MAONI YANGU:
Kwa sababu CCM na Serikali yake hawawezi kufanya kazi hadi wasukumwe na Chadema, basi naomba Chadema na hasa Wizara KIVULI husika na mambo ya Afya, Usafiri, Maji, Mawasiliano nk wafanye kikao na kuingilia kati hili swala.
Kama alivyopenedekeza mmoja wetu hapa, iwepo ofisi ya Booking mjini au mji mdogo sehemu fulani na watu wawe wanakwenda huko kwa makubaliano mapema. Iwepo booking na watu wajue watafika lini huko. Hawa wa bahati mbaya, waachwe wale tu ni mahututi na wenyeji wa eneo hilo ambao hawataweza tena kwenda hadi Arusha kufanya Booking.
Vinginevyo basi, hao watu wa kusimamia Booking, wawepo hapohapo kwa Babu na Computer zao/Simu zao. Unaweka booking na kujua kabisa siku fulani ndiyo uende.
Hivi vitengo vya kushughulikia MAJANGA kwa Tanzania vipo kweli au ni POROJO tu?
Chadema naomba tena, mkilivalia njuga hili swala, CCM watakurupuka kama kawaida ya na kujifanya ni lao. Ila mwisho wa siku, watu watafaidika na kupunguziwa matatizo yanayokwepeka. Utafikiri sijui tunaishi dunia gani?
Naomba watu wa Chadema wajulishwe kuhusu hii kitu na kwenye mawazo mengine basi na tuboreshe na utaratibu mzima wapelekewe Chadema na hapo watakapoutangaza, basi FIMBO itamchapa Kalumekenge na Kalumekenge (CCM) atakwenda shuleni..........