Pikipiki kwa Miaka 39 ya Utumishi, hii sio heshima bali Kejeli

Hiyo ni zawadi kutoka kwa staff wenzake, si kiinua mgongo wa si pension. Pikipiki haibatolewa na mwajiri bali staff wenzake kama zawadi. Zawadi ni kitu chochote tu, wengine hupewa suti n.k.
Duuuh hatari
 
Ndo ya walimu wakistaafu wanapewa bati 20 huku mijamaa imekaa CWT Hadi inagomea teuzi za wakuu wa nchi kazi kujichotea hela tu
 
Jiongeze, uza hizo bati, halafu huko bukoba zipigie katerero, urudi nyumbani mwepesi
Wakati huo Mke nyumbani anazisubili hizo bati kwaajili ya kuezekea Nyumba ilikua bado haijaezekwa Nyumba nzima
 
Huu ni udhalilishaji wa kiwango cha lami kabisa.
Ramadhani Mfaume ampewa zawadi ya pikipiki baada ya kuitumikia ofisi ya wizara ya habari, tamaduni na michezo kwa miaka 39 akiwa Mhudumu wa Ofisi.

Akimkabidhi zawadi iyo msemaji wa serikali Gerson Msigwa ameandika kuwa "Mzee Mfaume aliajiriwa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo huko nyuma ilibadilishwa idara mara kadhaa na yeye aliajiriwa wakati Idara ya Vijana ikiwamo.

KUAJIRIWA NI UTUMWA KIJANA AMSHA AKILI YAKO
kaa vijiweni endelea kulilia ajira
 
Kuna polisi mwaka Jana alitumia zaidi ya miaka name iliyopita na hayupo kazini, kisha kwa camera nyingi hapa mwaka Jana akatunukiwa kaburi janja (bodaboda)
 
Kauli ya Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, kuhusu kumuaga rasmi Bw. Mfaume Ramadhan baada ya miaka 39 ya utumishi wa umma imeibua mjadala mpana wenye maswali mazito kuliko majibu. Miaka thelathini na tisa si wiki mbili, wala si ajira ya muda mfupi. Ni karibu maisha yote ya mtu—ujana, utu uzima, na uzee—vimewekwa mezani kuitumikia serikali kwa uaminifu.
Bw. Mfaume, Mhudumu wa Ofisi, ameajiriwa tangu enzi za mabadiliko ya kiutawala ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; ameshuhudia misimu ya viongozi, sera, na majina ya wizara yakibadilika. Katika kipindi chote hicho, sifa zake zinasimama zenyewe: mchapakazi, mwenye nidhamu, mtulivu, msikivu, asiye na majivuno, na mpenda michezo. Huyo si mfanyakazi wa kawaida—ni nguzo tulivu ya taasisi.
Ndipo tunapofika kwenye kilele cha habari: zawadi ya kumuaga ni PIKIPIKI. Swali la msingi linajitokeza bila hofu—je, hii ni heshima au kejeli iliyofichwa kwenye tabasamu la sherehe? Taifa lenye bajeti kubwa, lenye magari ya kifahari na majengo ya mabilioni, linashindwa kumwonyesha mzee wa watu shukrani ya hadhi yake? Nyumba ndogo ya vyumba viwili? Gari la matumizi ya familia kama Toyota Noah? Hata pensheni yenye uhakika wa heshima? Hapana—pikipiki.
Hapa ndipo mjadala wa maadili ya utumishi wa umma unapopasuka. Tunawatuma vijana waingie kazini kwa moyo wa kujituma, lakini tunawaaga wazee wetu kwa ishara zinazoumiza tena zenye kebehi. Ujumbe unaofika ni hatari: jitume kadiri utakavyo, mwisho wa safari unaweza kuwa mdogo kuliko mchango wako.
Heshima si hotuba, ni vitendo. Kama kweli tunathamini utumishi wa umma, basi namna tunavyowaaga waliotumikia kwa uaminifu ndiyo kipimo cha utu wetu kama taifa.
Tanzania ndio nchi pekee duniani wanaweza kutumia bilioni kwenye sherehe za uzinduzi wa mradi wenye thamani ya milioni mia mbili.

Viongozi wanapenda sana sherehe kuliko maendeleo.

Viongozi wakistaafu wanapewa zawadi za mamilioni na viinua mgongo vya hadhi ya ulaya na marekani lakini mfanyakazi wa chini anapostaafu anapangiwa alipweje kiinua mgongo pamoja na kijisherehe cha bei nafuu kama huyo mzee.

Nataka kusema kwamba hata viongozi wenyewe hawajui wanatakiwa kufanya nini. Zamani tuliwachagua ili watutumikie lakini siku hizi wanateuana ili watufokee na kuturingishia ufahari wao.
 
Hao wanasiasa usitamani Sana mafanikio yao kwakuwa kuwa Mwanasiasa sio jambo jepesi pia
 
Kauli ya Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, kuhusu kumuaga rasmi Bw. Mfaume Ramadhan baada ya miaka 39 ya utumishi wa umma imeibua mjadala mpana wenye maswali mazito kuliko majibu. Miaka thelathini na tisa si wiki mbili, wala si ajira ya muda mfupi. Ni karibu maisha yote ya mtu—ujana, utu uzima, na uzee—vimewekwa mezani kuitumikia serikali kwa uaminifu.
Bw. Mfaume, Mhudumu wa Ofisi, ameajiriwa tangu enzi za mabadiliko ya kiutawala ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; ameshuhudia misimu ya viongozi, sera, na majina ya wizara yakibadilika. Katika kipindi chote hicho, sifa zake zinasimama zenyewe: mchapakazi, mwenye nidhamu, mtulivu, msikivu, asiye na majivuno, na mpenda michezo. Huyo si mfanyakazi wa kawaida—ni nguzo tulivu ya taasisi.
Ndipo tunapofika kwenye kilele cha habari: zawadi ya kumuaga ni PIKIPIKI. Swali la msingi linajitokeza bila hofu—je, hii ni heshima au kejeli iliyofichwa kwenye tabasamu la sherehe? Taifa lenye bajeti kubwa, lenye magari ya kifahari na majengo ya mabilioni, linashindwa kumwonyesha mzee wa watu shukrani ya hadhi yake? Nyumba ndogo ya vyumba viwili? Gari la matumizi ya familia kama Toyota Noah? Hata pensheni yenye uhakika wa heshima? Hapana—pikipiki.
Hapa ndipo mjadala wa maadili ya utumishi wa umma unapopasuka. Tunawatuma vijana waingie kazini kwa moyo wa kujituma, lakini tunawaaga wazee wetu kwa ishara zinazoumiza tena zenye kebehi. Ujumbe unaofika ni hatari: jitume kadiri utakavyo, mwisho wa safari unaweza kuwa mdogo kuliko mchango wako.
Heshima si hotuba, ni vitendo. Kama kweli tunathamini utumishi wa umma, basi namna tunavyowaaga waliotumikia kwa uaminifu ndiyo kipimo cha utu wetu kama taifa.

kama amefanya Kazi miaka 39 anashindwa kumiliki vitu vidogo Kama nyumba Magari binafsi n.k

Mimi naona hiyo pikipiki wamempa Kama Appreciation and nothing else.
 
Back
Top Bottom