Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

:hand: we acha tu imekuwa gunzo nenda mwenyewe ukapate ushuhuda c kuuliza watu kama unavyofanya.kaka kama unaukimwi nenda utapona
 
Baba yangu anayeishi Arusha alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukali amepona baada ya kutumia dawa yake wiki mbili zilizopita,baada ya kupimwa imeonekana kwa sasa hana ugonjwa wa kisukali tena!!
 
Ni kweli usemayo yaaani alitendalo mungu binadamu hana nafasi ya kutengua tumuachie mungu hayo yote.loo yaani ni sh 500 tu do yaani nim kweli ni miujiza ya mugu
 
Mimi nadhani badala ya wizara kufanyia utafiti dawa hiyo, kitu ambacho majibu yake yatakuwa sintofahamu, ingefanya yafuatayo;
-Kuchunguza miongoni mwa waliokuwa wagonjwa wa maradhi tajwa na kujiridhisha kwamba wamepona au la,
-kuwafanyia uchunguzi watu hao ili kujiridhisha kwamba hakuna side effects in future hata kama sasa wamepona,
-kushirikiana na serikali wilayani loliondo kuboresha mazingira ya eneo la Mchungaji ili dawa itolewe katika mazingira safi na salama.
 
ninashangaa sana watu wanapokuwa na wivu wa kiroho kama alivyojiweka wazi kakobe. Ikiwa mzee yule ameonyeshwa na Mungu au si Mungu kakobe hapaswi kumshutumu kwa namna hiyo kwani yeye kakobe ana namna ambavyo Mungu humtumia yeye binafsi. Mungu anavyomtumia x ni tofauti na anavyomtumia Y ndiyo maana katika Biblia miujiza ilikuwa tofauti tofauti kwa kila mtumishi/mtume wa Kristo na hata kristo mwenyewe. Wakati Kristo aliponya wengi, hakuna mahali Biblia inasema watu waliponywa kwa kupitia na kivuli chake kama ilivyokuwa kwa Petro na Yohana. Na Biblia hiyo hiyo haisemi kuwa kwa kugusa mavazi ya Mitume watu waliponywa kama ilivyo kuwa kwa Yesu.

Kakobe anapaswa ku-shutup
 
Ama kweli watu wana shida, hivi ni kweli kwamba dawa ya aina moja inatibu magnjwa ya aina mbali mbali .........au .......imani yako inakuponya.?......maana mambo mengine yanachanganya, unywe dawa aina moja tena kwa muda mfupi, upone ukimwi, kansa, kisukari.........eh.

Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo bayana na yasiyoonekana, (embu amini basi hta kidogo) au mpaka waje watu wa marekani ndo mtawaamini
 
Binafsi sijaenda Loliondo ,lakini haijaninyima kutafuta shuhuda za watu mbalimbali ili kujua nini kinaendelea . Mchungaji Mwasapile amepata ufunuo na kuoteshwa katika ndoto,akakabidhiwa kikombe ambacho atawapatia watu dawa nao watapona magonjwa mbalimbali yakiwamo ya kisukari,pumu,presha na hata ukimwi na magonjwa mengine sugu .kama una virusi ukishapatiwa dawa hiyo baada ya siku saba utaitajika kwenda kupima ili ukiri mwenyewe muujiza wako .


Kwangu sio tiba ya kisayansi na napinga wale wote wanaotaka kuingiza ubinadamu na hata usayansi wao katika hili . katika mambo haya ya kiroho hatua zozote za kibinadamu zitashindwa kabisa . kakobe kumpinga mchungaji huyu ilhali wapo mashuhuda wa miujiza hii ni anaonekana jinsi alivyo pindi anapokosa la kusema . Kama kakobe ataongea katika mlengo wa ushindani wa kibiashara katika huduma ya kiroho analipeleka wapi kanisa lake . Ina maana kama ni kweli yeye ( kakobe ) ana ufunuo wake ina maana hakuna mtu mwingine yeyote anaeweza kupata ufunuo kama wake na hata kumzidi .maneno yake dhidi ya mchungaji mwasapile hayana tija,hayafai kusikilizwa na anajivunjia heshima yake.

