Polisi wanawahujumu CCM na Serikali yake?

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Habarini za Tarehe 14 hii ya leo wapendwa?.

Kwa namna Jeshi la Polisi limetenda kumkamata Joseph Mbilinyi kule mbeya Katika mazingira ambayo wala hayakuhitajika kumkamata mgombea huyo wa ubunge aliyeenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge baada Ya kupitishwa na chama chake

Mitazamo kadhaa kinzani imenijia kichwani pangu na kuona nishirikiane nanyi kutafuta walau suluhu ya maono

Ninajiuliza na naomba tujiulize, je palikuwa na ulazima gani wa polisi kumkamata Sugu aliyeonekana kuwaingiza mkenge mbele ya Camera za waandishi?

Je, hivi hawa polisi hawakumsikia amiri jeshi mkuu JPM alipowahakikishia watanzania uchaguzi huru na haki na kuvitaka vyombo kutokutumia nguvu kubwa isiyo na sababu?

Je, Polisi hawa wa mbeya hawakuwaona wenzao wa Dar walivyomsindikiza Tundu Lissu kwa amani na utulivu kutoka amewasili uwanja wa ndege hadi makao makuu ya chama chake?. Nani kamtuma huyu polisi kumkamata Sugu?. Ni sirro au Chalamila?.

Hivi hawa polisi huku mikoani hawafahamu kuwa pindi tu wanapomkamata mwanasiasa hasa wa upinzani wao polisi huondolewa kwenye tuhuma na badala yake tuhuma hupelekwa CCM na kwa Magufuli hata kama hawajawatuma kufanya hivyo walivyofanya?.

Je, hizi tetesi zinazosemekana kuwa pana mashirikiano ya kimkakati baina ya polisi wa baadhi ya mikoa kama Mbeya, Songwe, Tabora, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na kwengineko yanayowataka polisi hao kuwakamata na kuwapiga mabomu viongozi wa upinzani matukio ambayo wapinzani hao huyatumia kisiasa. Tuuamini ukweli huu

Hivi kama si Polisi kumkamata Sugu leo, nani angejua kuwa Sugu amechukua fomu ya ubunge leo?.

Mbona tumeona baba Mchungaji Msigwa amechukua fomu na hakuna aliyehangaika nae na habari yake ikaishia kwenye makundi tu ya Whatsapp za Chadema?.

Mbona tumemuona meya wa Ubungo mstaafu kachukua fomua c yeye na bodaboda alizokodi tu wenzake na habari kuishia kwenye makundi ya Whatsapp ya chama chao tu?.

Nawaona polisi wakimkwamisha Magufuli kwa kukubali kucheza ama kuchezeshwa michezo ya chadema muda mchache ujao.
 
Ukitafakari kwa makini si kwamba polisi wanaipenda ccm Bali wanafarakanisha watz na ccm kwa kuwashughulikia wapinzani ili lawama zote ziende kwa CCM.

Mfano check hili la Mbeya Ackson Tulia alienda na msururu wa wasindikizaji kuchukua fomu but Sugu wamemzuia eti anafanya maandamano, hizi Ni kupandikiza chuki ili watz waichukie ccm na serikali yao
 
Huyu RPC wa Mbeya amesha kuwa babu. Nakumbuka hata IGP alishwa mwambia hastahili tena kuendela kuwa RPC arudi Makao Makuu awaache vijana site.

Sijui ana ngangania nini kuendelea kuwa RPC kwa style za kizamani.. Sasa amesha mpaisha Sugu..
 
Wapinzani watumieni polisi positive ili kukamatwa kwenu kuwajenga kisiasa maadamu tu msivunje sheria
 
Ukitafakari kwa makini si kwamba polisi wanaipenda ccm Bali wanafarakanisha watz na ccm kwa kuwashughulikia wapinzani ili lawama zote ziende kwa ccm. Mfano check hili la Mbeya Ackson Tulia alienda na msururu wa wasindikizaji kuchukua fomu but Sugu wamemzuia eti anafanya maandamano, hizi Ni kupandikiza chuki ili watz waichukie ccm na serikali yao
Tulia alienda lini kuchukua fomu?. Za chama gani kaka.
 
Wamempaa Kiki ya bure tu huyo sugu ila kwa namna watu wa mbeya wanavyo mjadili sugu ni wazi wamemchoka na drama zake,watu wa mbeya wanata maendeleo na sio Tena vioja vya sugu
 
Tatizo la Mbeya ni jinsi ya ubebwaji wa yule MAZA wa uspika inakuwa ntiani nkubwa.. ....

CCM inatia huruma mida mingine!!...tuwe wakweli.
 
Back
Top Bottom