Wandugu tafadhalini naombeni ushauri nifanye nini mimi kijana wenu..nilimaliza chuo kikuu mwaka 2008, nikabahatika kuajiriwa baada ya mwaka mmoja.baada ya ajira nlijiwekea malengo kadhaa lakini mpaka sasa sjatimiza hata moja. Mazingira ya kazi ni magumu sana nafanya kazi 12 hours kwa siku sita. Nimepoteza kabisa morale ya kazi na nataka kuacha kazi ila sijui ntaishi vipi ..mahusiano na mpenzi wangu yamevurugika nimekua mbali sana na familia. Nilikua sinywi pombe ila sasa nakunywa tena kila siku..
dawa ya matatizo ni suluhu na sio matatizo ju ya matatizo.
mpaka sasa umengeza tatizo moja la kunywa pombe kwa kua unasema ulikua hunywi.
jiulize, hivi kama sasa hivi pamoja na kua na hyo kazi maisha yako yapo hivyo yalivyo, je usigekua na japo hyo kazi??
ushauri wangu ni kua kabla ya kufanya maamuzi linganisha kwanza pande mbili (faida na hasara za maamuzi) za matokeo ya maamuz hayo.
ni changamot chanya kama kijana kufikiri namna unavyoweza uboresha maisha yako mbali na ajira.
me hua nawaza kila siku na kumwomba mungu anijalie siku moja niishi kwa kujitegemea na hata niajiri vijana wezangu,
lakini kabla ya kufikia kaucha kazi unaytakiwa ujue kwanza aunaacha kazi na nakwenda wapi kufanya nini?
je, kitakua na faida (kiuchumi, kijamii na materally and non materially) zaidi ya hapo ulipo sasa?
nakushauri utulie kwanza bro/sista then ufikirie vizuri.