Jumapili katika vijiwe vyetu vya weekend tumepata watu wakishuhudia miujiza yao . Kuna mzee mmoja alikuwa na presha mbaya kabisa leo hii presha yake ipo normal .Sijapata shuhuda wa HIV lakini wapo na nimesoma kwenye vyombo vya habari . Jana tarehe saba nimekutana na mzee mmoja / mfanyabiashara katika maongezi yake amesema sukari yake kwa sasa ipo normal . Alikuwa dhaifu sana mwanzoni na katika safari yake ya kurudi kutoka Loliondo alipofika mto wa mbu alikula Chips mayai kitu ambacho ni nadra sana kwa watu wenye kisukari.

Katika maelezo haya tunapaswa kuelewa kwamba uwepo wa mungu ni dhahiri,hasa kwa wale wanaomtumaini . Waliokuwa na mizigo yao ya maradhi hatimaye mungu amekuja kiuhalisia kumtumia mtumishi wake Mwasapile ili kuponya .

Wagonjwa wote wenye matatizo sugu waanze kuelekea loliondo . Zipo Changamoto kadhaa hasa za usafiri na wingi wa watu . Wajasiriamali wameshatumia mwanya huu na nauli kwenda na kurudi Lolionda kutokea Arusha ni Sh 100,000 kwa sasa . Usisahau 500 ya mzee yeye hana makuu kwani ana roho mtakatifu na sio roho mtaka vitu .Katika 500 hiyo 200 ni kwa ajili ya wamama wanaochemsha dawa,200 ni kwa ajili ya kanisa na mia ndio ya kwake.

Leo asubui nimemsikia naibu waziri wa afya akiongea na waandishi wa habari anasema wizara haiwezi kutoa tamko juu ya tiba hiyo lakini wanafuatilia ubora wa tiba hiyo na mazingira inapotolewa. Hapa namshauri mheshimiwa waziri abadili mawazo yako ,aondoe huo uchunguzi wake. Atakuta anachunguza matendo ya mungu ambapo ni dhambi kubwa . Hakuna chembe ya ubinadamu katika hili . Dawa hiyo hiyo inaponyesha ukimwi,kisukari na hata presha .hashangai ! Asije akatuma na/au akaunda tume katika hili kwani atashindwa.

Natumaini Mmenisoma

Hapo kwenye nyekundu nakuunga mkono Mkuu!! Kama kweli watu wanapona magonjwa mengi, hiyo siyo dawa bali ni miujiza ya Mungu. Hakuna dawa ya kisayansi inayotibu magonjwa mengi kiasi hicho, ila miujiza
 
jamani huyu babu alikuwa wapi cku zote asijitokeza kuokoa taifa linaloangamia?
 
kama mtu amepona atujuze yeye mwenyewe ili watanzania tujue kwani nina imani watu wengi ni wagonjwa. Aliyepona atuhabarishe kwani nae kapata uponyaji kutoka kwa Mungu kupitia babu nae kapewa bure! 500/=
 
Wamleta muhimbili au viwanja vya mnazi mmoja kugawa DOZI za magonjwa mbalimbali.

Mnasubiri nini?
 
Wajameni naomba mnijuze kuhusu huyu babu wa loliondo. Kuna mtu amepona? Kama kuna mtu naomba ushuhuda wake!

Hili ni jukwaa la siasa. Je, huyo babu alikuwa mwanasiasa? au anatibu wanasiasa tu.
 
mimi naamini ktk miracles babu anaponya lkn ugomvi mkubwa utakuja serikali itakapojidai kuthibitisha hizo dawa huko maabara na kukosa ushahidi through ma kemikaki yao na kusema dawa siyo halafu watajidai kupiga marufuku hapo nadhani wananchi watacharuka km mbogo
 
hili jukwaa ndilo linakuwa visited na watu wengi ndio maana nipost hii thread hapa! Kwa wale wanaojua reseach hii ndio good representative sample ya kupata response nzuri iwe positive or negative
 
kuna kakobe na huyu bwana wa clouds anaitwa KIBONDE jana kaniboa saana yeye anashupalia eti uchunguzi ufanyike ili ijulikane km ni dawa kweli au eti wakithibitisha sio dawa side effect yake itakuwa kubwaaaa. mimi nampa ushauri KIBONDE mambo ya mungu hayapimwi kwenye test tube maabara mtaishia kugombanisha watu tuuu acheni kazi ya mungu iponye watuuu msiwe na wivuuu
 
Back
Top Bottom