Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 115
- 258
Na Charles Heche
Waswahili wanasema siku za mwizi ni arobaini, bila kupepesa macho naona siku za Freeman Mbowe ndani ya Chadema zinahesabika kutokana na ubadhirifu ambao umefanywa bila huruma. Usijiulize kwanini nimemtaja Mwenyekiti wakati viongozi wako wengi, huyu kuna ushahidi mwingi na hajaanza mchezo huu leo.
Kwa mwenye swali basi hatakuwa na taarifa juu ya michango ya fedha zilizotolewa na Mzee Sabodo kwa Chadema, michango ya wabunge zaidi 30 kila mwezi kwa chama kwa miaka mitano, ruzuku ya serikali kwa Chadema. Kwa ujumla suala la mapato na matumizi limehodhiwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa muda mrefu sasa.
Hivi majuzi sote tunakumbuka harambee iliyoendeshwa na chama iliyojulikana kwa jina la "Join the chain", napenda kuwajulisha sasa ni rasmi kuwa michango iliyokusanywa imetafunwa na hivi sasa chama kiko juu ya mawe kiasi cha kushindwa kugharamia hata mafuta ya helikopta kwa ajili ya mikutano iliyokwisha pangwa.
Aibu hii ni vyema akaibeba Mwenyekiti Mbowe na maswahiba wake ambao wanayo kawaida ya kula kuku kwa mrija. Zipo taarifa kuwa baadhi ya viongozi wetu wamediriki hata kufanya ziara zisizo na tija nje ya nchi licha ya ukata unaokikumba chama chetu. Hii ni zaidi ya dharau kwa wanachadema na wapenda mabadiliko nchi nzima.
Dharau kwa wanachadema, matumizi mabaya ya fedha za chama matokeo yake ni aibu hii tunayoiona hivi sasa ambapo kuna mikutano haifanyiki kwa kigezo cha kukosekana kwa bajeti. Freeman Mbowe ifike wakati uone haja ya KUJIUZULU ili kulinda heshima yako, huu wizi wako tumeuchoka na ipo siku utaamsha vidonda vilivyopona, au unadhani tumemsahau Chacha Wangwe na hoja zake?