Amejitahidi kueleza kwa utulivu kiasi cha kuaminisha kuwa kuna matatizo ya msingi ndani ya CHADEMA. Kinachoshangaza ni kuwa anaonyesha tangu aingie, alikuwa hakubaliani au hapatani na mengi yanayoendelea ndani ya chama hicho kiasi cha kujiuliza alikuwa anafanya nini huko muda wote huo? He has all the time been against the Party and its leaders. Alikuwa anafanya utafiti au ushushushu?
Pili, inakuwaje anaondoka kipindi hiki ambapo watafuta fursa (opportunists) wengi wanahama CHADEMA baada ya kutishiwa na dola kuwa nafasi zao zitaminywa na chama kitanyongwa katika uchaguzi mkuu 2020? Tatu, cha kushangaza zaidi, anahamia NCCR-MAGEUZI of all parties? Anatarajia mema yepi huko?
Mtu aliyeridhika na maisha yake si rahisi kujihusisha na siasa za vyama Tanzania kiasi cha kupania kwenda NCCR ya Mbatia. Kuna fursa huyu naye anaifukuzia. Na anajua NCCR na Mbatia wameandaliwa nini na Serikali ya CCM. He’s just another smart politician. Hiyo press conference ni kuwaonyesha mabwana wapya uwezo wa kuibomoa CHADEMA kwa “hoja”. Muendelezo wa dirty politics.