Pole Mzee John, tulikushauri upumzike ukagoma

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Mzee John Malecela - pole sana kwa ajali ya kisiasa iliyokukuta, in fact hii ni ya pili. Ya kwanza kali zaidi ni ile ambayo ukaenguliwa jina lako na maswahiba wako wa karibu chamani - sababu kuu wakikutaka wewe ubakie kuwa mshauri wa chama hiki tawala na si kungombea urais, wakapuuzia justification yako kwamba bado una nguvu na kazi ya urais si kubeba zege bali ni ni kutumia ubongo na ubongo wako bado upo fiti. ukajitosa mikoa yote kuomba wadhamini ulipomaliza kurudisha form maswahiba wako hawa hawa wakakukata jina.

Baada ya kukatwa jina hukuongea chochote na sisi wenye uelewa tukajua kabisa kuwa mzee wetu sasa umekubaliana nao uwe mshauri na mlezi ndani ya chama. Tukashuhudia tena ukionyesha uvumilivu wako kwenda front line kupigana kwenye chaguzi ndogo bila kinyongo, nakumbuka kule buzwagi na kwingineko kazi yako kweli ilionekana wazi wazi mpaka ukapewa jina la TINGATINGA.

Sasa cha ajabu ni hii issue ya juzi juzi, Mzee si uliambiwa upumzike lakini tunashangaa unakurupuka tena kwenda jimboni kwako mtera, sisi tukajua unaenda kuaga alaa kumbe unachukua form tena za uongozi - Tukasema mzee umekuwa kiongozi toka ukiwa na miaka 25 (takribani miaka 50 na zaidi ukiwa kiongozi) hutaki kupumzika tu? Upumzike uangalie vijana wako wakiongoza uwakosoe wakati bado upo arround.

Sasa mzee wangu yamekukuta, rufani yako imetupwa na hii ni doa sababu inakuondolea wewe qualification ya kuitwa mlezi ndani ya chama, kuna kitu gani ulitaka kukitekeleza huko mtera ambacho hujakifanya kwa miaka yote hiyo ya ubunge wako? au uongozi wa nchi?

Mzee John - na wazee wengine igeni mfano wa baba wa taifa, hakuna mtu kwenye haki miliki ya kuongoza hadi kifo.

Hapo sasa Mzee John, aibu yako au aibu yetu? Uliambiwa pumzika ukagoma sasa naona unapumzishwa kwa LAZIMA.
 
Bado lipo Jimbo la IKULU nafasi zisizozidi 10. JK atumie busara tu kumkumbuka Mzee wetu huyu ambaye bado ana nia ya kulitumikia Taifa letu akiwa Bungeni. Ni afadhali yeye kuliko Makamba, Kingunge,...
 
Bado lipo Jimbo la IKULU nafasi zisizozidi 10. JK atumie busara tu kumkumbuka Mzee wetu huyu ambaye bado ana nia ya kulitumikia Taifa letu akiwa Bungeni. Ni afadhali yeye kuliko Makamba, Kingunge,...

Mbunge wa KUTEULIWA!
 
Dingi aibu kaitafuta mwenyewe. Kutoka waziri mkuu mpaka kugaragazwa na kijukuu tena cha elimu ya msingi, loo aibu ilioje?
 
Bado lipo Jimbo la IKULU nafasi zisizozidi 10. JK atumie busara tu kumkumbuka Mzee wetu huyu ambaye bado ana nia ya kulitumikia Taifa letu akiwa Bungeni. Ni afadhali yeye kuliko Makamba, Kingunge,...

Apumzike tu, sidhani kama ana jipya ambalo aliliacha pending miaka yote hilo analotaka kulileta kwetu. JK mwenyewe anapumulia machine 2010.
 
WENYE UMRI KAMA WAKE SAA HIZI NDIO WANASOGEA KWA MUNGU NA KUANZA KUCHUKUA UZEE WA KANISA AU MISIKITI, SASA UMRI KAM HUO UENDE KUPAMBANA NA VIJANA KWENYE hAYO MAMBO YA KURA?
 
