Pinda: Wanaopinga kodi ya simu hawana jema

Pinda: Wanaopinga kodi ya simu hawana jema

Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.

Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.

Aliongeza '' Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema Pinda.

source: Habari leo

Mimi na Pinda kifedha tunaweza kuwa sawa tu hivyo hii kodi haituumizi, tatizo ni wale watu wa chini ambao hiyo tozo ya elfu moja inaweza ikafanana kabisa na pesa anayotumia kununua vocha kwa mwezi, amesahau kwamba kuna watu wamenunua simu ili imsaidie kubeep tu akiwa na shida. Mimi kuna mtu namfaham amepanga chumba analipa Tshs3000 kwa mwezi pale ngudu nadhani unapata picha hii tozo ya elfu1 kwa mwezi ni mzigo kiasi gani kwake, na ana simu kila wakati ipo hewani kazi yake kubwa ni vibarua vya mashambani ile simu ipo ili apigiwe tu.
 
------- kweli,ina maana serikali ndio mwisho wake wa kufikiria huo,kuwa charge wananchi wake kodi zisizokuwa na kichwa wala miguu??eti wanataka wapelekewe umeme,kilaza kweli...

Tunajitaji mabadiliko kwenye hii nchi na viongozi wanaojitambua na sio kama hawa -------....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hapa sasa ile kauli ya Mh Sugu dhidi ya huyu waziri mkuu inaendelea kupata uhalali,na kuwa hatimiliki yake.

Kabisa ni ------- mheshimiwa Sugu hakukosea,umeona reason aliyosema??eti kijijini wapelekewe umeme...Nini faida ya serikali sasa??

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hapo ndo siwaelewi CCM kabisaaaa... hebu cheki
1. Makamba anadai alizidiwa nguvu mpaka tozo ya line ya simu ikaingia bungeni...
2. Wabunge wa CCM wasema NDIYOOOOOOO ipite, na ikapita....
3. Ilipoanza kulalamikiwa, NAPE akaema CCM inapinga uwepo wa tozo hiyo......
4. Makamba akarudi kwa Mnyika na mkumwambia aache unafiki wa mitandanoni.... na akaonyesha kama vile tozo hii itasitishwa...
5. Pinda naye anakuja na maneno yanayoonyesha kuwa tozo hiyo ipo na itatozwa kama kawaida

MASWALI...
1. Hivi, kwa nini Pinda, Makamba na Nape hawana kauli moja juu ya hili...??
2. Aliyemfanya Makamba ashindwe wakati anapinga tozo hii hadi ikaingia bungeni... NI PINDA..???
3. Hawana vikao vya kiserikali ili kutoa kauli moja..???
4. Nani msemaji wa jambo hili..??? Kwamba akitoa taarifa yeye ndo tuiamini..??

ndani ya ccm kila mtu ni kambale,
 
Kabisa ni ------- mheshimiwa Sugu hakukosea,umeona reason aliyosema??eti kijijini wapelekewe umeme...Nini faida ya serikali sasa??

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Shenzy kabisa huyo,watu wa vijijin hata chakula hawajui watapata wapi wanatoza kodi ya simucard ili wawape umeme wapi na wapi??
Nani kawaambia wao wanashida hiyo,na kama wanaona wana shida hiyo kwanin wasiwapelekee kwa gharama ya kodi zingine?lazima wawalimbikizie kodi zingine ili wawape umeme??kwan ndio makubaliano na hao walalahoi??upuuzi kabisa hawa viongoz wasio na mbele wala nyuma
 
Wenye taarifa nzuri naomba watusaidie:

(i) Najua kuna Wakala wa umeme vijijini ambao umeanzishwa nafikiri kwa sheria ya bunge. Je Wakala huu hauna njia ya mapato zaifi ya kuanxishiwa nje ya utaratibu mapato haya? Je hizi pesa zitakwenda moja kwa moja kwenye Wakala hawa au xitaingizwa kwenye mfuko mkubwa wa Serkali?
(ii) Kwa mawasilano ya simu tayari tunachangia mradi wa mawasiliano vijijini ambao kwa uelewa wangu huko chini ya TCRA na Wizara husika. Kwa nini sekita hii iongezewe gharama kuchangia kitu kidichohusiana kabisa nacho? Kwa nini wasiweke mchango kwenye umeme kughara ia hili?
 
