Kwetu-Mbagala
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 203
- 39
Tatizo hasa ni matokeo ya kodi tunazolipa!..Tumeshalipa sana kodi na matokeo hatuoni! Na hata kdg kinachofanyika pesa yake inakua imekopwa! SASA pesa za kodi tunampeleka wapi?
Hapa sasa ile kauli ya Mh Sugu dhidi ya huyu waziri mkuu inaendelea kupata uhalali,na kuwa hatimiliki yake.
Mh, Tanzania tuna Wazir mkuu kwel.
Hapo ndo siwaelewi CCM kabisaaaa... hebu cheki
1. Makamba anadai alizidiwa nguvu mpaka tozo ya line ya simu ikaingia bungeni...
2. Wabunge wa CCM wasema NDIYOOOOOOO ipite, na ikapita....
3. Ilipoanza kulalamikiwa, NAPE akaema CCM inapinga uwepo wa tozo hiyo......
4. Makamba akarudi kwa Mnyika na mkumwambia aache unafiki wa mitandanoni.... na akaonyesha kama vile tozo hii itasitishwa...
5. Pinda naye anakuja na maneno yanayoonyesha kuwa tozo hiyo ipo na itatozwa kama kawaida
MASWALI...
1. Hivi, kwa nini Pinda, Makamba na Nape hawana kauli moja juu ya hili...?? Hawana jeuri ya kauli moja hawa, hicho unachotamani hakitekelezeki ndani ya CCM hii ya mwenyekiti Jakaya Kikwete anayemwamini Mwigulu kuwa ndio 'nyundo' na 'jembe' jipya litakaloinusuru CCM hata akawataka wanaCCM wafuate mfano wa Mwigulu....aibu (!)
2. Aliyemfanya Makamba ashindwe wakati anapinga tozo hii hadi ikaingia bungeni... NI PINDA..??? Makamba amekuwa mnafiki sana kiasi nadhani hata mwenyewe anajishangaa. Ulimsikia kauli yake baada ya agizo la Pinda la 'wapigwe tu' lilivyotekelezwa huko Bumbuli?
3. Hawana vikao vya kiserikali ili kutoa kauli moja..??? Hawana ubavu wa kauli moja hawa, bila shaka umemsikia Nchimbi akijinasibu ati nchi ipo ICU, sijui kwenye hospitali gani, za hapa nchini ama India (!)
4. Nani msemaji wa jambo hili..??? Kwamba akitoa taarifa yeye ndo tuiamini..?? CCM hii ya Jakaya Kikwete kila mmoja ni msemaji, hujaona kauli za Mwigulu zinakinzana na zile za Nnape?
Mh, Tanzania tuna Wazir mkuu kwel.
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.
Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.
Aliongeza '' Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema Pinda.
source: Habari leo
Huyu mtoto wa 'Mpagazi' ni mtu mmoja very useless person. Uwaziri wake Mkuu hauna maana wala msaada wowote kwa WaTanzania. Ni bora awe anafunga bakuli lake tu kuliko kumwaga upup*u kila mara. Ati naye huyu anajiita 'mtoto wa mkulima'....sssshhh arrgggg...mkulima my foot!
wananchi wanapokataa mpango fulani wa serikali,basi viongozi ni lazima wasugue vichwa kwelikweli
ni kweli watozwe tu serikali haina hela tumechoka kuomba sasa.waziri mkuu mizengo pinda amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.
Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani ruvuma.
Pinda '' ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petrol, ambayo imetupa fedha nyingi katika mfuko wa barabara, za kuunganisha miji na mikoa''.
Aliongeza '' nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema'' alisema pinda.
source: habari leo