Waumini wa Kanisa Katoliki tugome kwenda kanisani kwa shinikizo la viongozi wetu kumhoji Papa Francis, Vitu anavyoruhusu ni kinyume na Kanisa letu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ingefaa sana waumini wote tugome, Muda ni sasa !! ikibidi makanisa ya Tanzania kujitenga na vatican kama kanisa la anglican walivyojitenga kuongozwa na kanisa la uingereza.

Makadinali wamueleze huyu papa achague upande, mambo anayoruhusu tayari yamehukumiwa na Mungu kwenye biblia Papa Francis yeye ni nani apindishe ?

Tangu jana nimesikia kuna waraka lakini nikakaa nikatulia na kuvuta pumzi kisha nikausoma waraka huo mimi mwenyewe maan maana sijawahi kuamini vyanzo vya habari kama bbc, Nilichogundua ni kwamba vyombo vya habari viliongezea chumvi (Propaganda) kwamba Papa Francis karuhusu ndoa lakini baada ya kuusoma waraka mimi mwenyewe bado nimesikitika kwasababu Papa karuhusu makasisi kubariki wapenzi wenye mahusiano ya jinsia moja ila anasisitiza Ndoa itabaki kuwa vilevile kati ya mwanaume na mwanamke, kuna utofauti gani sasa ? 😔😔 haikutosha hivyo nikatumia mpaka akili bandia ya Chat Gpt inisiaidie kuelewa vizuri zaidi lakini mambo ni yale yale tu.

Dini watu tumezifuata kwa sababu ya kutarajia kwamba zinatoa muongozo fulani kwa watu kuhusu maadili, usiibe, usizini, mpende jirani yako kama unavyojipenda, usitumie viungo kwa kazi ambayo havijaumbiwa, nk ,

Hii ndio ilifanya hata wazazi wetu na sasa tumekuwa wakubwa sisi wazazi kupeleka watoto wakafindishwe dini,

Ila kwa mambo yanayoendelea sasa ni mashaka tele, mtoto anaona jinsi papa anavyoheshimiwa kama kiongozi wa dini alafu anasikia ni huyo huyo anaruhusu vitu flani kinyume kabisa na maandiko, hii ni mbaya sana kwakweli, mtoto anakuzwa aone ni sawa na ni kawaida kufanya ufuska mwishowa nae anaweza kushawishika kuufanya hata kama wazazi hatumpi bataka ataenda kwa makasisi waliopewa go ahead na papa wabariki ufuska.

Ni muda sasa waumini nao wasikilizwe,
 
Ingefaa kanisa la waumini wote tugome, ikibidi makanisa ya Tanzania kujitenga na vatican kama kanisa la anglican walivyojitenga kuongozwa na kanisa la uingereza...
Wakatoliki Bwana!!

Nyie uovu was kanisa hili haujaanza Leo!!

Mengi ni ya sirini hayafunuliwi,muda wa kufunuliwa umefika na ndio huu!!

Shukuru kwamba umetambua mapema kuliko kushupaza shingo!!

Kimbia sasa kimbia!!
 
Ingefaa kanisa la waumini wote tugome, ikibidi makanisa ya Tanzania kujitenga na vatican kama kanisa la anglican walivyojitenga kuongozwa na kanisa la uingereza...
Hamuwezi goma unajua kitu kinaitwa behaviors or pattern of your daily life that are imprinted into your subconscious mind. Jiulize why Malaya ama mwizi,mvuta sigara ama mnywa pombe hawachi hizo Tabia. Ama mvivu kawa na nguvu na mwenye nguvu akawa mvivu.
 
Wakatoliki Bwana!!

Nyie uovu was kanisa hili haujaanza Leo...
Owwww !! inauma sana mkuu, wanachotaka kukifanya ni kuvuruga watoto wetu hawa wabichi waone ni kawaida kufanya ufuska, hata nguvu ya mzazi kukaripia ufuska haipo kwasababu makasisi wamepewa kibali cha kubariki.

Naanza kuona ni heri niende usabatoni, walianza Anglican sasa ni Katoliki sio muda hii ngoma inahamia Lutheran.
 
Ingefaa kanisa la waumini wote tugome, ikibidi makanisa ya Tanzania kujitenga na vatican kama kanisa la anglican walivyojitenga kuongozwa na kanisa la uingereza...
Msingi wa kanisa ni uongo kwamba Mungu yupo, wakati Mungu hayupo.

The problem of evil shows that your God (omnipotent, omniscient, all loving) does not exist.

Ukianzia hapo, hayo madudu mengine ya contradictions kanisani, mipasuko etc, haitakushangaza.

Huyo Mungu hayupo jamani nawaambia kila siku.

Huo uongo mnaodanganyana kwamba kuna Mungu ndiyo mzizi wa matatizo, haya mengine matawi tu.
 
Wakatoliki Bwana!!

Nyie uovu was kanisa hili haujaanza Leo!!

Mengi ni ya sirini hayafunuliwi,muda wa kufunuliwa umefika na ndio huu!!

Shukuru kwamba umetambua mapema kuliko kushupaza shingo!!

Kimbia sasa kimbia!!
Vipi uovu wa Kanisa lako mbona huuweki hadharani?."Unaposema ubaya wa wenzako,jitahidi pia kusimulia na uovu wako"-Msg kwenye gari moja kubwa.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom