PLEASE RESCUE ME.. najisikia kukata tamaa

PLEASE RESCUE ME.. najisikia kukata tamaa

gambagumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
2,341
Reaction score
3,166
Wandugu tafadhalini naombeni ushauri nifanye nini mimi kijana wenu..nilimaliza chuo kikuu mwaka 2008, nikabahatika kuajiriwa baada ya mwaka mmoja.baada ya ajira nlijiwekea malengo kadhaa lakini mpaka sasa sjatimiza hata moja. Mazingira ya kazi ni magumu sana nafanya kazi 12 hours kwa siku sita. Nimepoteza kabisa morale ya kazi na nataka kuacha kazi ila sijui ntaishi vipi ..mahusiano na mpenzi wangu yamevurugika nimekua mbali sana na familia. Nilikua sinywi pombe ila sasa nakunywa tena kila siku..
 
Pole Sana mkuu kama wewe ni mkristu (Roman Catholic) kuna kitu kinaitwa NOVENA huwa zinasaidia sana nakushauri uanze au kama ni mwislamu najua na wao wana njia na swala zao hasa ukiwa kwenye matatizo kama haya cha msingi wakati wa matatizo si muda wa kujiongezea matatizo mengi juu yake maana pombe unajiongezea mzigo zaidi.
 
Kama unakunywa bia kila siku jua kipato chako kimeongezeka.
Ukiacha kazi kabla hujapata elewa kuwa kuipata kazi mpya ni ngumu angalia huko Dom ma HR walijazana 2226 kwa nafasi 12 tu. We vumilia tu kama kuna tudeal hapo kazini endelea kupiga
 
usiache kazi kabla hujapata kazi,
punguza pombe-zitakuwa ndio zinazokumalizia hela yako na kushindwa kufika malengo.
kila kitu solution ni wewe mwenyewe,ukiamua kuacha hiki nakufanya kile unaweza
 
Hapo kwenye pombe sikushauri; kujifunza kunywa kama weye si mnywaji kwa minajili ya kuondoa mawazo ni kupotea zaidi; lakini pia nishangae kidogo; kama pesa haikutoshi hii ziada unayopeleka kwenye starehe ya pombe unaipata wapi; na ili ikutoshe unafikiri ni kiasi gani...................jifunze kujinyima siao uache kula lakini kuwa matumizi muhimu na ya lazima mambo mengine kama unywaji yaweke kando kwa sasa
 
asante kaka kwa ushauri wako mzuri ntaufanyia kazi
 
pole sana,kazi usiwache japo kua ngumu endelea kutafuta kazi wakati bado uko kwenye kazi,mahusiano na mpenzi wako yamevurugika unamanisha mmeachana au hamuelewani? sababu nini? pombe unayo kunywa hapendi unywe au sababu huna hela? kama sababu pombe ntamuelewa laa ikiwa sababu ni ugumu wamaisha sidhani kama nimwamnake sahihi kwako....
 
Hembu check ID name yako....then jivue gamba!!
 
@maskini jeuri...kipato ni cha kawaida ila kinachoniumiza zaidi ni nature ya kazi mazingira yake ni magumu sana.
 
Pombe tena wakati unaona malengo bado hujayatimiza
tatizo ulijiwekea malengo makubwa sana maana kwa sisi ambao tunamaliza chuo tunajiwekea malengo mengi sana ambayo kwa uhalisia kuyatekeleza kwa muda mfupi ni ngumu sana
Mkuu nenda taratibu na mpango yako wala usitake kupata kila kitu katika kipindi kifupi. Tumia kipato chako kufanya mambo yako ya muhimu na suala la kuacha kazi lifute kabisa

Huwezi kupata mafanikio ya haraka kw akufanya kazi miaka mitatu tuu na unataka kila kitu kiende kama unavyotaka
Jipangia malengo kutokana na kipato chako na timiza malengo hayo tena yakiwa madogo sio makubwa ambayo hayaendani na kipato chako
 
Pole Sana mkuu kama wewe ni mkristu (Roman Catholic) kuna kitu kinaitwa NOVENA huwa zinasaidia sana nakushauri uanze au kama ni mwislamu najua na wao wana njia na swala zao hasa ukiwa kwenye matatizo kama haya cha msingi wakati wa matatizo si muda wa kujiongezea matatizo mengi juu yake maana pombe unajiongezea mzigo zaidi.

