Polisi wadai Dr Slaa alikuwa na bunduki

Polisi wadai Dr Slaa alikuwa na bunduki

mpinga shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
3,234
Reaction score
960
Polisi mkoani Arusha wanadai kuwa baadhi ya wana-CHADEMA waliokuwa kwenye Mkesha wa NMC jumatatu usiku walikuwa na silaha za moto.

Kaimu Kamanda, Akili Mpwapwa amesema kuwa Dr Wilbroad Slaa alikutwa na Bastola "Walther Pistol T2-CAR-61074-327963" wakati alipokamatwa na Bwana Daniel Ezekiel Ogongo ambaye pia alikamatwa kwenye tukio hilo akidaiwa kuwa na ‘Pietro Beretta H-447577 CAT5802'

Cha kushangaza ni kwamba wakati Polisi ikiwaburuza mahakamani wafuasi wa CHADEMA wale wanachama wa CCM ambao wiki kadhaa zilizopita walikutwa na kosa hilo hilo la kuandamana na kufanya mikutano bila kibali mjini Arusha ‘wamesamehewa' na kupewa ‘onyo kali!'

Polisi wamekiri kuwa pamoja na kwamba wakeshaji pale NMC walikuwa hawajajiandaa na walipovamiwa walikuwa tayari wamechoka kwa kuimba usiku kucha, bila chakula na kwenye mvua na baridi kali bado wasingeweza kuwadhibiti na hivyo kulazimika kutumia magari nane pamoja na lile lori lenye maji ya kuwasha.

Na haikuwa rahisi pia, pamoja na zana zote hizo.

Kama wana akili wangetakiwa kujua kuwa hakika hali inaenda kuwa mbaya.
 
Lakini Nadhani hajashtakiwa kwa kosa la kukutwa na silaha.
Katika mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Arusha leo mpaka muda huu ambao ni majira ya saa 10:29 (kumi na dk 29 jioni) Dr.Slaa na Lissu na wananchi wengine 27 wamesomewa mashtaka na yako kama ifuatavyo;

1. Kukusanyika kinyume cha sheria .
2. Kukataa kutii amri halali ya polisi

Ila Slaa kasomewa shitaka la tatu peke yake nalo ni la uchochezi, ila maneno yaliyosemwa na polisi kjuwa yalitamkwa sijui yatakuwa yalitamkwa wapi ila sio kwenye mkutano wa hadhara wa jana kama ambavyo mwendesha mashitaka anataka kuiaminisha mahakama .

Taratibu za dhamana zinaendelea kwenye mahakama hiyo , ila ntawajulisha nini kiuitatokea kwani taarifa ni kuwa Lissu na Dr.Slaa wao wataenda Kisongo kuonana na LEMA na kupafanya kuwa ni makazi ya kudumu kama ambavyo polisi na serikali wanataka .
 
Kosa la kukutwa na bastol fine yake ni Tshs. laki moja. Si mnakumbuka yule Msomali Rage alipanda nayo jukwaani kabisa kule Igunga
 
Polisi njaa hawa!...Wanangoja kufanya matukio ya utesaji ili wapate cheo!
You wont succeed that way oooh!
 
Nini cha ajabu hapa, au kwa vile Dr. Slaa ni CHADEMA. Mbona kuweka silaha kiounoni kwenye mikutano ni kawaida tu Bongo. Mbona Rage kule Igunga haikuwa issue kuwa na pistol kwenye mkutano wa Hadhara.

Acheni ujinga nyie POLICCM.
 
Kosa la kukutwa na bastol fine yake ni Tshs. laki moja. Si mnakumbuka yule Msomali Rage alipanda nayo jukwaani kabisa kule Igunga
kuna neno siwezi kuliandika humu...but hiyo silaha imetumika kumtisha mtu?je ilitolewa hadharani? ama kuna risasi iliyofyatuliwa? maana kama kuna ganda litaonyesha namba ya silaha iliyotumika. shwain
 
Wayapanue magereza maana tuko wengi ambao siku si nyingi tutaingia huko maana naona hali siyo yenyewe.
Hongereni POLICCM,ila msije kujutia maamumuzi yenu ya uonevu.
 
Tangu lini kubeba bunduki ikawa kosa? Polisi wanamjua mheshimiwa mmoja anayeitwa Rage? Or is it case of - it is ok when I do it but 'you'?
 
Nina wasiwasi na ukweli wa kamanda wa polisi. Maana swala la kubambikwa kesi huko polisi limekuwa ni jambo la kawaida!
 
Nadhani polisi ifikie sehemu waelewe kuwa haki za binadamu zitabanwa sana lakini zitainuka tu. Waangalie na wasome kwenye historia ya yaliyotokea Tunisia, Misri, na kwingineko. Watu itafikia wakati wataamua kuwa imetosha! Na ikishafika hapop watakubali chochote kile watakachoamua kukifanya.
 
Nadhani polisi ifikie sehemu waelewe kuwa haki za binadamu zitabanwa sana lakini zitainuka tu. Waangalie na wasome kwenye historia ya yaliyotokea Tunisia, Misri, na kwingineko. Watu itafikia wakati wataamua kuwa imetosha! Na ikishafika hapop watakubali chochote kile watakachoamua kukifanya.

Hii inanikumbusha yale mauaji ya wachimbaji wa Morogoro na Dereva taxi - we later learned the truth!
 
kile ninachotaka kufanya 2015,nasikia kimeanza kufanyika,kama ni kweli nitajiunga nao sasa,ili ang'oke kabla ya uko.
 
Kosa la kukutwa na bastol fine yake ni Tshs. laki moja. Si mnakumbuka yule Msomali Rage alipanda nayo jukwaani kabisa kule Igunga

Kwa Chadema sheria huwa zinabadilishwa mkuu.
 
Kwani Rage Ilikuwaje si alidaiwa laki tu???
 
Maswala ya kumiliki silaha tena kutupiana risasi kwa wanasiasa yamesemwa yametokea sana kwenye Uchaguzi Igunga na mpaka sasa hatua za msingi hazionekani zikilingana na ukali wa taarifa zilizokuwa zikitolewa ktk kipindi kile cha uchaguzi wa Igunga.

Mengi yatasemwa ili kutisha watu ila kimsingi na kiuhalali kila mwenye silaha anapaswa kuwa na silaha yake popote alipo hata mimi binafsi nilikua njugu 17 kiononi(halali) ila sikudhubutu wala sikufikiria kuigusa silaha yangu kwa sababu sikuwa na matumizi nayo kwa wakati ule pale NMC kwenye mkesha.
 
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa leo amekamatwa na polisi na baada ya kumpekua wamemkuta akiwa na Bastola 2 na risasi 17 eneo la NMC majira ya saa 11 alfajiri akiwa kwenye mkesha wa kushinikiza Lema aachiwe huru kutoka rumande.
Source Taarifa ya Habari ya Channel 10 saa moja Usiku leo
 
kwani kutakuwa na tatizo kama atakuwa anazimiliki kihalali...?
 
Back
Top Bottom