BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,119
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia Askari wa Usalama Barabarani kutoka Mkoani Arusha SGT Ismael Katenya (48) anayeonekana pichani, kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi mabunda 340 yenye uzito wa kilo 140 iliyokua ameiweka ndani ya mabegi.
Taarifa ya Polisi Manyara jioni ya leo imesema Askari huyo amekamatwa na Askari waliokuwa doria katika kijiji cha Silaloda Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara akitumia gari lake aina ya Nissan Patrol (T148 CTB) kusafirisha dawa hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP George Katabazi amethibitisha kukamatwa kwa Askari huyo pamoja na gari lake kama inavyoonekana pichani na kueleza kuwa kwa sasa anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini Wahusika wengine wa mtandao huo wa biashara haramu huku taratibu nyingine za kisheria zikifuata.