Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu

Ila elimu angalau ya diploma na degree ni muhimu sana kwa Polis wetu, ijapokuwa kuna ulakini katika elimu yetu ya juu!

Nilijaribu kufanya utafiti kidogo, na kubaini kuna utofauti mkubwa sana wa kimawazo kati ya Polisi au mwanajeshi mwenye bachelor degree na huyo form four failure!
Mkuu wa msafara wao ni Sajenti na ni degree holder ila sijui nini tu kiliwafanya washindwe kuzingatia 'police jurisdiction'
 
Ila elimu angalau ya diploma na degree ni muhimu sana kwa Polis wetu, ijapokuwa kuna ulakini katika elimu yetu ya juu!

Nilijaribu kufanya utafiti kidogo, na kubaini kuna utofauti mkubwa sana wa kimawazo kati ya Polisi au mwanajeshi mwenye bachelor degree na huyo form four failure!
Kuhusu elimu ni popote pale.
Wenye elimu ndogo za form IV na Diploma sijui Certificate ni wasumbufu sana. Nenda Mamlaka za maji, umeme, polisi, jwtz jkt, nk.
 
Ukionja Asali Unachonga mzinga kabisaaa!!!!! Kibaya mzinga unaenda utundika SHAMBA la jirani loooo!!!
 
Polisi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya wametandikwa na Raia wa Malawi baada ya kuingia nchi hiyo ya kigeni kwa lengo la kuwasaka wafanya magendo .

Bado Haijafahamika walikopata utaratibu huo wa kuingia nchi ya watu kutafuta wahalifu huku Nchi ya Malawi ikiwa na Polisi wake , hata hivyo tunaishukuru serikali ya Malawi kwa kuwanusuru na vifo baada ya kuingilia kati kuwaokoa .

View attachment 1941078
Wamalawi wangewaua kabisa. Majambazi tu hayo. Wanaweza kuleta vita baina ya Tanzania na Malawi sababu ya tamaa zao za rushwa ya magendo
 
Askari Polisi wanne wa Tanzania wanashikiliwa nchini Malawi baada ya kuvuka mpaka kwa lengo la kuwakamata wahalifu.

Askari hao walikuwa na gari aina ya Toyota Landcruise pickup ambalo limeharibiwa na wananchi. Kuharibiwa kwa gari hiyo kulitokea baada ya polisi hao kulitelekeza wakiwakimbia wananchi waliowazingira.

Polisi hao hivi sasa wanashikiliwa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo kijiji cha Ipenza.

malawi N.JPG
 
NIMEPITIA COMENTS ZOTE NAONA WENGI KAMA SIO WACHANGIAJI WOTE WANASEMA "WAPIGWE TU".

WENGI WANAONA HATA JANGA LILILOWAPATA NI DOGO WANGETAMANI WANGEPATA MADHARA MAKUBWA ZAIDI.

POLISI WAJITAFAKARI
NI KWANN RAIA WENGI HAWAWAPENDI?
 
Mbona taratibu za kukamata muharifu nchi za wengine ziko wazi, ilikuaje wakavuka border? Na umeona hapo wamalawi hua wanakua treated vibaya kwenye selo za Tanzanaia hivo wamelipa kisasi ndio tujifunze kuishi kwa sheria na kutonyanyasa wageni sio vizuri
 
Inamaana hapo kuna tuhuma pia za wamalawi kunyanyaswa wakiwa upande wetu kitu ambacho sii kizuri
 
Polisi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya wametandikwa na Raia wa Malawi baada ya kuingia nchi hiyo ya kigeni kwa lengo la kuwasaka wafanya magendo .

Bado Haijafahamika walikopata utaratibu huo wa kuingia nchi ya watu kutafuta wahalifu huku Nchi ya Malawi ikiwa na Polisi wake , hata hivyo tunaishukuru serikali ya Malawi kwa kuwanusuru na vifo baada ya kuingilia kati kuwaokoa .
Siku zote tunasema IGP Sirro na genge lake lote wanaojiita Polisi uwezo wao wa kufanya kazi professionally na kwa kutumia akili ni mdogo sana, lakini watu wanabisha. Haya ndio matokeo. Hebu angalia maelezo ya hili tukio hapa chini, na ieleweke ni kina nani walifanya upumbavu wa namna hii. Angalia hata kuandika tu ni tatizo, hakuna hata vituo.

TAARIFA YA TUKIO LA ASKARI POLISI WETU 7 KUINGIA NCHINI MALAWI.

