Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
 
Pole ndugu,,, mungu ana makusudi yake jaribu kutambua funzo analokupa leo ili rizki yako ikirudi uwe imara has a katika kuwekeza nguvu zako kwa Mungu.

Nimeona mlikuwa n ujenzi wa nyumba je kwanini msiiuze uanze biashara? Au ukopee mkopo hiyo nyumba?
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia akiba yangu yote. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu kwenye mfupa.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu ba msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta"

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Elimu yako?
 
Pole sana mkuu, makampuni mengi hayafanyi vizuri sokoni na watu wengi wanapunguzwa mimi nikupe moyo, wewe bado ni kijana na una nguvu ma safari ndefu ya kwenda, kwa vyovyote kama kuna uwezekano wa kuuza hilo gari na isikuathiri sana uza, fanya mambo mengine, au kama una aina ya gari ambayo hauwezi kufanyia biashara ya uber, fanya mchakato ubadilishane na ambayo utaweza kufanyia biashara hiyo hata kama ni kwa hasara ila itaku boost, kisha ufanye mchakatk uhame hapo kwa rafiki yako, kabla naye hujampoteza
 
Pole Sana mkuu,

Hakuna gumu lisilo na njia ya kutoka. Haijalishi ni magumu mangapi unapitia usiruhusu kichwa kivurugwe. Boresha kichwa chako. Pokea na jua umeanguka Kuna nafasi nyingine ya kuamka. Kaa chini na mwenzio muongee kuhusu nafasi Yake kwasasa kipindi hiki uko chini.

Nimewahi kupitia hali Kama yako kiukweli wanawake wana roho ya ajabu sana ( sio wote) ila hata wangu alikuwa ananiBully sana.

Naamini watakuja watu wengine wenye msaada tangible zaidi ya huu.

Stay on lane brother
 
Pole.
Tunapowekeza mahali pamoja pakaticki tusijisahau kuwekeza na pengine tofauti tofauti.maana kimoja kinaweza anguka,kingine kikabaki na kukushika

Mkeo ni mjinga na hana busara,million sita ni pesa nyingi sana kuwekeza ya kaenda katafuta mteremko QNet kaliwa ni mjinga!.kapata kazi bado anakuumiza ilhali anajua kazi huna na unaumwa hana busara!
Kwanini usiuze vitu ulivyonayo baadhi vyenye thamani vikusongeshe kuliko vikikaa tu vinachakaa ukweni?
Ulisema mna nyumba mnamalizia kujenga kwanini usiuze angalau utapata hata million 20-40 uanze upya?
Ama uza hili gari kisha hamia nyumba mnayojenga ikiwa hata pagala juu bati madirisha ya nyavu muanze maisha huku unaendelea kutafuta kazi?

Ni ushauri tu maana huwezi jua Hiki kilio kitachukua mda gani..so ujiongsze kwanza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom