Pongezi kwa Zakazakazi kuufafanua mgogoro wa Israel na Palestina kwa facts na kuweka udini pembeni

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
asili ya mgogoro huu siyo dini bali ni ardhi. Wanagombania ardhi ya kuiita nyumbani, hawagombanii dini.

Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu ambao ndiyo wapalestina, eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.

2-ii.png

Kuna sehemu mbili za waarabu.

1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.

2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.

Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah, sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza, eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9 lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.

Asilimia kubwa ya watu wa Gaza ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu, hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).

kikundi hiki mechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel, ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.

ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel, kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.

Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni, wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani. Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru, Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena na baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.

Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina, hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao', Wayahudi wakasambaa Ulaya ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita, kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea na yeye kuwa Mkristo.

Constantine akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi, Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu., Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.

Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu, Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu, hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.

Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina lakini hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi, vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.

Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.

Lakini kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka pia nao Uingereza walikuwa na maslahi yao walipoitawala Palestina, waliwanyima wayahudi vibali vya kununua ardhi, kuweka ugumu wa kutoa vibali vya kuwaruhusu wayahudi wa Ulaya warudi Palestina sambamba na kukandamiza jitihada za wayahudi wanaopaza sauti kupewa eneo wawe na taifa lao.

Ni mpaka Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel, Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

"ramani ya pendekezo la umoja wa mataifa mwaka 1947 kuigawa ardhi ili kuwe na mataifa mawili"
asa-1.png


Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao la Israel, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.

......................................................................................................

Kabla ya kuendelea kwanza nikupitishe kwenye historia ya kiutawala ya nchi hiyo tangu kuingia kwa warumi, miaka zaidi ya 3000 iliyopita.


1. WARUMI

Wakati wa utawala wa warumi kwenye nchi yao, dini ya wazawa ilikuwa moja tu, uyahudi, baadaye mnamo karne ya kwanza ikazaliwa dini mpya kutoka uyahudi ambayo ilianza kama tawi la uyahudi na baadaye ikaitwa dini kamili, Ukristo.

Warumi walikuwa na dini zao za kipagani na waliwalazimisha wayahudi na wakristo kuzifuata.,waliweka sheria kwamba lazima wayahudi na wakristo watoe sadaka kwa miungu ya kirumi na masanamu, baadaye wayahudi wakaondolewa ulazima huo kwa fidia ya malipo maalumu yaliyoitwa Fiscus Judaicus yaani Kodi ya Wayahudi.

Lakini wakristo hawakupewa hiyo nafasi, badala yake walitakiwa kutekeleza tu sheria ya sadaka kwa miungu ya kirumi, warumi hawakuupenda kabisa ukristo na ilikuwa kosa kisheria kuwa mkristu, ndiyo maana waliwalazimisha kufanya ibada za kipagani.

Ilipofika karne ya pili, ndipo wayahudi wakaanzisha vita kubwa ya kudai uhuru, kwa hasira warumi wakawafukuza kabisa wayahudi katika nchi yao na kuibadili jina na kuwa Palestina, wakaweka marufuku kwa wayahudi kurudi katika nchi ya Palestina.

Mnamo karne ya nne, mtawala wa warumi, Constantine, akaupokea ukristo na kuufanya kuwa dini kuu ya warumi, hii ni baada ya kuona kwamba ukristo ulikuwa unakuwa kwa kasi na hata yeye alibadili dini kuwa mkristo, lakini pia alitaka kuitunza amani ya nchi kwa kuondoa ukandamizaji wa kundi linalokuwa kwa kasi.


Ukristo uliposambaa ulaya kulikuwa na chuki dhidi wa wayahudi (Anti-Semitism), sababu kuu zilikuwa ni kwamba wayahudi walionekana wauaji wa Yesu Kristo na dini yao haimtambui Yesu. Matukio kadhaa yakiwemo mauaji yalifanyika kwa wayahudi, Kusambaa kwa elimu ya dini ndiko kulisaidia kujua kwamba hata alieamuru kusulubiwa kwa Yesu hakuwa Myahudi bali ni Pilato wa warumi ambao waliabudu masanamu kwa muda huo.
2. DOLA ZA KIISLAMU

Mnamo karne ya sita dini mpya ilizaliwa kutoka makabila ya kiarabu, yakiongozwa na Mtume Muhammad (SAW). Muhammad hakuwa tu kiongozi wa kidini bali pia kisiasa, alizaliwa mji wa Maka na baadaye kuhamia mji wa Yathrib.