Pinda fanyeni yafuatayo:Komesheni UFISADI Serikalini na kwenye Halmashauri,Punguzeni matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya anasa Serikalini kama vile kununua magari ya bei kali,Fanyeni utaratibu wa kuwatibia viongozi wa serikali na wanasiasa katika hospitali za hapa hapa Nchini,Punguzeni Ziara za mara kwa mara za Viongozi wetu nje ya Nchi,Achaneni na Semina Zisizokuwa na tija kwa Taifa,Punguzeni ukubwa serikali hasa Baraza la Mawaziri,Achaneni na mpango wenu wa kuongeza Wilaya mpya,Mikoa mipya na Majimbo mapya ya Uchaguzi kila kukicha pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa baadhi ya POSHO wanazolipwa baadhi ya watumishi wa umma.Na mwisho kusanyeni kodi bila kuwaonea haya wafanyabiashara wakubwa husasani hawa wafanyabiashara wanaomiliki makumpuni ya simu,mahoteli na wale walioko katika sekta ya madini.Serikali wakifanya haya hatutaona tena usumbufu wakubambikiana kodi hizi zisizokuwa na kichwa na wala mguu kwasababu serikali itakuwa na fedha za kutosha kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi.
 
zile nyumba za tembe DOdoma mtawekaje umeme? si mlisema mnaanza kuuza umeme nje ya nchi sasa iweje muwe na uwezo wa kusambaza umeme nje then kwa wananchi mle vibuku buku, wataweza kununua nguzo, nyaya, na vitu vinavyotumia umeme, kama rice cooker, pasi,
 
"Wapigwe wanaopinga kodi wapigwe tu maana hatuna namna nyingine tumechoka sasa"
 
Hapo ndo siwaelewi CCM kabisaaaa... hebu cheki
1. Makamba anadai alizidiwa nguvu mpaka tozo ya line ya simu ikaingia bungeni...
2. Wabunge wa CCM wasema NDIYOOOOOOO ipite, na ikapita....
3. Ilipoanza kulalamikiwa, NAPE akaema CCM inapinga uwepo wa tozo hiyo......
4. Makamba akarudi kwa Mnyika na mkumwambia aache unafiki wa mitandanoni.... na akaonyesha kama vile tozo hii itasitishwa...
5. Pinda naye anakuja na maneno yanayoonyesha kuwa tozo hiyo ipo na itatozwa kama kawaida

MASWALI...
1. Hivi, kwa nini Pinda, Makamba na Nape hawana kauli moja juu ya hili...??
2. Aliyemfanya Makamba ashindwe wakati anapinga tozo hii hadi ikaingia bungeni... NI PINDA..???
3. Hawana vikao vya kiserikali ili kutoa kauli moja..???
4. Nani msemaji wa jambo hili..??? Kwamba akitoa taarifa yeye ndo tuiamini..??

Tusubiri Msimamo wa mwisho wa CCM kutoka kwa Mwigulu .............. wengine wanapiga kelele tu!!
 
Tusubiri Msimamo wa mwisho wa CCM kutoka kwa Mwigulu .............. wengine wanapiga kelele tu!!
Mwigulu huyu huyu wa ushahidi wa mbinguni na duniani au mwingine...?? Yaani huyu ndo PINDA kabisa
 
Wahenga walisema masikini akipata ------ hulia mbwata!
 
Uongozi huu umepata FISTULA mbaya sana kwani kila inachofanya matokeo yake huwezi jua au kupanbanua kama ni mkojo au choo
 
Ni jambo la kushangaza sana January kulalamika kwenye vyombo vya habari. Unafiki tu[/QUOTE]

Kama kweli Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnatafuta fedha kwa ajiri ya kuongeza mapato ya kuwa wezesha kusambaza umeme vijijini nashauri serikali iache ubaguzi wa kimatabaka kati kodi ya PAYE.... Wa heshimiwa wabunge wote na baraza lote la Mawaziri nao walipe PAYE kama tunavyo lipa sisi wafanyakazi hohe hahe. Pia walipe withholding tax ( asilimia 15%) kwa allowances zao. Mathalani wabunge wanapokea mshahara wa zaidi ya sh 11,000,000/=. Kila mbunge atachangia sh 3,189,700/= na tufanye bunge letu lina wabunge 345... serikali itakusanya sh 1,100,446,500/= au kwa urahisi ni bilioni 1.1. hiki ni chanzo kabla ya kuhusisha baraza la mawaziri
 
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.

Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.

Aliongeza '' Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema Pinda.

source: Habari leo
4467301_orig.png
 
Back
Top Bottom