Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 59 ya Uhuru wa Malawi, leo Julai 6, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais Samia akishiriki Maadhimisho ya Miaka 59 ya Uhuru wa Malawi, leo Julai 6, 2023.



====

IMG_7915.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Malawi kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Nchi hiyo kwenye Sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.


IMG_7916.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati Gwaride la Heshima likipita mbele ya Jukwaa Kuu katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

IMG_7917.jpeg
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akicheza ngoma pamoja na kikundi kimoja cha ngoma za asili kutoka Malawi wakati wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi kwenye Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu Mutharika, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.
 
Back
Top Bottom