Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Kila kwenye mchemko wa serikali hii utamkuta Mizengo Pinda.
 
Hiyo siyo amri ya Pinda bali ya JK kwa kuwa malori mengi ni ya Riziwani. Sasa magufuli kujiuzulu unasubili nini?!!!!
 
Tatizo siyo 5% tolerance, tatizo ni barabara hafifu zilojengwa chini ya viwango kwa ushirikiano haramu kati ya mafisadi na makandarasi.
 
Tutachukua mda mrefu sana kuendelea kama taifa maana watu wana protect personal interest kuliko maslahi ya taifa..alichofanya fanya pinda ni kulinda maslahi ya watu wachache kwa faida zao..Nadhani wangeshauriana kati ya pinda na magufuri then magufuri atoe tamko jipya kuhusu kauli yake,lakini waziri mkuu kuingilia utendaji wa waziri waliemuamini na kumpa dhamana ya kuongoza wizara,inaonesha mapungufu katika serikali ya ccm.
 
Mgomo wa wasafirishaji ni matokeo ya ubovu wa sera zinazo endesha nchi yetu.Mengi yamesemwa kuhusu kuweka wafanya biashara katika uongozi wa Serikali na Chama pia.Wafanyabiashara ya usafirishaji waliopo ndani ya serikali ndiyo waliosababisha kasheshe hii,kwanza wamefanikiwa kuikosesha serikali mbadala wa malori ambao ni Treni! Serikali inalijua hilo lakini kwa kuwa miongoni mwa-serikali kuna hao wamiliki wa malori hakuna kitakachofanyika kwa maslahi ya nchi.Hata hiyo kamati itakayo undwa na Mh.Pinda ndani yake kutakuwa na wadau wa makampuni hayo,Mh.Magufuli atajikuta peke yake ketetea nchi hii! Nijambo lisiloingia akilini Reli zetu kutopewa Msukumo wa kutosha,sababu utaambiwa pesa hakuna! Labda ndugu zangu wana-JAMVI nimalize kwa kuuliza swali moja tu,kungekuwa na umakini tungeanza lipi,Kujenga daraja la KIGAMBONI au kuimarisha/kufufua reli ya kati na Katika hiyo miradi miwili upi unagusa wananchi wengi?
 
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana amefuta agizo lililotolewa na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli la kuwataka wamiliki wa magari makubwa ya mizigo, kutozwa asilimia tano kwa kila gari litakalozidisha uzito na kuagiza kurudiwa kwa utaratibu wa zamani wa msamaha wa asilimia tano ya tozo hiyo.............. POMBE MAGUFULI pima mweneywe.........!!!!
 
Mwaka 2006 wakati serikali imeruhusu 5% walishirikiana na wadau ila wakati ya kuiondoa wadau wasishirikishwe ?Huyo ndiye Magufuli na washabiki wake akina Manyerere!
 
GT wa JF majanga tu, badala ya kudai kila mtu afuate sheria wao wanashabikia watu waruhusiwe kuvunja sheria. Kuna baadhi ya maeneo hata hiyo rami wahaijui, lakn maeneo mengine barabara zinafumuliwa kila baada ya miaka mitatu badala ya miaka 13 normal life span ya barabara ya rami. Kwa mtu aliyewahi kuendesha barabara ya chalinze Ruvu atakubaliana na magufuli kuzuia magari yasibebe mzigo kupita viwango vilivyopendekezwa..

Mkuu hakuna anayependa kuvunja sheria lakini kuna tatizo kwenye hizo mizani. Ukipima kibaha uzito utapata tofauti na Mikese wakati mzigo uko kwenye container ambalo liko sealed. Sasa hiyo 5% ilikuwa ina ondoa hili swala la variation toka mizani moja mpaka nyingine. Halafu swala la barabara sio kwamba magari yanaharibu tuangalie na wajenzi wanaojenga je wanajenga kwa kiwango.Nakumbuka barabara ya chalinze -segera ilijengwa na Kapico mwaka 1984-89 iliweza kudumu mpaka 2010 wakapewa wachina ambao waliondoa ile ya Kapico nakuweka yao ambapo ilikuwa hata kabla hawajamaliza walikuwa wanaweka viraka kwa ambae anakumbukumbu anaweza kuchangia zaidi, maana hii barabara sasa sio kama ilivyokuwa hapo nyuma kwa maana ya viwango.
 
Mkuu hakuna anayependa kuvunja sheria lakini kuna tatizo kwenye hizo mizani. Ukipima kibaha uzito utapata tofauti na Mikese wakati mzigo uko kwenye container ambalo liko sealed. Sasa hiyo 5% ilikuwa ina ondoa hili swala la variation toka mizani moja mpaka nyingine. Halafu swala la barabara sio kwamba magari yanaharibu tuangalie na wajenzi wanaojenga je wanajenga kwa kiwango.Nakumbuka barabara ya chalinze -segera ilijengwa na Kapico mwaka 1984-89 iliweza kudumu mpaka 2010 wakapewa wachina ambao waliondoa ile ya Kapico nakuweka yao ambapo ilikuwa hata kabla hawajamaliza walikuwa wanaweka viraka kwa ambae anakumbukumbu anaweza kuchangia zaidi, maana hii barabara sasa sio kama ilivyokuwa hapo nyuma kwa maana ya viwango.
Umemaliza mjadala!Ndiyo ukweli wenyewe!!!
 
Magufuli has a metal block!! anafikiri uchumi wa nchi unajengwa na barabara nzuri tu zisizokuwa na vyombo vya usafiri!? Mara nyingi anakuwa na nia nzuri lakini top - down approach yake is very very detrimental to our national well being!
And he thinks he can develop Tanzania single handedly; Huyu JOHN POMBE"KALI" MAGUFULI has outlived his shelf life; its time for him to give way!
Barabara zenyewe anajenga sub standard kwa sababu ya 10%; the man can not listen to logic; too opinionated! hivi huyu Magufuli ni animist, a sadist, a chauvanist?! kwa nini hawezi kuzungumza na na binadamu wenzake akawasilikiza; wakamsikiliza tukapata muafaka?! kwa nini hajifunzi kutoka kwa Boss wake JK; mbona JK is more accomodating; more tolerant?! nani mkubwa baina ya JK na Magufuli!!????????????????; kwani yeye ndiye mwenye uchungu na nchi hii peke yake kuliko Rais?!
kwenye swala la barabara na bomoa bomoa zake aliaambiwa na JK na PM hadharani aache ubabe hakusikia!

what is wrong with this man!? this man needs psychiatric help probably!! msaidieni jamani!!

John Magufuli Tanzania sio yako peke yako; utaiacha. wisen up!

Adieu John Pombe Magufuli; God speed!
You have nailed it, brother! The guy thinks him alone can change the country. Him alone is the smartest. Him alone can translate the laws. Hajui kuwa uongozi unahitaji hekima zaidi kukiko kutafsiri sheria. Bomoabomoa aliendelea nayo ingawa alipingwa na Pinda na JK. Anatakiwa atimuliwe sasa.
 
​Magufuli ni janga la Taifa! Ashtakiwe kwa kuhujumu uchumi!
 
Safi sana mtoto wa mkulima nawatakieni Kila la kheri ndani huo mwezi mfikie suluhu ya kweli!
 
Back
Top Bottom