Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Waungwana wa JF, husikeni na mada ya hapo juu.
Nikiri wazi kuwa katika kufuatilia kwangu siasa za Tanzania kupitia redio, magazeti, runinga na mitandao ya kijamii, sijawahi kuona au kusikia kuhusu barua iliyowasilishwa na CCM kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waweze kuendesha maandamano ya amani au mikutano ya hadhara kwenye wilaya husika.
Imekuwa kawaida kusikia na kuona vyama vya upinzani vikiandika barua ya kutoa taarifa kwa OCD kwa ajili ya mambo hayohayo. Kuna wakati taarifa hiyo huridhiwa na upo wakati taarifa hiyo hairidhiwi kutokana na sababu za kiusalama almaarufu kama taarifa za kiintelijensia.
Je, CCM hukidhi matakwa ya kisheria na kikanuni katika kutoa taarifa Polisi? CCM wamewahi kutoridhiwa kufanya maandamano ya amani au mkutano wa hadhara?