Mkuu lakini hii inaleta picha gani? Kwani gharama za kujenga barabara za lami kilometer moja ni kiasi gani? Hivi ni sahihi kuleta mambo ya siasa kwenye vitu vya kiufundi - binafsi nashindwa kuelewa kabisa, kuna mantiki gani Wasafirishaji wa barabara ambao baadhi yao ni waharibifu wakubwa wa barabara, na ndio wako very vocal wanapewa leeway ya kujadiriana na Magufuli ambaye anatetea kwa nguvu zake zote barabara zetu zisiaharibiwe ovyo na watu wenye jeuri ya pesa. Serikali yetu ina wajibu wa kumlinda, mradi hakihuki sheria/anasimamia sheria na sio kumfanya ajisikie mnyonge, ili suala la kumshinikiza afanye mazungumzo na wakihukaji sheria binafsi sihafikiani nalo - tusijaribu ku-undermine mawaziri wetu wachache wanao simamia sheria na kufanya kazi kwa ufanisi, kwa bahati mbaya hii si mara ya kwanza kwa ofisi ya Waziri mkuu kujaribu ku-clip wings za Mzalendo Magufuli - tunakwenda wapi ndugu zangu.Kwa nini hatutaki kujilinganisha na majirani zetu mfano: Kenya hivi wanaruhusu uzito kiasi gani kwenye barabara zao? Na kwa nini watu wachache hawa wanag'ang'aniza kuendelea kusamehewa malipo ya excess za tani tano mpaka wanafikia hatua ya ku-hold nchi nzima to ransom, kuna nini pale? Ni excess ya tani tano tu au kuna mengine ya ziada, isije ikiwa walikuwa wana-abuse msamaha huo kufanya madhala zaidi kwenye barabara zetu - na kwa nini wakasirike baada ya wapima mizani walio wazoea kutimuliwa kazi/kuhamishwa na Magufuli, yaani baadhi ya mambo mabaya wanayo mzuria Magufuli tusingekuwa tunaona matunda ya kazi zake tungemtilia shaka sana, Watanzania tu mabingwa sana wa kuwaharibia sifa watu ambao tunawaona ni tishio kwetu hiwe ni kisiasa au kibiashara - Dk.Magufuli na Dk.Mwakyembe wamekuwa victim wa Vices hizi kwa muda sana. Nimalizie kwa kusema Mzalendo Magufuli anapashwa kulindwa sio kumdhalilisha - hayo ni maoni yangu nimeyasema kwa nia njema tu.