Polisi wanawahujumu CCM na Serikali yake?

Polisi wanawahujumu CCM na Serikali yake?

Habarini za Tarehe 14 hii ya leo wapendwa?.

Kwa namna Jeshi la Polisi limetenda kumkamata Joseph Mbilinyi kule mbeya Katika mazingira ambayo wala hayakuhitajika kumkamata mgombea huyo wa ubunge aliyeenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge baada Ya kupitishwa na chama chake

Mitazamo kadhaa kinzani imenijia kichwani pangu na kuona nishirikiane nanyi kutafuta walau suluhu ya maono

Ninajiuliza na naomba tujiulize, je palikuwa na ulazima gani wa polisi kumkamata Sugu aliyeonekana kuwaingiza mkenge mbele ya Camera za waandishi?

Je, hivi hawa polisi hawakumsikia amiri jeshi mkuu JPM alipowahakikishia watanzania uchaguzi huru na haki na kuvitaka vyombo kutokutumia nguvu kubwa isiyo na sababu?

Je, Polisi hawa wa mbeya hawakuwaona wenzao wa Dar walivyomsindikiza Tundu Lissu kwa amani na utulivu kutoka amewasili uwanja wa ndege hadi makao makuu ya chama chake?. Nani kamtuma huyu polisi kumkamata Sugu?. Ni sirro au Chalamila?.

Hivi hawa polisi huku mikoani hawafahamu kuwa pindi tu wanapomkamata mwanasiasa hasa wa upinzani wao polisi huondolewa kwenye tuhuma na badala yake tuhuma hupelekwa CCM na kwa Magufuli hata kama hawajawatuma kufanya hivyo walivyofanya?.

Je, hizi tetesi zinazosemekana kuwa pana mashirikiano ya kimkakati baina ya polisi wa baadhi ya mikoa kama Mbeya, Songwe, Tabora, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na kwengineko yanayowataka polisi hao kuwakamata na kuwapiga mabomu viongozi wa upinzani matukio ambayo wapinzani hao huyatumia kisiasa. Tuuamini ukweli huu

Hivi kama si Polisi kumkamata Sugu leo, nani angejua kuwa Sugu amechukua fomu ya ubunge leo?.

Mbona tumeona baba Mchungaji Msigwa amechukua fomu na hakuna aliyehangaika nae na habari yake ikaishia kwenye makundi tu ya Whatsapp za Chadema?.

Mbona tumemuona meya wa Ubungo mstaafu kachukua fomua c yeye na bodaboda alizokodi tu wenzake na habari kuishia kwenye makundi ya Whatsapp ya chama chao tu?.

Nawaona polisi wakimkwamisha Magufuli kwa kukubali kucheza ama kuchezeshwa michezo ya chadema muda mchache ujao.
Polisi ndio ccm na ccm ndio polisi hatuwezi kuwatenganisha kwa maneno na vitendo vyao. Ukiangalia matukio kuanzia mbali utaona namna yule dada na ccm yake walivyo fanya kampeni na kutumia pesa nyingi sana. Na kimya cha upinzani kilicho sababishwa na m/kiti wa ccm kilipelekea walio wengi waamini propaganda kwamba upinzani umekufa/hauna nguvu tena kama ilivyokuwa chaguzi za huko nyuma, lakini ghafla ccm na polisi wameshtuka kuona nguvu ambayo waliamini kwamba walishaingamiza. Hivyo wanajaribu kumtafutia dada nafasi yakupita bila kupingwa kwa sababu hali imeshaanza kujionyesha kwamba kwenye sanduku la kura kuna mtihani mgumu.
Na kwa kuwa kwenye nafasi ya ubunge wa kuteuliwa kuna akiba ya jina la makonda, hivyo ni lazima dada atafutiwe nafasi kwa namna yoyote ile.
 
Wamempaa Kiki ya bure tu huyo sugu ila kwa namna watu wa mbeya wanavyo mjadili sugu ni wazi wamemchoka na drama zake,watu wa mbeya wanata maendeleo na sio Tena vioja vya sugu
Kumbe wengi tumeona hivyo
 
Polisi wanatekeleza maagizo toka juu uhutuni ,kutoka kwa mhutu.
Hapa Mimi napingana na wewe kwa jinsi navyo mjua sugu wa kipindi hiki Cha siasa za mbeya na sugu wa hippop nitofauti kabisa ,na utofauti hu umeanza tangu alivyokuwa karibu na lema,hapo ndio alipo Anza kumfundisha michezo ya drama na ndio hiyo anaendelea nayo. kwa mbeya sugu mapolisi wote kawaweka mfukono wanafanya wanavyotaka kwa maelekezo na mikakati ya sugu
 
Kuna mmoja nilikutana kwenye chombo fulani cha usafiri , sio basi, ikatokea tukawa tuna chat socially akaanza kuniambia issue za Jecha baada ya kufanya mapinduzi matukufu ya kura za wananchi 2015.

Akakiri kwamba ni kweli wanafanya tu katika kutimiza viapo vyao ila mioyo yao inawauma kwa wanayoambiwa wayafanye.

Askari wa hivyo Ni wengi kuliko wanao pokea maagizo toka juu... Kiongozi anapokea maagizo alafu wa chini yake anaenda kumponda ndugu yake... Hii inasikitisha alafu inauma Sana.
 
Back
Top Bottom