Alipohamia mji huu, wenyeji wakaubadili jina na kuuita Madinat Al Nabii yaani mji wa Nabii, ndipo mji huu ukaitwa Madina. Akiwa hapo Muhammad SAW akaanzisha taifa jipya la kislamu lililorudi na kuuteka mji wa Maka, alipofariki nafasi yake kisiasa ikarithiwa na Abu Bakr halafu akaja Umar au Omar.

Huyu Omar akaitanua nchi hadi kufika Palestina, chini ya tawala za kiislamu, mambo yakabadilika sana Palestina, Ile marufuku ya warumi juu ya wayahudi kurudi ikaondolewa...wayahudi wakaruhusiwa kurudi Palestina.

Waislam, wayahudi na wakristo wakaishi pamoja nchini Palestina chini ya utawala wa Omar.

Mji mkuu wa Jerusalem uliruhusu dini zote tatu, waislamu waliwaita wakristo na wayahudi DHIMMI, ambayo maana yake WATU WA KULINDWA, Waliwaita hivyo kwa sababu walikuwa Ahl Al Kitab yaani watu wa taifa la kitabu, kwenye kitabu cha waislam yaani Koran, wakristo na wayahudi wametajwa kwamba wamepewa kitabu na Mungu cha miongozo ya kumuabudu.
3. CRUSADERS

Baada ya karne nyingi za kuwa chini ya tawala za kiislamu, wakristo wa Ulaya wakataka kuurudisha mji wa Jerusalem na nchi ya Palestina mikononi mwao, wakaanzisha harakati zilizoitwa CRUSADE, yaani vita vya msalaba, waliopigana vita hii waliitwa Crusaders, hii ilikuwa vita iliyopiganwa kwa miaka zaidi ya 200 kuanzia 1095 hadi 1291

IIianza mwaka 1095 baada ya kiongozi wa kanisa katoliki, Papa Urban II, kuitisha kongamano kuu la Clermont kuwataka watu wa Ulaya kutumia kila aina ya uwezo walionao kuuchukua mji mtakatifu wa Jerusalem kutoka kwa waislam, ulaya iliitikia wito huu na wafalme wake wakatuma jeshi kubwa lililoenda kuuteka mji huo na nchi yote ya Palestina, na miji mingine ya karibu.

Chini ya utawala wa Crusade, Palestina haikuwa tena mahala salama kwa wengine zaidi ya wakristo, waislam na wayahudi waliteswa na kuuawa, Hii ilipelekea ulazima waungane kupigana dhidi ya Crusaders.

Wakiongozwa na Sultan Saladin, wakafanikiwa kushinda na kuwapindua Crusaders.

Hata baada ya Papa Urban II kufariki, Mapapa wengine waliofuata waliendelea kutuma misafara mingine katika awamu saba zaidi na kufanya jumla kuwa na misafara nane ya Crusade ambazo zote hazikufanikiwa kuirejesha Palestina mikononi mwao, Wafalme kadhaa wa Ulaya waliamua kwenda wenyewe vitani kuongoza mapambano katika misafara tofauti mfano ukiwa ni Mfalme Richard The Lion Heart wa Uingereza aliongoza Crusade ya tatu lakini haikufanikiwa.
4. SALADIN

Dola ya kiislam ilikuwa ikiangukia kwa watawala tofauti kulingana na koo zao, nao walihamisha makao makuu kupeleka walipopata au kwenye asili yao.

Kwa mfano, wakati wa Mtume Muhammad SAW, makao makuu yalikuwa Madina, Ali ibn Talib, alihamishia mjini Kufa katika nchi ambayo sasa ni Iraq, Umayyads watu wa Syria wakahamishia huko kwao makao makuu, Hali ilienda hivyo hadi dola ikawa chini ya Sultan Saladin aliyechukua madaraka kutokea Misri.

Chini ya Sultan Saladin,Waislam walijipanga na kuirudisha Palestina mikononi mwao.

