Nimemsikiliza vizuri Mustapha Muro mwanzo mwisho
Halafu nimesoma comment zote za waliochangia huu mjadala hapa
Mustapha Muro namfahamu vizuri sana. Simfahamu kama mwanasiasa tu, bali namfahamu kama msomi mtaalamu wa networking engineering, aliyewahi kuwa mmoja wa watu muhimu kwa kushika top position kwenye hii mitandao ya simu unayoifahamu hasa Vodacom ambapo alifanya kazi kwa muda mrefu
Namfahamu kama mfanyabiashara na mdau muhimu katika sekta ya mawasiliano hapa Afrika mashariki kwa kuwa miongoni mwa wamiliki wa makampuni ya minara
Namfahamu kama Baba mwenye familia imara, kaka, mjomba na aina ya mtu mstaarabu na ni miongoni mwa watu wenye siasa za kistaarabu na za kisomi
Mwaka 2015 kipindi cha uchaguzi mke wake ndio alikuwa mtu muhimu wa mfumo uliotumiwa kukusanya kura toka mikoani
Kwa kifupi, yeye ndio alikuwa organizer wa wale vijana waliokamatwa hotelini wakikusanya na kuhakiki kura kutoka majimboni
Baada ya sakata lile, mke wake na baadhi ya wanafamilia wake walipitia wakati mgumu sana maana walikamatwa wote na kufunguliwa kesi tofauti kabisa ya human trafficking. Mke wake alisota segerea karibu mwezi mzima
Muro kama msomi na mtu mstaarabu anajua anachokiongea
Hoja inayotoka kwa Muro si ya kubeza hata kidogo. Ni mtu mzima na anafahamu mengi ndani ya chama na ndani ya nchi hii
Ni bahati mbaya sana wanachadema wengi hadi sasa bado wanaamini katika siasa za matusi, udhalilishaji na kukoseana adabu
Ni bahati mbaya sana chadema bado inaamini aina ya ukosoaji wa kina mdude mitandaoni
Namfahamu Bwana Malisa, ni mtu wa chadema. Anaandika sana mitandaoni. Anakosoa kwa hoja. Sikumbuki kama ameshawahi kuonekana mkosa adabu na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi au udhalilishaji wa kimtandao
Ifike mahali tujadili hoja zinazotolewa kuliko kubeza na kujipa moyo kwamba chama kiko imara
Wanachadema wengi hata hamjui kwanini siku hizi Mnyika kawa kimya sana
Si jambo la kawaida sana wanamageuzi kama kina Mabere Malando, Prof. Safari na wengine wengi walioisapoti chadema nao wakawa wendawazimu kusema chadema haiko sawa
Kwanini? Lazima kuna kitu
Tuachane na hao wengine wanaolilia pesa ambazo wanafahamu kabisa kwanini walikuwa wanakatwa na miaka yote imekuwa hivyo
Tuachane na hao wanaolilia kudhalilishwa kingono kwasababu wanazozijua wao maana wanajua madawati rasmi ya kwenda kulalamika lakini hawakwenda
Tujadili hoja kama hizi za Muro. Ni hoja nzito zilizo na ushahidi na zinaweza kujadilika na kizuri zaidi hoja za Muro hazina majungu wala vijembe. Ni hoja ambazo zikichukuliwa zinaweza kukirudisha chama kwenye mstari
Huwezi kutaja umasikini wa Tanzania bila kuitaja CCM, huwezi kuisema serikali iliyoko madarakani bila kumtaja Magufuri. Hali kadhalika huwezi kutaja udhaifu unaotokea chadema bila kumtaja Mbowe!
Ifike mahali tukubali kwamba "huwezi kukwepa ngumi kwa kufumba macho"