Picha: Mwingine familia ya Nyerere ajiunga CHADEMA

Last edited by a moderator:
Watoto wa Nyerere wanajulikana hii tabia ya ktumia majina ya wa tu kwa umaarufu haifai,Esther na Lilian Wasra nao walijifanya kama watoto wa Wasra kumbe ni geresha,sasa Mzee Joseph Nyerere nae ni nani katika nchi hii hadi mtoto wake apewe coverage kisa kujiunga na Chadema! Au mnatumia Jina la Nyerere kujifanya kama ni watoto wa Mwl Nyerere!

Joseph Nyerere alishashika nyadhifa tofauti katika nchi hii. Alishakua Waziri Mdogo wa Utalii, Mkuu wa Mkoa Mwanza n.k. pia alikua mbunge wa muda mrefu, na alishakua mbunge wa East Africa Legislative Council. Mengineyo, wazo la kuanzisha JKT ni la kwake, alitoa Israel, na pia alianzisha TANU Youth League, ambayo sasa ni UVCCM.
 
Waislamu wamekataa kuchinja sasa sijui kitimoto tutakulaje, Viva CDM
 
Movement za kibongo za kishamba sana too primitive,sasa huyo F.Nyerere ananizidi nini mimi au ndo mnaanza yale yale ya CCM ya kujuana(usultani) ukiwa na jina kubwa tu unang'aa,Usishangae muda si mrefu akapewa cheo huyo kisa mtoto wa Nyerere,siasa za kiafrika ni kama pipa na mfuniko tu.
 
Mwalimu Nyerere amefariki ameacha watoto saba tu.

1) Andrew Nyerere

2) Anna Nyerere

3) Magige Nyerere

4) John Nyerere

5) Makongoro Nyerere

6) Madaraka Nyerere

7) Rosemary Nyerere

Hao wengine wanaotumia jina la Nyerere watakuwa wanandungu wa Butiama tu au Makoko.

CC. Kimbunga, Pasco, Mingoi, Mlengo wa Kati, Ng'wamapalala, Butola,

kwa hiyo watoto wa Kambarage pekee ndo wana haki ya kutumia jina la Nyerere?grow up
 
Last edited by a moderator:
nimeipenda hiyo.... ngoja ni dedicate na kawimbo..... Ona Ridhiwani hafanani na Makongoro... by Roma
 
Mkuu Butola, comments nyingine ni za hatari sana!, angalia zisije zikaingiliana na zikatutibulia ule mchakato wetu wa Mwenye Heri kuelekea kwenye Utakatifu!.
P.

Mkuu Pasco hiyo lugha sio mimi tu ninayeitumia bali pia Mwenyezi Mungu mwenyewe kupitia maandiko ya Biblia...




Refer: 2 Mambo ya Nyakati 6:8-9"...Bwana akamwambia Daudi Baba yangu, umefanya vyema kuwaza kujenga nyumba ya Bwana ya Bwana,.....lakini si wewe utakayeijenga nyumba hiyo bali "MWANAO ATAKAYETOKA KWENYE VIUNO VYAKO"....
 
Mimi,pamoja na Watanzania wengi bado hatujaona kwamba CCM ina matatizo,ndiyo maana bado ipo madarakani.

Babako hakuwa mchumia tumbo, wewe unaanza kuwa mchumia tumbo uzeeni utaweza?...Sitaki jibu lako ila ninauhakika dhamira inakusuta sana...wee endelea kutoza ada kwa waokuja kuhiji kaburi la baba...

RIP Mwalimu ulipigania nchi hii lakini wale maadui uliokuwa unapambana nao kwa dhaati wameongezeka sasa wamefika wa 4! UFISADI, UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI...
 
Mimi,pamoja na Watanzania wengi bado hatujaona kwamba CCM ina matatizo,ndiyo maana bado ipo madarakani.

Mkuu Watanzania wengi wangapi? Mwaka 2010 Watanzania tulikuwa wangapi kwa makadirio? na ni Watanzania wangapi tulipiga kura? Je ni Watanzania wangapi waliopia kura CCM? Mwisho ni Watanzania wangapi ambao wahakupiga kura? Na unadhani ni kwa nini hawakupiga kura?
 
Tusubiri mkapa atuambie kama aliwahi kumfahamu huyu kamanda Francis Nyerere.

Hii ni hatua kubwa sana ya kuonyesha namna Chadema inavyowavutia watu wa kada mbalimbali.

Hakuna cha ajabu labda kama mmeingia kwenye siasa za tz baada ya slaa kugombea urais,kihistoria babaake huyu kijana alikua mpinzani hata wa serikali ya kakaake,na ndi miongoni mwa watz wa mwanzo kabisa kuwa kwenye upinzani kabla hata slaa hajaujua na kuukubali upinzani,so hapo hakuna ajabu ni suala la maji kufuata mkondo tu.
 
Mkuu Watanzania wengi wangapi? Mwaka 2010 Watanzania tulikuwa wangapi kwa makadirio? na ni Watanzania wangapi tulipiga kura? Je ni Watanzania wangapi waliopia kura CCM? Mwisho ni Watanzania wangapi ambao wahakupiga kura? Na unadhani ni kwa nini hawakupiga kura?
kwanini uende mbali kote huko 2010,kwanini usiende mwaka jana tu hapo kwenye uchaguzi wa local government ambako ndiko waliko wapiga kura na watanzania wote,jiulize wangapi waliikataa chadema licha ya jitihada za m4c na wangapi waliikataa ccm kwa jitihada za Nape tu,utaelewa ni watz wangapi bado wanaiamini ccm,acheni kudanganyana na wingi wenu humu jf,huko site wigo wenu wa watu wanaowakubali ni mwembamba sana!
 
Back
Top Bottom