Saladin hakulipa kisasi kwa wakristo bali aliwaruhusu waendelee kuishi na kufanya ibada zao bila tatizo lolote, Yeye ndiye aliyekabidhi kwa familia ya kiislamu ufunguo wa kanisa kuu la Holy Sepulchre ambapo wakristu wanaamini ndipo alipozakiwa Yesu, alipokufa na kuzikwa.
5. OTTOMAN

Kutoka kwa Saladin, Palestina ikaangukia kwa utawala mwingine wa kiislam wa Ottoman, maisha yaliendelea kuwa ya pamoja kati ya dini zote tatu kubwa za eneo hilo.

Updated uingereza
6. UINGEREZA

Kuanzia 1914 hadi 1918 dunia ilikuwa kwenye vita kuu ya kwanza, pande mbili za wababe zikigombania heshima, Uingereza na washirika wake dhidi ya Ujerumani na washirika wake ikiwemo Himaya ya Ottoman iliyokuwa na mamlaka Palestina,

Mwaka 1917 wakati vita vya kwanza vya dunia vimechanganya, Uingereza ilitaka sapoti ya wayahudi ambao walitapakaa Ulaya. Kupitia Azimio la Balfour, Uingereza ikawaahidi wayahudi kuwasaidia kupata taifa lao endapo watajiunga nao kwenye vita kuwapindua Ujerumani na washirika zake ikiwemo himaya ya Ottoman.

Ujerumani na washirika wake wakashindwa vita hii, washindi waliwafanya vibaya sana walioshindwa, walihakikisha wanawafilisi ili wasije kurudia chokochoko, na pili ili kufidia hasara walizopata kwenye vita, Ujerumani ikanyang'anywa makoloni yake yote likiwemo la Afrika Mashariki ambalo lilijumuisha eneo la sasa la Tanzania Bara, Rwanda, Burundi na kipande fulani cha Msumbiji. Washindi wakaligawa eneo hili kisha kugawana kwa dhamana ya umoja wa mataifa, Uingereza ikakata kipande kikubwa cha Mashariki na kukiita Tanganyika, Ubelgiji ikachukua vipande viwili vya Magharibi na kuviita Rwanda - Urundi.

Ottoman ilitawala eneo kubwa la Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na katikati ya Ulaya na Asia (Euro-Asia), Uingereza na Ufaransa wakaenda kuchukua maeneo hayo na kuyagawana kama makoloni na mengine kama dhamana ya umoja wa mataifa, Palestina ikaanguakia kwa Uingereza kwa dhamana ya umoja wa mataifa.

Uingereza ilipoichukua Palestina, ukawa ni wakati rasmi wa kukamilisha ahadi ya kuwasaidia wayahudi kurudi Palestina wapewe eneo wawe na taifa lao, lakini sasa maslahi binafsi ya Uingereza yalivuruga utekelezaji wa hii ahadi, Hawakutoa ama walitoa ulinzi kidogo pale waarabu waliposhambulia wayahudi waliorudi na vurugu hizi wakazitumia kimaslahi kuweka ugumu wa kutoa vibali vya kusafiri kwa wayahudi wa Ulaya kurudi Palestina, waliweka ugumu kwa wayahudi kupata vibali vya kununua ardhi, waliua na kuwafunga wayahudi walioshinikiza Uingereza itimize ahadi yake ya kuwapa taifa lao.

Ilipelekea kuanzishwa kwa vikundi vya kiyahudi kama Irgun Zvai na Lohamey Heruth Israel vilivyowalinda wayahudi waliposhambuliwa na waarabu bila kulindwa na Uingereza, pamoja na kuishinikiza Uingereza itimize ahadi yake ya kuwapa eneo ili wawe na taifa lao, vikundi hivi vilionekana na Uingereza ni vya kigaidi, Kufikia mwaka 1947 maafisa wa Uingereza zaidi ya 700 ndani ya Palestina waliuawa na vikundi hivyo.

Vita vya pili vya dunia vikiwa vimechanganmya, Ujerumani ikiwa inaongozwa na Dikteta Hittler yalifadhiliwa mauaji mauaji ya kinyama (Holocaust) kuhakikisha wayahudi wanauawa wote, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kwa njia za kinyama zikiwemo kuwapiga risasi, kuwafunga katika makambi bila chakula wala dawa hadi wafe kwa njaa, kuwaua kwa gesi ya sumu katika makambi maalumu na vikosi maalum viliundwa kuua wayahudi majumbani. Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yalichangia kwa kiasi kikubwa kurudisha tena harakati za wayahudi kupewa taifa lao, tena kwa wakati huu, Umoja wa matafa nao uliingilia.

Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.

Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo. Kuanzia hapo ndipo machafuko yote ya sasa yanakuja

Itaendelea ....
 
Naomba kujua asili halisi ya wapalestina?@sky soldire ili tuwaombee tu wakakatiwe kaeneo hata size ya dar waunde taifa lao?wasipoangalia miaka 100 ijayo wapalestina watakua wamebaki 50%duniani kote
 
Waisrael (daudi) alipigana na wafilisti(falastini)..
Watu wanapotosha sana.
Wafilisti walikuwepo enzi na enzi zaidi ya miaka 500 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Enzi za Ibrahimu,
MImi ni Mkristo.
Ukweli ni kwamba Wafilisti ndio
Wakaazi wa kwanza pale Kanaan/Israel.

Ona
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:14
Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

Mwanzo 21:32
Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 21:34
 
Watu wanapotosha sana.
Wafilisti walikuwepo enzi na enzi zaidi ya miaka 500 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Enzi za Ibrahimu,
MImi ni Mkristo.
Ukweli ni kwamba Wafilisti ndio
Wakaazi wa kwanza pale Kanaan/Israel.

Ona
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:14
Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

Mwanzo 21:32
Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 21:34
Umemaliza kila kitu.
 
Watu wanapotosha sana.
Wafilisti walikuwepo enzi na enzi zaidi ya miaka 500 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Enzi za Ibrahimu,
MImi ni Mkristo.
Ukweli ni kwamba Wafilisti ndio
Wakaazi wa kwanza pale Kanaan/Israel.

Ona
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:14
Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

Mwanzo 21:32
Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 21:34
Mawazo yako ni kama yangu niliochangia sehemu flan kuhusu chanzo cha mgogoro. Watu wengi hawaanzii mwanzo wa mgogoro. Wao wanaanzia Israeli kashaingia Kanaani na kuvamiwa na warumi kisha wapalestina wakachukua ardhi yao. Sijui ni maksudi au wanasahau.

Kingine ambacho sijui, hawa wapalestina ndo wale wafilisti wa mwanzo au hawa ni wengine? Na kama sio, wafilisti wa kale masalia yao ni akina nani wa sasa?
 
Mawazo yako ni kama yangu niliochangia sehemu flan kuhusu chanzo cha mgogoro. Watu wengi hawaanzii mwanzo wa mgogoro. Wao wanaanzia Israeli kashaingia Kanaani na kuvamiwa na warumi kisha wapalestina wakachukua ardhi yao. Sijui ni maksudi au wanasahau.

Kingine ambacho sijui, hawa wapalestina ndo wale wafilisti wa mwanzo au hawa ni wengine? Na kama sio, wafilisti wa kale masalia yao ni akina nani wa sasa?
Mkuu
Mfilisti=paletian
 
Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.

Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.

Photo by thabith chumwi zakaria on October 10, 2023. May be an image of map and text that says...jpg


Kuna sehemu mbili za waarabu.

1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.

2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.

Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.

Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.

Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.

Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.

Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.

Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).

Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.

Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.

ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.

Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.

Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.

Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.

Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.

Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.

Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.

Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.

Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.

Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.

Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.

Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.

Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.

Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.

Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.

Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.

Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.

Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.

Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.

Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.

Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.


Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.

Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.

Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

Ramani inahusika.

View attachment 2778309

Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.

Itaendelea...
Pdf yake tafadhali, kitu tamu sana hii
 
Abraham/Ibrahim aliishi wapi
Watoto WA Abraham/Ibrahim ni Akina Nani.
Makabila yaliokuwepo huko ni yapi.
Kuna makabila 12 ya wayahudi ni yapi.

Wayahudi walivyokwenda utumwani Misri , nchi Yao ilikaliwa na Nani.

Walivyo Rudi toka utumwani waliishia wapi , na nchi ya ahadi ilikuwa ipi.

Hii itakuwa agano la kale .

Na baada ya agano Jipya kuondoka Kwa wayahudi ilikuwaje na nchi Yao ilitwaliwa na Nani.
 
Back
Top Bottom