MNAMO TAREHE 15/09/2021 MAJIRA KATI YA SAA 16:30 - 17:30HRS HUKO MANEO YA KITONGOJI CHA MTIMA, KIJIJI CHA IKUMBILO, KATA YA CHITETE, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE NA MKOA WA SONGWE ASKARI G.3695 D/SGT RAMADHANI,H.694 PC EDWARD, H.8096 PC SAFARI, WP.12285 PC ANASTAZIA, H.9727 PC JOSEPH, H.9781 PC HUSSEIN NA H.8764 PC JUMANNE WAKIWA NA GARI PT.3676 TOYOTA L/CRUISER MALI YA JESHI LA POLISI TANZANIA WAKITOKEA VWAWA KUPELEKA WATUHUMIWA WA KESI YA MAUAJI PI.3/2020, WALIPOFIKA MAENEO YA MTIMA NA KUONA PIKIPIKI INAYOSADIKIWA KUWA IMEBEBA MAGENDO KUTOKA NCHI JIRANI YA MALAWI, WALIISIMAMISHA LAKINI PIKIPIKI HIYO ILIAMUA KUKIMBIA KUELEKEA NCHI JIRANI YA MALAWI, ASKARI. WALIAMUA KUIFUKUZIA NA KUVUKA MPAKA WA TANZANIA NA KUINGIA NCHINI MALAWI NA NDIPO WANANCHI WA MALAWI WALIIZINGIRA GARI HILO IKIWA NA ASKARI NCO G3695 DSGT RAMADHAN, H.8096 PC SAFARI, H9727 PC JOSEPH, H.694 D/C EDWARD, H.9781 PC HUSSEIN, WP.12285 PC ANASTAZIA NA H.8764 PC JUMANNE WAKIWA NA SILAHA MBILI AINA YA AK 47 NA KUANZA KUWASHAMBULIA.KWA.MAWE NA BAADAYE KUPATA MSAADA WA KUOKOLEWA NA ASKARI POLISI WA MALAWI(+) KATIKA VULUGU HIZO ASKARI MMOJA H8764 PC PC JUMANNE AMBAYE NI DEREVA ALIJERUHIWA KWA KUKATWA NA PANGA KICHWANI HALI YAKE SIO MBAYA ANAENDELEA VIZURI PIA GARI INASEMEKANA LIMEHARIBIWA KWA KUPIGWA KWA MAWE NA SILAHA AK 47 ZOTE MBILI ZIPO SALAMA NA ZIMEHIFADHIWA KITUO CHA POLISI CHITIPA MALAWI. ASKARI NO. G.3695 D/SGT RAMADHANI AMBAYE ALIKUWA KIONGOZI WAO, H.8096 PC SAFARI NA H.9727 PC JOSEPH WALIFANIKIWA KUTOROKA KATIKA VULUGU HIZO NA KURUDI KITUONI SALAMA NA WAPO MAHABUSU KWA HATUA ZA KINIDHAMU. MAWASILIANO KATI YA UONGOZI WA WILAYA NA MKOA TANZANIA NA MALAWI YANAENDELEA KWA AJILI YA KUWAREJESHA NCHI ASKARI HAO PAMOJA NA GARI NA SILAHA.
 
Watu wengi wanatype kuuliza 'Hawakuuona mpaka?' wakidhani ni kama kwenye muvi kwamba mpaka utakua na watu wa custom, askari wengine, maafisa uhamiaji n.k.

Yes, sehemu ambayo mtu anataka kupita kihalali itakua hivyo.

Lakini hawa walikua wanafuatilia magendo unadhani wangepitia hapo? Logically it means walipita njia za panya na njia hizo zilivyo kujua kwamba upo sehemu nyingine ni kazi ya ziada. Kwani mnavyosikia kuna waTz wananunua sukari Malawi unafikiri wanapita wapi? Kwenye hilo eneo la ukaguzi?

Na kuna swala jingine hapa. Hii ishu haitakua treated kama askari wameingia Malawi bali itakua ni waTz wameingia Malawi. Na haitasemwa wananchi wa Ipenza wamerushia mawe gari la askari wa Tz no itakua ni waMalawi wamewashambulia waTz.

Kwahiyo mtu yuko bize kusema hao askari ni divisheni zero but actually hata yeye hana tofauti na hao askari na inamaanisha tu hata kiingereza hajui. WaTz tubadilike tusiione habari na kuipokea kwa kuangalia inafeed vipi ego zetu badala yake tuielewe habari na tusisome ili tujibu, tusome kuelewa.

Kama unashangaa hao askari kuingia Malawi huku hawana hata ramani nikikuambia kuna jenerali wa jeshi aliingia nchi nyingine, akiwa na ramani na akasimika bendera ya nchi yake eneo jingine huku akiwa na kikosi bila kujua kama yupo nchi nyingine utasemaje?
 
Back
Top Bottom