Nawashauri hao wanaojuwa kulaan waanze kulaani upumbavu huu kwanza halafu ndio nitaelewa kweli wanasimama kwenye misingi ya haki.
[h=3]
Yaliyojiri Zanzibar[/h]
Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed
Baada ya jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wafuasi wa kikundi cha uamsho kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa kiongozi wao, hali inaendelea kuwa tete na hivi sasa baadhi ya wafuasi hao wameingia mtaani wakishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo huku jeshi la polisi likilazimika kutumia mabomu kuwatawanya wafuasi hao …..
Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini.
Waanamanaji hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja vya Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani Maskani ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya Lumumba.
Maandamano hayo walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa lililoandaliwa na Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la kuzungumzia mfumo wa elimu Zanzibar.
Akizungumza na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao ndani ya nchi yao....................