Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi

Kwa hiyo polisi wamekuwa madaktati? Ni CCM so whatever happens. Tutagurahi9...good riddance
Mkuu wewe una uhakika hao polisi kablay ya kutoa hiyo taarifa hawakuhusika madaktari?
Ulisoma ukaelewa kilichoandikwa kwamba.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam likishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na taasisi mbalimbali limebaini kwambandani ya mwili wa Mzee Mangula kulikuwa na sumu.Uchunguzi kuhusu namna sumu hiyo ilivyoingia mwili mwake bado unaendelea kufanyika. "

Je waliposema na taasisi mbalimbali zimehusishwa wewe bado tu unaona hapo madaktari wakuhusika?Je unajua kama kuna polisi ambao ni madaktari?Ok,kama hakuna polis ambao ni madaktari najeshini je?Elewa wanaposema na taasisi mbalimbali zilishirikishwa.
 
Kiukweli mchawi wa CCM siyo Chadema wala chama chochote cha upinzani bali ni CCM yenyewe na ni lazima ijitafakari.

Kwa umri wa mzee na mwalimu wetu Phillip Mangulla hastahili kabisa kupitia madhila haya anayopitia. Ninamuomba Mungu wa mbinguni amfanyie wepesi aweze kupona haraka.

Yesu Kristo alisema "..../ikiwa wanayatenda haya katika mti mbichi je itakuwaje katika mti mkavu!"

Nawatakia Kwaresma yenye baraka!
 
johnthebaptist,
john, hizi ni drama hakuna cha sumu wala upuuzi wowote. Kuna mtu anataka kusingiziwa na most likely ni Niguse ninuke! Mbona ya mwakyembe haikutangazwa kama hii, Mbona ya Magudfuli ezni hizo akiwa ujenzi haikutangazwa hivi? Hii ni drama tu
 
johnthebaptist,
Hiyo ni drama kama drama nyingine za kitoto za ccm chini ya Magufuli. Unakumbuka lile igizo baada ya Lissu kupigwa risasi, eti mwanajeshi mstaafu naye akapigwa risasi kisha akalazwa Lugalo, halafu Magufuli akaenda kumtembelea akiwa ICU, cha ajabu akiwa huko huko ICU akawa anamueleza Magufuli jinsi alivyoshambuliwa! Kweli kuongozwa na watu wenye mawazo ya kizee ni shida sana.
 
Kwa hiyo polisi wamekuwa madaktati? Ni CCM so whatever happens. Tutagurahi9...good riddance
Kwa nini uwe 'negative' hivyo? Imesemwa kabisa alilazwa ICU Muhimbili ukafanywa uchunguzi akaonekana na sumu. Vipi unakimbilia kusema polisi wamekuwa madaktari?
 
"Ukizoea kula nyama za binadamu kamwe huwezi kuacha kuzila". RIP Mwalimu Nyerere. maadamu sasa ni nyie kwa nyie mtajuana.
 
Ushauri wa bure kwa wanachama wa CCM,kwa kuwa historia inaonyesha kuwa CCM siyo mahali salama,wanachama wa CCM wanatakiwa wawe na mavazi maalumu ya kuzuia sumu kama yale ya kuzuia sumu ya mabomu ya nuclear,wayavae wanapoitwa kwenye kitu kinachoitwa kamati ya maadili vinginevyo watakuwa wanapotea kama Kolimba.
 
Kwa hiyo polisi wamekuwa madaktati? Ni CCM so whatever happens. Tutagurahi9...good riddance
Acha upuuz police wanapokea ripoti ya daktari, kwani unavockia mtu kabakwa kwa kuwa ripoti ya daktari inathibitisha, ukisikia mtu kagongwa na ktu kzito ni daktari ndiye anayetoa report na kukabidh police.

Upumbavu si mzigo tu kwa mpumbavu bali kwa taifa Zima -The great B
 
hivi kamamda mambosasa ndie amekuwa msemaji wa hospitali ya Muhimbili na mtoaji report wa findings za wagonjwa ? huu mkanda CCM tiyari mmeshaunguza kabla haujatoka.

Lakini tujiulize hii michezo ccm mtakoma lini kutiliana sumu wenyewe tena kwa mtu mzee kama Mangula lakini mwisho wa siku mnawaangushia mzigo wapinzani wenu wa kisiasa.

Ina maana Jiwe bado hajatosheka na Membe kufukuzwa uanachama? CCM punguzeni uoga na mkae mkijua hivi vyeo vinapita msifikie kutoana roho.
 
Sio kila kitu polisi waseme. Hilo suala la kidaktari ilishindikana nini daktari akaongelea hilo tena huwenda angekuja na maelezo ya kitaalamu zaidi.

"Polisi wameelezea namna mkazi wa Buza alivyoshinda Jackpot"
Usalama wa Raia, yaani Police ndiyo wenye mamlaka na ndiyo kawaida wanatakiwa watoe taarifa kwa umma.

Daktari yeye anatoa technical report na kuwakabidhi wao, na kwa ethics zao madaktari, taarifa za mgonjwa wao huwa ni siri, na hivyo Daktari mhusika akitoa taarifa hiyo inakuwa ni makosa, anaweza akafukuzwa kazi na ama kushtakiwa au vyote viwili.

Muwe mnajifunza msiwe mnabwabwajabwabwaja tu humu kwenye mitandao kisa mnapenda kukosoa kosoa tu kila kitu. Toeni hoja ambazo zitakuwa zinawaainisha kuwa kweli nyie ni wasomi!
 
Mbona hajaeleza maendeleo ya mwenye sumu mwilini??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona wametangaza hadharani hivyo, ujue ameshapona, yuko safi sasa hivi. Ingekuwa kwa bahati mbaya labda angekuwa amepoteza maisha, taarifa za kuwekewa sumu zisingetangazwa, ingebaki siri ya madaktari na sytem ya Nchi.

Unaona sasa hawa watu ambao huwa hawatoi Press Release, vitu ambavyo huwa wanakaa navyo vifuani? Ukikoswa koswa kuwekewa sumu wewe kwenye bar unayopenda kwenda kupata kinywaji baridi kila siku jioni, halafu wao wakazuia pasipo wewe kujua, hawakuelezi, wanakaa nayo ka siri yao, na wewe mwenyewe unakuwa hujui na utaendelea kutkujua maisha yako yote kama waliwahi kukuepusha na janga zito kama hilo!
 
Back
Top Bottom