Mtakatifu wa siku za mwisho aise nakutafuta kama shilingi ya mkoloni
 
arabia falcon..kuna siku nlikua na stress tukafight ikafikia stage nikamwambia tusijuane..tangu siku hiyo amepunguza sana imani kwangu..
 
asante sana mkuu rocky ntajitahidi kuacha pombe..nalazimika kunywa ili kupunguza stress..lengo langu saa hivi ni kuwa mjasiriamali kama ningepata capital
 
asante sana mkuu rocky ntajitahidi kuacha pombe..nalazimika kunywa ili kupunguza stress..lengo langu saa hivi ni kuwa mjasiriamali kama ningepata capital
Pole sana ila kunywa pombe kwa kupunguza msongo wa mawazo sio njia sahihi,....weka malengo ya kupata mtaji kama unaweza biashara na mtaji utapata,....kunywa pombe kwa ajili ya leisure sio kupunguza stress mkuu
 
asante sana mkuu rocky ntajitahidi kuacha pombe..nalazimika kunywa ili kupunguza stress..lengo langu saa hivi ni kuwa mjasiriamali kama ningepata capital

Mkuu stress zitapungua baada ya kunyw apombe na pombe zikiisha kichwani bado mambo yako pale pale tena worse zaidi maana hata kile kidogo ulichokuwa nacho umekinywea pombe
jipange tuu maishani mwako mkuu kwa kile kidogo ukipatancho
 
gambagumu, pole sana kwa msongo wa mawazo. ili nikuelewe uzuri:
1 unasema unafanya kazi 12 hrs, muda na nguvu za kunywa pombe kila siku unaupata wapi?
2 kipato unasema hakitoshi, inakuwaje bajeti ya pombe haikosekani?

ukishajijibu maswali hayo, pitia hapa kwa moskwito
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/185126-mafanikio-kimaisha-3.html#post2693062

Ushauri wangu sasa ni huu:
1 Badilisha mtazamo wako kuhusu maisha, kuwa positive na mshukuru Mungu kwa yale aliyokujaalia (kuna thread humu watu wana masters na wako jobless kwa miaka, kuna wagonjwa, kuna wenye family crisis)

2 fanya kitu cha kukusaidia kubadili maisha yako ya baadae, mfano badala ya kunywa pombe ungewekeza kwenye masomo ya jioni. hii itakusaidia kubadili nafasi yako kazini kama sio kupata kazi yenye kipato zaidi

3 usijichukulie serious sana. kuna maisha zaidi ya maghorofa na magari (mfano tu). adjust malengo yako kulingana na hali halisi na ufurahie baraka za Mungu kwako

4 Shughulikia mahusiano yako na familia na mwenza wako. Haya mengine yanapita tu, angalia wanacholalamikia na uone kama ni muhimu kwako, na pia kama ni muhimu kuliko uhusiano wako na wao

kila la kheri

Wandugu tafadhalini naombeni ushauri nifanye nini mimi kijana wenu..nilimaliza chuo kikuu mwaka 2008, nikabahatika kuajiriwa baada ya mwaka mmoja.baada ya ajira nlijiwekea malengo kadhaa lakini mpaka sasa sjatimiza hata moja. Mazingira ya kazi ni magumu sana nafanya kazi 12 hours kwa siku sita. Nimepoteza kabisa morale ya kazi na nataka kuacha kazi ila sijui ntaishi vipi ..mahusiano na mpenzi wangu yamevurugika nimekua mbali sana na familia. Nilikua sinywi pombe ila sasa nakunywa tena kila siku..
 
asante sana mkuu rocky ntajitahidi kuacha pombe..nalazimika kunywa ili kupunguza stress..lengo langu saa hivi ni kuwa mjasiriamali kama ningepata capital

jitahidi kupata muda wa mapumziko , achana na pombe maana wengi huamini zinaliwaza, fanya mazoezi au matembezi ya alfajiri au jioni.. achana na makundi yasiyofaa
 
asanteni sana BMP, IGWE AND KINGASTI ushauri wenu unanifanya nijiskie mpya tena..nawahaidi kwamba nitazingatia ushauri wenu.
 
Back
Top Bottom