GE2025 Polepole: Luhaga Mpina hana sifa kikatiba na kikanuni kugombea Urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 Polepole: Luhaga Mpina hana sifa kikatiba na kikanuni kugombea Urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Imeandaliwa na Ndg. Humphrey H. Polepole, Mwana CCM wa Imani

1. Msingi wa Kikatiba na Kikanuni

Katiba ya ACT Wazalendo (2024), Ibara 16(4):
"Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo atakuwa ni mwanachama wa chama kwa kipindi kisichopungua siku thelathini (30) kabla ya uteuzi rasmi kufanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa."

Kanuni za Uchaguzi za ACT Wazalendo (2024), Kifungu 8(a):
"Mgombea wa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama ni lazima awe amejiunga na chama si chini ya siku saba (7) kabla ya tarehe ambayo mchakato wa uchaguzi umetangazwa kuanza."

2. Mtiririko wa Matukio Muhimu (Chronology)

15 Januari 2025 Katibu Mkuu Ado Shaibu alitangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.

8 Januari 2025 - Mwisho wa muda wa kujiunga ili kutimiza sharti la siku 7 kabla ya tangazo (Kanuni 8a).

18 Aprili 2025 - Tangazo la Katibu Mkuu: muda wa kuchukua na kurejesha fomu umeongezwa (lakini si masharti ya uanachama).

7 Julai 2025 Mwisho wa muda wa kujiunga ili kutimiza sharti la siku 30 kabla ya Mkutano Mkuu wa Taifa (Katiba 16(4)).

4 Agosti 2025 Luhaga Mpina alijiunga rasmi na ACT Wazalendo na kukabidhiwa fomu ya kugombea urais.

6 Agosti 2025 mgombea urais.


3. Uchambuzi wa Kisheria

Kwa mujibu wa Kanuni (8a):
Mgombea alipaswa awe amejiunga kabla ya 8 Januari 2025. Mpina alijiunga 4 Agosti 2025 maana yake amekosa sharti hili.
Kwa mujibu wa Katiba (16(4)):

Mgombea urais alipaswa awe mwanachama kabla ya 7 Julai 2025. Mpina alijiunga 4 Agosti 2025 maana yake amekosa sharti hili pia.
Tangazo la 18 Aprili 2025: Liliweka nyongeza ya muda wa kuchukua/kurejesha fomu, lakini halibadilishi masharti ya uanachama yaliyowekwa na Katiba na Kanuni.

4. Hitimisho
Kwa kuzingatia: Katiba ya ACT Wazalendo (Ibara 16(4)),
Kanuni za Uchaguzi (Kifungu 8(а)), па Mtiririko wa matukio,
Luhaga Mpina hana sifa kikatiba na kikanuni kugombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Masharti yote mawili (siku 7 kabla ya tangazo na siku 30 kabla ya uteuzi) ameyakosa.

Mwandishi wa uchambuzi huu ni Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye amejipa kazi maalumu ya kupambana na wahuni kokote kule waliko.

Ni maoni yake kwamba hatuwezi kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu bila kuibomoa na kuijenga CCM, bila ya kuwa na mchakato halali wa kumpata mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amepatikana kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Desturi nzuri za Chama Cha Mapinduzi (CCM), bila ya Chama Kikuu cha upinzani kuruhusiwa kufanya siasa na Mwenyekiti wake kuachiliwa mara moja bila masharti, bila ya kuwa na uelewa wa pamoja na muafaka wa kitaifa utakao lileta Taifa pamoja kabla ya Kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025.

1755584135632.png

1755584161430.png
 
' Kazi Maalum ya kupambana na wahuni popote pale Walipo'..!

Hivi hakuna mtu mwenye hoja zenye nguvu zaidi anayeweza kujibu hoja za Polepole kbs..? Iwe ndani ya chama chake au hata nje ya chama chake.

Ona sasa anawaumbua ACT... najua sio Bwana Zito ama Shaibu ama yule dogo mwenye michezo ya kujiteka 'Nondo' anayeweza kujibu hapa.!
 
Hauwezi kuwa mwanachama zaidi ya chama kimoja cha siasa kwa wakati mmoja. ??? Loophole hii itatumika na trust me, jamaa atagombea TU!!
 
Hauwezi kuwa mwanachama zaidi ya chama kimoja cha siasa kwa wakati mmoja. ??? Loophole hii itatumika na trust me, jamaa atagombea TU!!
Huyu Esther Matiko alikuwa mwanachama wa CCM toka July 2022 na huku akiwa bungeni kupitia Chadema. Na zaidi alikuwa mahakamani kutetea uanachama wake wa Chadema huku akiwa na kadi ya CCM kiunoni.
 

Attachments

  • Screenshot_20250710_131821.jpg
    Screenshot_20250710_131821.jpg
    281.4 KB · Views: 17
  • Screenshot_20250710_131807.jpg
    Screenshot_20250710_131807.jpg
    252.7 KB · Views: 18
Kuna muda CCM wahuni ni kupambana nao kihuni.

This time around ACT wako sawa tu.

Njia ya Polepole iko sawa ila haiingii kwenye sanduku la Kura.
 
Hauwezi kuwa mwanachama zaidi ya chama kimoja cha siasa kwa wakati mmoja. ??? Loophole hii itatumika na trust me, jamaa atagombea TU!!
ikiwa hivyo ,basi na LUHAGA MPINA ni mhuni kama wauni wengine.na ACT itakuwa ni chama cha wahuni.sasa unawezaje kumpa nchi mhuni ?
 
ikiwa hivyo ,basi na LUHAGA MPINA ni mhuni kama wauni wengine.na ACT itakuwa ni chama cha wahuni.sasa unawezaje kumpa nchi mhuni ?
Sina uhakika kisheria itakua imekaaje kama mwanasiasa ambaye ni mgombea anaweza kuwa mwanachama wa vyama viwili at the same time. Nilikua tu nawaza nje ya box, kwahiyo ni mawazo yangu binafsi
 
Huyu Esther Matiko alikuwa mwanachama wa CCM toka July 2022 na huku akiwa bungeni kupitia Chadema. Na zaidi alikuwa mahakamani kutetea uanachama wake wa Chadema huku akiwa na kadi ya CCM kiunoni.
ndiyo maana POLEPOLE anasema ndani ya CCM kuna wahuni.sasa unawezaje kuwa na kadi mbili za vyama viwili kama wewe siyo mhuni ili uweze kukikilagai chama kimojawapo.huwezi kuwatumikia mabwana wawili.

KATIBA MPYA INATAKIWA IWAONDOE WAHUNI WANAMNA HII
 
Back
Top Bottom