Picha za matukio: Ziara ya Rais Samia Nchini Malawi akiwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. Chakwera

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye eneo la Kapeni View Point pamoja na Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati walipokuwa wakiangalia maeneo hayo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga cha kitropiki cha Freddy, Blantyre nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023.

2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye eneo la Kapeni View Point pamoja na Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati wakiangalia Video inayoonesha kuhusu maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga cha Kitropiki cha Freddy, Blantyre nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023.

4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye eneo la Kapeni View Point pamoja na Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati wakisikiliza maelezo kuhusu maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga cha kitropiki cha Freddy, Blantyre nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023.

5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake nchini Malawi kwenye Mkutano uliofanyika Blantyre nchini humo tarehe 7 Julai, 2023.

Nape.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati wakishuhudia utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Tanzania na Malawi kuhusiana na mashirikiano kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) mara baada ya mazungumzo yao Lilongwe nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023.

Aliyeketi (kulia) ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye wakisaini Mkataba huo pamoja na Waziri wa Habari na TEHAMA wa Malawi, Moses Kunkuyu Kalongashwa wa kwanza (kushoto).

Nape 2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera kwenye picha ya kumbukumbu na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye pamoja na Waziri wa Habari na TEHMA wa Malawi, Moses Kunkuyu Kalongashwa mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusiana na mashirikiano kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Lilongwe nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023.
 
Naona wanasaini kitu, si ajabu hapa ameuza Mlima Kilimamnjaro na wachaga wote
 
Mleta uzi umetukosea sana sisi Chawa wa Rais Dkt Samia kwa kuandika kichwa cha habari kwa kumuaddreaa rais Samia kimakosa. Anaitwa Rais Dkt Samia na siyo rais Samia, rekebisha heading yako Roving Journalist na usipofanya hivyo nitakugonga dislike
 
Back
Top Bottom