Wewe ni aina ya kina mdude tu! Humfahamu mtu unayemsema
Muro aligombea udiwani kwasababu ya UKAWA! Tangu yuko CCM hakuwahi kuwaza kugombea udiwani
Alikuwa ni candidate sahihi wa kinondoni mwaka 2015 lakini CUF wakalalamika ndio ikabidi aachiwe Mtulia
Na kama hujui miaka yote akiwa CCM alikuwa anahujumiwa kwenye kura za maoni kupitishwa kuwa mgombea wa kinondoni
Aligombea udiwani kama sehemu ya kumpoza baada ya kukubali kumuachia Mtulia ubunge na kuendelea kubaki kwenye siasa na mahesabu yalikuwa aje kuwa meya wa kinondoni
Lakini kwa usaliti uleule wa viongozi aliousema wakamsaliti wakampa Boniface (my class mate) na kwasababu alikuwa mgeni kwenye chama na aliuamini uwezo wa Boniface, alikubali na akamsapoti
Ubungo na Kinandoni vilipogawanywa, akagombea umeya wa kinondoni lakini chama hakikumpa sapoti stahiki hadi CCM wakaweza kuiba kura (usaliti wa viongozi) na hata mahakamani walienda kutimiza wajibu tu
Kwa kifupi, Chadema ni chama kilichopendwa na chenye mvuto wa aina yake kwa vijana. Lakini wanachadema ndio watakayoiua chadema
Kuna watu ndani ya chadema wanahisi wao ndio chadema na chadema ni wao hivyo hawako tayari kuona mwingine anakua zaidi yao
Kazi aliyoifanya Mbowe ya kuwakuza kisiasa kina Mnyika, Zitto, Boniface na wengine siku hizi hata haipo tena
Kila anayetaka kuibuka wanampiga kwenzi abaki chini ili wao wabaki juu na kushangiliwa kila siku
Kifupi baadhi ya waliokuzwa na Mbowe hawahangaiki kuibua vipaji badala yake wanahangaika kutafuta mashabiki wa kuwapigia makofi na kutukana wanaowakosoa. Wanaogopa kuibua vipaji kwasababu wanaogopa kupewa challenge. Kutwa kucha wanahangaika kutengeneza mashabaki mwisho wa siku chama kitakosa wajenga hoja na yatakuwa yale yale ya ndioooo ambayo tunayaona CCM
Akisema Mbowe itakuwa ndioooo, akisema Mdee, Ndioooo, akisema Lema, Ndioooo, akisema Bulaya Ndioooo....akija wa kuhoji kilichosemwa mashabiki wazomee! Hii sio siasa! Huu ni ufuasi
Lazima kama Baba, Mbowe akae chini ajiulize na abuni mbinu mpya ya kuendeleza chama
Muro hajawahi na hatawahi kuwa na njaa ya pesa Kama unavyodhani labda afilisiwe!
Ni bahati mbaya kudhani kila anayeingia kwenye siasa anatafuta hela
Ungesema anapoteza muda na hela bure kwenye siasa ningekuelewa