Iko hivi , kwanza huwezi amini baadhi ya machifu ndo walikuwa madalali wa kuwakamata watu wao na kuwakabidhi kwa waarabu, ambao ndiyo walikuwa wakamataji wakubwa huku bara. Waarabu wakifika kwa machifu wanakuta mzigo tayari wanamkabidhi chifu nguo, shanga etc then wanachukua mzigo. Pale ambapo mzigo hautoshi chifu anawapa waarabu maaskari kwenda kusaidia kukamata watumwa. Hawa machifu wangekuwa kama akina Mkwawa au Mirambo mbona waarabu, ndo walikuwa maajeti wa wazungu, wasingetia mguu?? Sasa turudi kwa watawala wetu baada ya uhuru.... Kama ingetokea independent investigation ya namna viongozi hawa wameuwa na kuleta mateso makubwa kwa raia wao, ili tuu waendelee kubaki madarakani au tuu kwa sababu za kiukatili tuu (mfano mauwaji ya Rwanda ambapo mpaka vitoto vilikula risasi, au recent BBC documentary ambayo iko twitter where askari katili wanne wanawaongoza mama mwenye mtoto mgongoni na mwingine wa miaka kama sita mpaka kwenye kichaka kidogo na kuwamiminia risasi wote!!!), believe me wanaweza kukaribia waliochukuliwa utumwani.