Pinda: Wanaopinga kodi ya simu hawana jema

Pinda: Wanaopinga kodi ya simu hawana jema

Huyu mtoto wa mkulima sasa hivi naona amekuwa mtoto wa fisadi. Juzijuzi wametangaza kuanza kupeleka umeme nje ya nchi na reli kupeleka nchini kongo drc ila umeme wa kwenda vijijini inabid tuuchangie 1000. Halaf hajatueleza marundo ya kodi tunayolipa yanakwenda wapi

uwezo huo wa kuchakata mawazo unao wewe tu si wale waliohutubiwa
 
>wabunge wa CCM- NDIOOOOOOOOOOOOO
>Naibu waziri wa mawasiliano (Makamba)- SIOOOOOOOOOOOOOOOOOO
>Waziri wa Fedha (Mgimwa)- NDIOOOOOOOOOOOO
>Chama cha Mapinduzi kupitia kwa katibu mwenezi (Nape)- SIOOOOOOOOOOOOOOOO
>Waziri Mkuu (Pinda)- NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Duh mnatuchanganya sasa,hamjajipanga hata kichama na kiserikali.

wizara na wizara zinapingana,
Chama kinachotawala na waziri mkuu wanatofautiana,

SASA SISI TUWAELEWAJE NYIE ******
 
Huyo ndio mzee wa KUPIGA TU!!!

  1. Hivi Pinda anataka kumdanganya nani? Zile tambo na majigambo ya ziara ya Obama pale kwenye mitambo ya Symbion Ubungo wakiwa na Kiwete wake zimeishia wapi?
  2. Tuliambiwa Obama analeta 7 Billion USD za ku-Power Afrika na TZ ikiwemo! Sasa huu umeme wa Pinda wa kuchangia elfu elfu ni upi tena????
  3. Mizengo Pinda tumeshaambiwa Watanzania kuwa ni PM Dhaifu siku zote anaweza kusema chochote mahali popote na wakati wowote bila kufikiria maneno yake na athari yake.
  4. Pinda asitake kuleta siasa hapa. Nani alimwambia kuwa shs. 1000/- kwa kila mtumiaji wa simu inaweza kupeleka umeme vijijini?

Hapo ndipo uwezo wa Pinda kufikiri unapogota!

Hilo suala la umeme ni siasa tu...kwani tozo nyingine za kodi zapelekwa wapi hadi hiyo iwe ya umeme(project specific tax)! Nasema msipolipa hiyo kodi mtapigwa tu na naagiza polisi wawapige maana tumechoshwa na mapingamizi hayo..! Serikali bila kodi haiendesheki na rais hatoweza kusafiri..! Tumechoshwa bora wapingaji wakapigwa na mtwara tulishaonyesha kwa kuwapiga kama ilivokua arusha, iringa na sehemu nyingine!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Pinda aache unafiki, Mhe. Zitto katoa mbadala wa hiyo hela ambayo Pinda anasema wanataka itumike kupeleka umeme vijijini. Zitto amewaambia hela wanayolipwa wabunge kama sitting allowance ni mara nne ya hela ambayo itakusanywa kupitia kodi ya laini. Kwanini wasisitishe sitting allowance kwa wabunge ili hiyo hela waipeleke kwenye mradi wa kusambaza umeme vijijini? Kama Pinda kwa hakika anafanya haya kwa nia ya kuwasaidia watanzania basi apeleke pendekezo la kufuta allowance kwa wabunge ili hiyo hela itumike kupeleka umeme vijijini.
 
Last edited by a moderator:
CCM kina msemaji wake (NAPE) na Serikali ina msemaji wake pia, ingawa wanatuchanganya sana na hatujui ni nani hasa.

Ni jambo la kushangaza sana January kulalamika kwenye vyombo vya habari. Unafiki tu
January alikuwa anajibizana na mnyika wala hayatuhusu sisi na hakuwa anaongea kwa niaba ya chama wala serikali.
 
Wajamen, Wachumi wetu, Kwani hakuna Vyanjo vingine vya Mapato ??
Maana Mheshimiwa Mtoto wa Mkulima anasema Pesa zinaenda kusambaza Umeme Vijijini.
Au kuna Agenda nyuma ya Pazia, Maana Uchaguzi upo karibu na Mwisho wa Madaraka/Uongozi 2015 kwa wengine.

Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.

Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.

Aliongeza '' Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema Pinda.

source: Habari leo
 
The holy book says- They see but they see not,hearing they hear not, neither do they understand. Hii ndio serikali sikivi.
 
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.

Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.

Aliongeza '' Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema Pinda.

source: Habari leo

hi pesa tunayolipa kwa kununua mafuta ni kweli inaenda kutegeneza mabarabara? manake kila siku nasikia ni mikopo tu yakutegeneza hayo mababara.
tofauti na kipindi cha mhe Mkapa tulikuwa tunajua kabisa barabara kutoka Singida kwenda Dodoma inajengwa kwa fedha zetu za ndani
kwa JMk sifahamu barabara yeyote inayo jengwa kwa kodi zetu au ushuru wa mafuta labda mwenye kuelewa zaidi anifahamishe wa ndugu
 
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.

Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.

Aliongeza '' Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema Pinda.

source: Habari leo

hawa watu si wazalendo wala hawana nia ya kupeleka huo umeme vijijin ni siasa tuu hizo kwasababu wana mpango wa kuuza umeme nche ya nchi ifikapo 2014 . kumbe wanaweza kuupeleka nje lakin kupeleka vijijin ni tatizo.
 
The holy Koran says- Dumb,deaf and blind they will not return to the true path. Hii ndio serikali yetu sikivu.
 
Ngoja niishie kupita tu..kwa maana nikianza kucomment hasira niliyo nayo juu ya mzee wa kupinda.....nitakula ban!
 
Tulipe hii kodi tutengeneze umeme vijijini wenzatu pia wanataka maendeleo kama sisi.

Kwenye harusi watu wanachangia hadi shilingi 50,000 sioni kwanini hii kodi mnaipinga.
 
pesa za madini yote zinakwenda wapi?.Uganda wamekundua mafuta wameweka mikakati yao inayoitwa uganda vision 2030.yaani barabara,mashule ,mahospitali na miundombinu mingine itafanikiwa kutokana na faida ya hii rasilimali ya mafuta.Sasa narudi kwetu sisi ni wapi pesa za madini ya hii nchi zinakwenda?gesi,uraniunium [Namtumbo],n.k
 
Hii kitu wakiendelea kuikomalia yaweza kuwa kaburi lao zuri sana 2015, hiyo kitu ina athari ya moja kwa moja hadi kwa kwa wale wazee kule vijijini ambao ni mtaji wao mkubwa.

Mie naomba waikomalie hadi 2015 watu wapate daraja la Rufiji kama sio la Kigamboni
 
yani waziri mkuu sijui amekutwa na mdudu gani kila anachoongea safari hii ni kinyume na matakwa ya watanzania.
 
pinda hivi alishapona alikuwa amepata ajali
 
Back
Top Bottom