Polisi Mbeya: Ulinzi waimarishwa kuelekea uchaguzi mdogo wa Ubunge Mbarali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga vyema kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbarali.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 18, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga amesema, "Vikosi vyote vya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya vipo imara na vipo kazini kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa maeneo yote ya Wilaya ya Mbarali" alisema Kamanda Kuzaga.

Mbeya.JPG
Aidha, Kamanda Kuzaga amewataka wananchi wenye sifa na vigezo vya kupiga kura kwenda kwenye vituo vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kumchagua mbunge wa jimbo lao bila hofu yoyote kwani ulinzi na usalama ni wa kutosha.

Jumla ya vyama vya siasa nane vinashiriki uchaguzi huo ambavyo ni CCM, ADC, UPDP, DP, NLD, UDP, TLP na ACT WAZALENDO.

Uchaguzi huu unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mbarali kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Francis Leonard Mtega kufariki dunia baada ya kugongwa na Trekta @ Power Tiller Julai mosi 2023 huko wilayani Mbarali.

Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbarali utafanyika Septemba 19, 2023 siku ya jumanne.
 
Ulaji wa watu huo, ngoje niendelee kupambania tonge langu.
 
Huu ni uchochezi ionekane hakuna amani wakati wa uchaguzi, lakini uchaguzi ukiwa wa haki, huru na bila vitisho wapiga kura hawana tatizo na mtu.

Hii ya kuwatia hofu wapiga kura inaweza kutafsiriwa ni mbinu ya kuvuruga uchaguzi maana kutisha watu wasijitokeze kwa kuwa kuna ruhani / ghost asiyekuwepo anayeitwa jina la Kukosekana Amani ni kuingilia mchakato huru wa uchaguzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom