Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Nadhani Pinda angeamuru Magufuli apigwe... Maana ni wote ni sawa tu...
 
Kwa sisi tulio kwenye hiyo industry tunajua kinachoharibu barabara si malori, bli viwango duni vya wakandarasi wanaopewa tenda za kujenga barabara pamoja na matuta wanayowekakwenye barabara kila kukicha!

Ni kweli barabara zetu nyingi zinajengwa chini ya viwango na maeneo mengi yenye matuta utakuta barabara zimeharibika sana. Kuna ulazima wa kuondoa matuta ktk barabara kuu,na kukwepesha barabara hizi kupita nje ya miji na vijiji.
 
:tinfoil3:
GT wa JF majanga tu, badala ya kudai kila mtu afuate sheria wao wanashabikia watu waruhusiwe kuvunja sheria. Kuna baadhi ya maeneo hata hiyo rami wahaijui, lakn maeneo mengine barabara zinafumuliwa kila baada ya miaka mitatu badala ya miaka 13 normal life span ya barabara ya rami. Kwa mtu aliyewahi kuendesha barabara ya chalinze Ruvu atakubaliana na magufuli kuzuia magari yasibebe mzigo kupita viwango vilivyopendekezwa..

Mkuu tatizo kubwa la tz ni viwango,,barabara zinajengwa chini ya viwango ndo maana unakuta baada muda mfupi zinaharibika, haohao kina Magufuli wanacheza na 10% return kwenye makampuni wanayoyapatia tender
 
Jana nilisema na ninarudia amri nyingine kuliko kusaidia zinahujumu. Jana nilisema wengi wawatakaodhurika na amri tukutu ya waziri wa ujenzi ni mawaziri wenzake. Wakati waziri wa fedha (TRA) anahaha kukusanya hela waziri mwenzake wa ujenzi halioni hilo ni mapato kiasi gani serikali ile ile imeyakosa kutokana na mgomo wa malori, bandarini mizigo imefurika, mambo hayaendi, mbolea haiendi na msimu ndio huu, mafuta hayaendi karibu kila kitu kitapanda bei, ujenzi wa barabara lazima utasimama hakuna mafuta hakuna vifaa vya ujenzi, wa Dar es Salaam wajiandae kutafuta mbadala wa nyanya, vitunguu, kabichi hoho nk, hospitalini wajiandae dawa karibu zitakosekana, mwenye akiba ya chakula na akitumie vizuri, wenzangu na mimi huko Iringa wajiandae kunywa komoni na ulanzi hakuna bia. Yote tisa kumi mfumko wa bei. Waziri yote haya hakuyaona. Namshukuru Pinda kwa kuokoa jahazi, watu wenye hekima hukaa mezani na kujadiliana huku shughuli zinaendelea, mtu jinsi hii tukimpa urais ni majanga.
 
Magufuli kapigwa KO ya mara ya pili na Mizengo. Aache kukurupuka. Bandarini meli zinashindwa kupakua shehena zimerundikana.
 
Safiiii safi sanaaa!!
''Tumechoka sasa, na waendeshe tu hayo malori yao...!!'' By Mizengo Pindaaa
Tumethubutu,tumeweza na sasa tunasonga mbele
KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI,KWANI NI FIKRA SAHIHI.
 
Iwe Magufuli kaamua vile au Pinda kaamua hivi...mwisho wa siku sisi wenye fikra pevu tunaelewa kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni DHAIFU.

Kati ya Pinda na Magufuli kuna mmoja amefanya maamuzi kwa hofu na wala sio matakwa ya Sheria zilizopitishwa kusimamia utunzwaji wa barabara.

Kumbe mwanasheria pamoja na kuzifahamu vema sheria anaweza kuvunja sheria kwa makusudi!
 
Sarakasi za serikali ya JK ni kiboko! Ndio maana nchi haisongi mbele, kila waziri na lake kama kwenye kilabu cha mataputapu vile
Nimekumbuka kichwa ni kidhaifu..
 
Huyu Magufuli hana lolote kazi kukunja kamdomo kama beberu aliyenusa mbunye ya mbuzi jike. Ni mla rushwa kama mla rushwa mwingine tu. Hivi ile ishu ya kumuuzia nyumba ya serikali kimada wake kwa bei ya banda la kuku pale Ubungo iliishia wapi vile?

Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Nimekugongea like mkuu .
 
Waziri mkuu mh Mizengo Peter ameamuru wizara ya ujenzi kuruhusu magari ya mizigo kuendelea na mpango wa zamani ili kunusuru uchumi wa nchi baada ya Wamiliki wa malori kugoma kwa kile kinachodaiwa ni kupinga amri ya Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli ya kutaka wawe wanalipa tozo la 5% ya mzigo unaozidi.

Akiongea na waandishi wa habari mh Pinda ameagiza wizara ya ujenzi kuruhusu magari ya mizigo kuendelea na utaratibu wa zamani kabla ya Mgomo na baada ya mwezi mmoja wataunda tume itakayo washirikisha Wadau wote ili kupata suluhu ya kudumu bila kuleta madhara.

Source;ITV HABARI

Pinda huyu wakati mwingine tusimsikilize sana, migogoro yote aliyojaribu kusuluhisha ilimshinda hadi JK mwenyewe anapokuja kumalizia. Tunakumbuka wakati ule alipozuia bomoa bomoa ya Magufuli kwenye hifadhi ya barabara Pombe alisema watu watadanganywa na wanasiasa wakati sheria ipo pale pale.
 
Anaetaka Kugoma aka Pack Lori lake Jikoni nisilione Barabarani-John Pombe Magufuli
 
Nilijua tu kitakachofuata ni tume. Nchi ya tume asubuhui, mchana, jioni, na usiku. Sasa undeni na tume kuchunguza umuhimu na uhalali wa waziri mkuu kulipwa milioni 26 kila mwezi bila kodi huku akilishwa, kuvishwa, kusafirishwa, kutibiwa, kulindwa bureee wakati wananchi masikini wanatakiwa kulipa kodi ya line na yeye anaunga mkono!
 
Hahahaha.....

Na mifugo iwe inapata Birth and Death Certificates kuweka kumbukumbu sawa hahahaha....

Ukistaajabu ya Musa ........ full ubunifu...aisee...nimecheka sana!

niweke sawa mkuu..... maana haya mambo ni ya muda kdg.
 
Back
Top Bottom