Bado lipo Jimbo la IKULU nafasi zisizozidi 10. JK atumie busara tu kumkumbuka Mzee wetu huyu ambaye bado ana nia ya kulitumikia Taifa letu akiwa Bungeni. Ni afadhali yeye kuliko Makamba, Kingunge,...

Aisee no mater uwe na akili na utendaji kiasi gani kazi ya kupewa na kazi uliyoapply naukafanyiwa usaili zina tofauti. Kazi ya kupewa inapunguza uadilifu na hata maadili sahihi ya utendaji.

JSM hawezi kuwa yule yule hata akipewa cheo gani?
 
Tuwapongeze Wagogo wa Mtera!
Mnamkumbuka yule jamaa wa suti nyekundu,Mh Stephen Kuwayawaya!!!Alishamfanyia hivi Mzee John!
 
With many trials and errors katika political life yake Mzee Malecela amejifunza kitu kimoja unique sana cha kukubali kujishusha na kusahau mapema yaliyopita. Ndio maana aliweza kumudu mikiki mikiki mbalimbali ndani ya siasa za nchi yetu hii. Times change. Amezeeka. Atulie sasa watu wawe wanamuita kwa ushauri sio kama tinga tinga tena. All in all, ana mchango wake mkubwa sana katika mambo mbalimbali ndani ya nchi yetu, kwahiyo bado anastahili heshima yake ingawa naona anasahau hilo.
 
Apumzike tu, sidhani kama ana jipya ambalo aliliacha pending miaka yote hilo analotaka kulileta kwetu. JK mwenyewe anapumulia machine 2010.[/QUOTE]
Afu shida ni kuwa mashine yenyewe geji ya presha haisomi uzuri,sijui hata kama itamvusha safari hii!Kuna haja ya kurudi kwa mababu,lolz!
 
Field Marshall we rudi tu janvini yaliyompata mzee ni ajali za kisiasa!!

Ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tehe tehe tehe ,atakuwepo tu ila uso una haya takuwa na jina jingine si ila ya sauti za umeme
 
:becky:
labda wata-introduce 'meza maalum' ili mzee aende na 'kiti' chake kama in case chama chake hakitachinjiwa baharini na wananchi waliochoka kuwa-overtaxed in all aspects of lyfe!
 
Tumuombee duwa jamani babu arudi atakufa na pressure akimwacha kimwana bungeni pekee!wajanja watampora bana!
 
Wakuu zangu ikiwa hamjui kitu ni bora sana mkae kimya kusikilizia..Mimi binafsi siamini kwamba mzee Malecela ametupwa nje ya hizo kura za maoni, isipokuwa umefanyika mchezo ili mwanaye kijana Lusinde kuingia ktk serikalini. Kumbukeni kwamba mzee Lusinde na Malecela ni ndugu hawa! hivyo yawezekana kabisa Mzee aliingia ili kuondoa Upinzani wa Lusinde kwa mtu mwignine isipokuwa yeye mwenyewe. Nikiwa na maana, kama mzee Malecela asingegombea basi nafasi yake ingevuta vijana wengi kugombea hivyo kuifanya nafasi ya Lusinde kuwa ngumu kupita..

Kwa nini nasema hivi, wanapopigana ndugu wawili ni rahisi watu kufikiria tu kwa mapana ya ndugu hao lakini kama mzee asingegombea watu wangezungumzia zaidi kama wameachiana madaraka. lakini maadam mzee mawazidi karata basi nyote mnafikiria kwamba kashindwa hali yawezekana kabisqa imepangwa kuwa hivyo na mzee nafasi yake ipo ktk viti maalum. Nasikia vimeongewzeka hadi 100... ama kweli nchi ya Wadanganyika hii..
Chama kimoja kuamua mfumo na ukubwa wa bunge hata baada ya bunge lenyewe kufungwa..
 
Back
Top Bottom