Picha ya siku: Tujikumbushe vituko vya awamu ya tano

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
35,187
2,000
Kuna exception kwenye taasisi za intelijensia mkuu
kama ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya ujasusi utagundua kuwa taasisi za kiitelligensia kuanzia CIA,FBI,MOSSAD ,za Russia na kadhalika zimekuwa zikifanya makosa ya wazi kabisa,ya kijinga na yenye gharama kubwa sana kwao.Mfano mzuri ni jasusi la Israel bwana Eli Cohen ambae alitumwa Syria na Mossad na kuna kosa kubwa tena la kijinga kabisa walifanya mossad ikasababisha huyu jasusi kudakwa na Syria na kunyongwa hadharini uwanjani mchana kweupe mbele ya uma huko Syria.
Eli_Cohen.jpg


Hizi taasisi huwa wanakosea pia na huwa wanakosea kwa sababu wao ni binadamu na binadamu siyo perfect.
 

Jerry Ekky

JF-Expert Member
May 6, 2018
1,200
2,000
kama ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya ujasusi utagundua kuwa taasisi za kiitelligensia kuanzia CIA,FBI,MOSSAD ,za Russia na kadhalika zimekuwa zikifanya makosa ya wazi kabisa,ya kijinga na yenye gharama kubwa sana kwao.Mfano mzuri ni jasusi la Israel bwana Eli Cohen ambae alitumwa Syria na Mossad na kuna kosa kubwa tena la kijinga kabisa walifanya mossad ikasababisha huyu jasusi kudakwa na Syria na kunyongwa hadharini uwanjani mchana kweupe mbele ya uma huko Syria. View attachment 1906199

Hizi taasisi huwa wanakosea pia na huwa wanakosea kwa sababu wao ni binadamu na binadamu siyo perfect.
Kosa gani lilifanywa?
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
35,187
2,000
Kosa gani lilifanywa?
Huko Syria kulikuwa na huyu jamaa👇
b17d0647-3451-4fa0-9f09-14f5f964f9ee.jpg

ambae alikuwa ni mkuu wa ujasusi katika jeshi.Sasa huyo jasusi wa Israeli alifanikiwa kujipenyeza katika Taifa la Syria hadi kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya jeshi na ilichukua miaka mingi hadi akafanikiwa kujipenyeza ndani ya serikali.Lakini tokea mwanzo huyu mwamba ambae ni mkuu wa ujasusi kwenye tawi la jeshi alikuwa hamkubali kabisa jamaa lakini viongozi wote katika Syria kuanzia Rais walikuwa wanampenda na kumkubali sana huyo jamaa kiasi kwamba Rais alikuwa na mpango wa kumfanya kuwa waziri wa ulinzi.

Sasa siku zilivyokuwa zinaenda kukawa kuna dalili ya vita kati ya Israel na Syria na wakati huohuo huyo mkuu wa ujasusi kitengo cha jeshi akawa anazidi kumkataa jamaa na kumshtukia.Na ndiyo mtu pekee serikalini alikuwa hamkubali jamaa

Jasusi wa Israel akaona kuwa siku zake huenda zinahesabika akaamua kurudi israel kimyakimya na kuripoti kwa mossad kuwa hali ni mbaya sana na huenda akashtukiwa kwa hiyo anaomba asirudi tena Syria.

Sasa kwa sababu ya presha ya vita kati ya Syria na Israel Mossad wakawa wana presha ya kupata taarifa zaidi kutoka Syria na wakasahau kuwa anachosema jasusi wao ni kitu proffesional kutoka kwa mtu professional kwa hiyo ni muhimu kumsikiliza.

Wakamlazimisha arudi Syria ili aendelee kunyonya taarifa.Syria ikashangaa kuwa habari zao zinavuja sana kwa israel hadi zile habari nyeti kabisa zinatangazwa na vyombo vya habari vya Israel.

Ikabidi Syria iombe msaada Russia kufanya msako ni nani anavujisha habari hizo.Russia wakaja na kivaa cha kunasa mawimbo ya radio kisha wakaliambia jeshi la syria kimyakimya kuwa wazime vifaa vyote vinavyotumia radio waves bila ya kumshirikisha huyo jasusi wa Israel kwa sababu tayari walikuwa wanamhisi.

Huyu jasusi wa Israel alikuwa na tabia ya kusafirisha taarifa kila siku saa mbili asubuhi kwenda Israel kwa kutumia kifaa cha radio waves nyumbani kwake.

Wale expert wa Russia wakanasa mawimbi ya radio ambayo hawayaelewi wakati wameshaagiza vifaa vyote vizimwe.Wakafuatilia kimyakimya yanapotokea mawimbi hayo wakamkuta huyo jasusi wa Isreal nyumbani kwake akiwasiliana na israel.Basi wakawa wamemnasa.
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
64,114
2,000
Mi mbona sijaona mtu akizungumzia uokotaji wa vichwa vya treni bandarini?
 

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
9,017
2,000

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
15,023
2,000
Uzuri wa serikali hufanya jambo makusudi ili anayejifanya anajua aaamini anachokijua bila kujua hajui
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom