wewe Ben Saanane unasikitisha sana kwa Phobia yako uliyonayo kuhusu Zitto. Imani yako kuwa ili CHADEMA iwe chama kikuu cha upinzani basi kila mwana CHADEMA afanane kimtazamo ni kielelezo tosha kuwa ufahamu wako kuhusu Democrasia unatia mashaka, Kuamini kwako kuwa ili Maamuzi ya Chama na busara za mwenyekiti zinahitaji kuchunguzana kama KGB zinaonesha kuwa ingawa wewe ni kijana mtazamo wako hauna tofauti na babu yetu kingunge na cold war politcs.
CHADEMA hamumhitaji ZITTO kukubaliana na MBOWE kwa kila jambo ili muweze kukubalika kwa wananchi, ingawa sikubaliani na lugha ya kejeli iliyotumia "kama haukuwa edited kuyaongeza-kama mwandishi Mkumbo alivyosema". waraka ule was simply political ambitions za wahusika. Nyie vichwamaji wa chadema mmekuwa so "Hot Headed" mkakurupuka na kuusambaza kwenye Media. hilo lilikuwa kosa kubwa sana. Pale hamkujenga.waliyoyaandika kina Kitila Hayana Tofauti na mipango mnayopanga Chadema Kila siku ili kuiondoa CCM madarakani,sio Uhaini,sio Usaliti ni USHINDANI.
Inasikitisha kuona chama chenye neno DEMOKRASIA hakielewi "building block" ya demokrasia, kina Hillary Clinton walimpa Obama all sorts of names,lakini wakafanya naye kazi baada ya kuwa nominated. hivi mnaamini kabisa kuwa hawakuwa na "some sorts of" mpango mkakakti kama huu wa Zitto?
Kwa sisi tusio Tanzania na Tusioshiriki kwenye siasa za nchi yetu "on the ground" hali hii inasikitisha. Chadema Mlianza vizuri, bahati mbaya mmekuwa "paranoid" na mmelewa sifa mapema mno.kwa yanayoendelea sasa hivi Chadema inaonesha mkichukua nchi mtakuwa "more of the same".
Rudini kwenye Mstari wa kutafuta mageuzi kwa njia ya demokrasia,sio kufukunyua wasaliti kila siku ya mwaka. Nakuhurumia, kama kazi waliyokupa ni hiyo ya kufukunyua wasaliti."energy" unazaozitumia ungezitumia kufukunyua hija za kusaidia watanzania lingekuwa jambo la busara zaidi.
Ni jambo lililo la wazi kuwa Zitto ni "house hold" name Tanzania, kama walivyo Slaa,Mbowe,Kikwete,Chenge, Karamagi na Rostam,kila mtanzania anawafahamu kwa mabaya au mazuri. mashindano yako na Zitto kwenye kila hoja inayoletwa JF inaonesha kutaki kukubaliana na ukweli huo. mambo mengine ni busara kukaa kimya.