Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,616
- 1,778
Ujima huu wa kisiasa sasa umevuka mipaka ya nchi yetu kiasi kwamba wale waliokuwa wanatuona sisi ni 'role model' kwao wameshuhudia kwa macho yao tukigeuka kuwa kichekesho na kikanda na dunia. Kutokana na historia ya kisiasa ya nchi yetu, kwa sehemu kubwa viongozi bado wanakuwa 'nominated' badala ya kuchaguliwa. Haya yametupata kwa sababu kuna taasisi na watu mmoja mmoja wenye dhamana ambao hawakuwajibika ipasavyo. Bila shaka wanatambua kuwa jambo baya zaidi kwa maisha ya taifa ni kurudia kosa.