Wakuu JF Amani iwe Nanyi.
Wakati Napitia Kwenye Uzi wa
VIKWAZO
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wahariri-hii-tabia-ni-sahihi.html#post6892227
Ndo nikakuta Malelezo ya PM Pinda kuwa Tozo la 1000% per month kwenye kila SIM Card ni kwa ajili ya Kupeleka Umeme Vijijini.
Hivi Jaman hii ni comment ya Kutolewa na Serikali Kweli ??? tena wakati Huu ambao kila Mtanzania mwenye kutumia simu ya Mkononi analalamikia Hii Tozo !
Hivi Obama amekuja Tanzania kufanya nini?
Si Serikali hii hii imesema kuwa Obama na Rais wa China wame ahidi kusaidia kufikisha umeme Vijijini!
Ina Maana kutoza watu 1000 kwa Mwezi kupitia SIM card zao ndo Mchango wa Tanzania Kwenye ku Boost Ahadi ya China na Obama?
Hivi jamani Serikali yetu inatufanya Mazuzu ama yenyewe ndo Serikali Impotent kwa Kushindwa Kusoma Saikolojia ya Wananchi wake!
Yaani ni Serikali hii hii iliyotaka kutunyang'anya Wa Fanyakazi Fao letu la Kujitoa, tuka React, leo hii tena Wamekuja na Kodi ya SIM Card?
Hii Kodi Technically ina Maana kuwa Gharama za Mawasiliano zimepandishwa?
Nini Maana ya Kupunguza Gharama za Mawasiliano (TCRA, kuanzia March this Year).?
Hata Miezi sita Haijafika, washakuja na Kodi ya SIM Card.
Ushauri wa Bure kwa Serikali
Kama kweli wangekuwa wana hitaji 1000 Kwa Mwezi kwa Kila Mmiliki wa SIM Card, si wangepandisha tu Gharama za Mawasiliano na Waka kata Chao Juu kwa Juu kutoka kwa Makampuni ya Simu.