Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu

Siku wakijaribu huku Kenya,tutawarudushie majeruhi.Polisi wa Tanzania hata Kiingereza tu hawajui
Mbona Kuna Askari wenu alijaribu kuleta mambo kama haya kule kwenye boda ya Jasini, Tanga. Ashukuru viongozi wenu wa County ya kwale walikuja kupiga magoti la sivyo angeliwa kiboga
 
Hawa ndio Polisi wetu tunaowategemea kuwa makini

TAARIFA YA TUKIO LA ASKARI POLISI WETU 7 KUINGIA NCHINI MALAWI.

MNAMO TAREHE 15/09/2021 MAJIRA KATI YA SAA 16:30 - 17:30HRS HUKO MANEO YA KITONGOJI CHA MTIMA, KIJIJI CHA IKUMBILO, KATA YA CHITETE, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE NA MKOA WA SONGWE ASKARI G.3695 D/SGT RAMADHANI,H.694 PC EDWARD, H.8096 PC SAFARI, WP.12285 PC ANASTAZIA, H.9727 PC JOSEPH, H.9781 PC HUSSEIN NA H.8764 PC JUMANNE WAKIWA NA GARI PT.3676 TOYOTA L/CRUISER MALI YA JESHI LA POLISI TANZANIA WAKITOKEA VWAWA KUPELEKA WATUHUMIWA WA KESI YA MAUAJI PI.3/2020, WALIPOFIKA MAENEO YA MTIMA NA KUONA PIKIPIKI INAYOSADIKIWA KUWA IMEBEBA MAGENDO KUTOKA NCHI JIRANI YA MALAWI, WALIISIMAMISHA LAKINI PIKIPIKI HIYO ILIAMUA KUKIMBIA KUELEKEA NCHI JIRANI YA MALAWI, ASKARI. WALIAMUA KUIFUKUZIA NA KUVUKA MPAKA WA TANZANIA NA KUINGIA NCHINI MALAWI NA NDIPO WANANCHI WA MALAWI WALIIZINGIRA GARI HILO IKIWA NA ASKARI NCO G3695 DSGT RAMADHAN, H.8096 PC SAFARI, H9727 PC JOSEPH, H.694 D/C EDWARD, H.9781 PC HUSSEIN, WP.12285 PC ANASTAZIA NA H.8764 PC JUMANNE WAKIWA NA SILAHA MBILI AINA YA AK 47 NA KUANZA KUWASHAMBULIA.KWA.MAWE NA BAADAYE KUPATA MSAADA WA KUOKOLEWA NA ASKARI POLISI WA MALAWI(+) KATIKA VULUGU HIZO ASKARI MMOJA H8764 PC PC JUMANNE AMBAYE NI DEREVA ALIJERUHIWA KWA KUKATWA NA PANGA KICHWANI HALI YAKE SIO MBAYA ANAENDELEA VIZURI PIA GARI INASEMEKANA LIMEHARIBIWA KWA KUPIGWA KWA MAWE NA SILAHA AK 47 ZOTE MBILI ZIPO SALAMA NA ZIMEHIFADHIWA KITUO CHA POLISI CHITIPA MALAWI. ASKARI NO. G.3695 D/SGT RAMADHANI AMBAYE ALIKUWA KIONGOZI WAO, H.8096 PC SAFARI NA H.9727 PC JOSEPH WALIFANIKIWA KUTOROKA KATIKA VULUGU HIZO NA KURUDI KITUONI SALAMA NA WAPO MAHABUSU KWA HATUA ZA KINIDHAMU. MAWASILIANO KATI YA UONGOZI WA WILAYA NA MKOA TANZANIA NA MALAWI YANAENDELEA KWA AJILI YA KUWAREJESHA NCHI ASKARI HAO PAMOJA NA GARI NA SILAHA.
Mshika mawili moja humponyoka.Mna wahalifu wa kupeleka mahakamani na mnabadili route baada ya kuona bodaboda yenye magendo.Mungu tuhurumie!!
 
Mshika mawili moja humponyoka.Mna wahalifu wa kupeleka mahakamani na mnabadili route baada ya kuona bodaboda yenye magendo.Mungu tuhurumie!!
Wamalawi hawakopeshi bwana

1631866039202.png
 
Askari Polisi wanne wa Tanzania wanashikiliwa nchini Malawi baada ya kuvuka mpaka kwa lengo la kuwakamata wahalifu.

Askari hao walikuwa na gari aina ya Toyota Landcruise pickup ambalo limeharibiwa na wananchi. Kuharibiwa kwa gari hiyo kulitokea baada ya polisi hao kulitelekeza wakiwakimbia wananchi waliowazingira.

Polisi hao hivi sasa wanashikiliwa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo kijiji cha Ipenza.
Tena wangepigwa kipigo cha mbwa mwizi wakome kuvuka mipaka, walidhani ni Kariakoo huko?
 
Natamani ningekuwepo hapo askari wa Malawi wangekuwa na kazi kubwa ya kunizuia kuwachakaza hao PT
 
Inamaana hapo kuna tuhuma pia za wamalawi kunyanyaswa wakiwa upande wetu kitu ambacho sii kizuri
Hamna kitu Kama hicho, wamalawi mbona wanaingia tz na kutoka bila shida yeyote, sema inshu ni askali wa tz na askali wa Malawi , huwa wanakaziana kwelikweli pale mmoja anapoingia kwenye 18 za mwngine. Nawajua vzr ma pot wa Malawi nimewahi kuwa Malawi Mara kadhaa kwa wananchi hawana shida nao peace tu !!
 
Back
Top Bottom