Katoliki Duniani Kwa Papa Francis kubadili GIA Angani akidai watu wanapotosha taarifa ya mafundisho yake.

Adai kinachotakiwa Kubarikiwa ni vitu vyao ila sio Ndoa zao 🤣🤣🤣

My Take
Acheni kutapatapa,Kwa asili yake RC linakubaliana na Ushoga ndio maana Kwa miaka Mingi Makasisi wake Wana kashfa za ulawiti na Kanisa Huwa linaficha.
Komaa na dhambi zako. Hutaenda mbinguni kwa kumuangalia mtu na dhambi zake
 
Hali si Hali huko Vatican na Kanisa Katoliki Duniani Kwa Papa Francis kubadili GIA Angani akidai watu wanapotosha taarifa ya mafundisho yake.

Adai kinachotakiwa Kubarikiwa ni vitu vyao ila sio Ndoa zao 🤣🤣🤣

My Take
Acheni kutapatapa,Kwa asili yake RC linakubaliana na Ushoga ndio maana Kwa miaka Mingi Makasisi wake Wana kashfa za ulawiti na Kanisa Huwa linaficha.
Huyo naye ni papa wa ajabu kuwahinkuchaguliwa. Mara nyingi nimeona akiwasukuma watu wanayotamka kumsalimia kwa Mila na destiri za kikatoliki kwa kulamba Pete,
Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa kidunia anatdkiwa atoe statement ambazo ni unambiguous ambazo hazitaleta absurdity.

Kwa nini aitoe hiyo kauli? Na kwa nini atoe press kuzungumzs vitu ambavyo ni dhambi kwenye kanisa? Tena kipindi hiki muhimu kwa kalenda ya kanisa kukumbuka kuzaliwa kwa Kristu?

Si ni juzi tuu kamtimua Askofu wa marekani aliyekuwa anapinga ndoa za jinsia Moja? Kwa nini alimtimua halafu muda mfupi anatoa statement ya hovyo namna hiyo?

Anawapa kazi makardinali na maaskofu kutetea kauli hiyo ya hovyo kujaribu ku construe kwamba halumaanisha hivi alimasnisha vile.

Makardinali wafanye maamuzi magumu wamtengue huyu mtu laa sivyo ataliparaganyisha kanisa. Huo usasa wake haupo kwenye kanisa.

Kwanza kashaa badilisha mambo kibao kwenye litrujia mfano BWANA AWE NANYI tulikuwa tunajibu AWE PIA NAWE, lakini yeye kale kitu tofauti eti AWE ROHONI MWAKO. Yaani sisi waamini haitakiwi Mungu awe rohoni mwetu ni wao tu? Mimi siwezi kubadilisha nitaendelea kutamka tena kwa nguvu AWE PIA NAWE
 
Kwamba papa anabariki kazi na vitu vya mashoga ila sio mashoga wenyewe, hizo akili ama bangi?

Kwamba kitimoto huli ila mchuzi wake unakunywa.
Kwani lengo la Mungu ni kwa ajili ya watu wasafi au kuokoa wenye dhambi?
 
Back
Top Bottom